Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,989
- 3,692
Kwenye vyakula watanzania wanakula Nyani nenda ngoro ngoro pia kuna mnyama jamii ya Nyani anaitwa Kima analiwa na baadhi ya watu mkoa wa Kilimanjaro.Hili nimeliona kwamba sisi tuko tofauti sana na Waafrika wa nchi nyingine kitabia, sisi tumestaarabika sana ikilinganishwa na Waafrika wa nchi nyingine na hapa naongelea Waafrika weusi tuishio Kusini mwa Sahara!
Na hili utaliona karibia kila mahali kwamba tunawazidi Waafrika wengine sana kuanzia kwenye ustaarabu, vyakula tunavyokula, ni sisi watanzani pekee ndiyo tunaokula vyakula vya maana yaani hatuli vyakula vya ajabu ajabu kama Waafrika wengine kwa mfano Kongo wanakula Nyani na Sokwe kwetu hatuli, ukienda Afrika Magharibi kuanzia Kameruni mpaka Nigeria huko wanakula Kono kono, Mende, miti shamba na mizizi ya ajabu ajabu kwetu hatuli wanyama wa ajabu ajabu Tanzania tunakula nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, Kuku, Kondoo baadhi Nguruwe, samaki lkn pia siyo wa aina zote kuna Samaki wengine Watanzania hatuli na tunachagua!
Ukija kwenye swala tu la maisha ya kila siku, Waafrika wengi hawawezi kusema tafadhali, asante, samahani, nakupenda, uniwie radhi, kwa heri ya kuonana, maneno ya kistaarabu kama haya hawana kwenye Misamiati yao kwa mfano ukienda Kenya ni kawaida mtu hata asiyekujua kukwambia we kuja hapa, sasa Mtanzania hawezi kusema hivi bali tutasema kistaarabu na kiheshima samahani nakuomba uje, sasa ni kwa nini tuko tofauti na Waafrika wengine?
Utaona hata mambo ya uhalifu ingawaje ni kweli kwamba tuna uhalifu Tanzania lkn ukilinganisha na nchi nyingine za Kiafrika Tanzania yetu ni Paradiso, kuna nyumba nyingi sana Tz wala walinzi hazina na watu wanalala usingizi lkn nchi nyingine hili haliwekani, mimi huwa natembea mpaka saa kumi Alfajiri na poa kabisa sijawahi kutishiwa wala kukabwa, huko kwingenie Uhalifu ndiyo nyumbani...
Yaani sisi tumestaarabika zaidi klk Waafrika wengine wote niwajuwao, na hili hata sehemu zilizoendela kama AK nimefika huko Waafrika wa huko hawana ustaarabu kama wetu, Je kuna sababu maalumu kwamba sisi tuko tofauti na wao?
au imeandikwa kwenye vitabu vya Dini labda tumetabiriwa ...
Mbwaa analiwa na baadhi ya watu mkoani Iringa.
Panya nenda Lindi, Mtwara analiwa vizuri tena ni kitoweo pendwa. Kuhusu ustarabu sio kweli watanzania tu matapeli na tunaishi kiujanja ujanja kwani life style yetu sio original ni ya kuiga tu kwa wazungu na mitandao ndio maana siku izi neno nakupenda halitumiki kama neno I love you.