Kwanini waTanzania sio wazalendo!?

mimi ni mzawa haswa wa hii nchi!huenda nchi hii ilikuwa bora kabla sijazaliwa,hii ni kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kuona lolote la kufurahisha,hebu jiulize,ni raia wangapi wakimuona polisi au mtu yeyote mwenye wadhifa kwenye dola huogopa?kwanini iwe hivyo?
Tanzania ilikuwa bora na bado ni nchi bora hata sasa na itaendelea kuwa bora zaidi. Uzalendo ni asili ya m-Tanzania, popote ulipo jivunie nchi yako. Tanzania ndio nchi bora zaidi kwa kila m-Tanzania mzalendo. Usikubali mtu aitukane nchi yetu Tanzania.
 
hakutakuwa na uzalendo kama hakutakuwa na viongozi wazalendo...
angalia swala la madini toka mwaka 98! na hapo kuna mambo kedekede tu rushwa,ubinafsi,upindishwaji wa sheri + sheria kutofuatwa,ukandamizaji wa maskini... hlf uje uniambie niwe mzalendo! utanisaidia nini huo uzalendo mahali pasipo na wazalendo..?

huku mtaani mimi nijifanye mzalendo huko majuu wanapiga mpunga tu wa maana huo utakuwa uzalendo au uboya!
mkuu kawafundishe viongozi kwanza kuwa wazalendo hlf ndo uje kwetu ndo itakuwa rahisi maana kama nikujisifia nitajisifu kwani nchi itakuwa na wazalendo ambao najua zile sifa mbaya zitakuwa zimekoma! hivyo nitakuwa mzalendo hata kuipeperusha bendera ya nchi yangu kwani najua kodi yangu,kiwanja changu vipo salama,huduma za kijamii zipo gud everything kipo gud.. hapo nisipoipeperusha bendera yangu nitastahili kuitwa gaidi!
KENZY vyote ukivyovitaja hapo vinafuraha sana endapo uzalendo utakya ndani ya kila mTz swala tufanyeje!! Turudishe uzalendo kwa kizazi hiki na kijacho
 
Tanzania ilikuwa bora na bado ni nchi bora hata sasa na itaendelea kuwa bora zaidi. Uzalendo ni asili ya m-Tanzania, popote ulipo jivunie nchi yako. Tanzania ndio nchi bora zaidi kwa kila m-Tanzania mzalendo. Usikubali mtu aitukane nchi yetu Tanzania.
Si kwamba watu tunaichukia hii nchi!bali walioshika hatamu za uongozi ndio tunawachukia hasa!naamini hakuna mtanzania ambaye atamvumilia mtu yeyote aitukane nchi hii!mapenzi na nchi yapo kwa karibu kila mtu.
 
Ukishaathiriwa na siasa za vyama utaona uzalendo haupo, ila uzalendo upo. Tunaipenda Tanzania bila kujali siasa za nchi zikoje kwa sababu ndio nchi yetu. Silaha ya kukomesha upumbavu wa wanasiasa ni kuwa mzalendo tu. Popote ulipo jivunie u-Tanzania, waambie watu wewe ni m-Tanzania, tembea kifua mbele. Tuna mlima mrefu wa kipekee mlima Kilimanjaro, tuna mbuga kubwa za wanyama, tuna maziwa na bahari, tuna ardhi ya kututosha yenye rutuba, tuna mito na hifadhi kubwa za misitu nk. Hakuna kama Tanzania, uzalendo ndio asili yetu. Proud TANZANIA.
Je katika harakati zako za kimaisha umezungukwa na kundi gani!? Viongozi wazalendo,vijana wazalendo au wazalendo binafsi naona hakuna hicho kitu nchini kwetu kimekosekana kabusa
 
Huo mlima umekufaidisha nini wewe binafsi?bahari na maziwa yamekufaidisha nini?kama hakuna ndugu yako ambaye aliwahi/ni kiongozi serikalini sahau kunufaika na hivyo vitu!mfano mzuri hebu angalia chuo cha usimamizi wa wanyama pori namna ada zao zilivyo kubwa,unafikiri wamemlenga mtoto wa masikini wa nchi hii?
Upendo wa maslahi sio upendo wa kweli. Hatuwezi kuacha kuwa wazalendo kwa sababu hatufaidiki na tulivyonavyo. Kama kuna wanaosababisha kwa makusudi tusinufaike basi ni uzalendo pekee ndio utakaowatokomeza hao wahujumu na si vinginevyo.
 
Huo mlima umekufaidisha nini wewe binafsi?bahari na maziwa yamekufaidisha nini?kama hakuna ndugu yako ambaye aliwahi/ni kiongozi serikalini sahau kunufaika na hivyo vitu!mfano mzuri hebu angalia chuo cha usimamizi wa wanyama pori namna ada zao zilivyo kubwa,unafikiri wamemlenga mtoto wa masikini wa nchi hii?
Wewe tunaongea lugha moja
 
Na mwalimu mkuu duniani ni familia,huko utajifunza kuwajibika,kuheshimu,kujali,kuona haya,kuthamini, kutunza na karibu kila kitu. Bila hayo hakuna uzalendo. Mama anapiga hela ya ada,baba anapiga pato la familia na mtoto anakuwa muongomuongo tu..
Mkuu nini kifanyike
 
Tanzania ilikuwa bora na bado ni nchi bora hata sasa na itaendelea kuwa bora zaidi. Uzalendo ni asili ya m-Tanzania, popote ulipo jivunie nchi yako. Tanzania ndio nchi bora zaidi kwa kila m-Tanzania mzalendo. Usikubali mtu aitukane nchi yetu Tanzania.
Je unafikiri viongozi wako ni wazalendo!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom