Kwanini waTanzania sio wazalendo!?

Very hurting but unafikiri kipo chama kinachoweza kuokoa Taifa kutoka kwenye huu uzandiki !? Je nini kifanyike sote tufaidike hasa watoto wetu wafurahie matunda ya mbegu njema
Ishu siyo chama tu,mdudu anayeitwa demokrasia ndiye adui namba moja,huyu mdudu ndo analeta mgawanyiko kati ya raia wa nchi hii,watu wanatambuana kwa itikadi za vyama.Mzungu alitushika pabaya sana.Kwenye uchaguzi tu nchi inapoteza mabilioni ya pesa kuchagua watu wasiokuwa na hata chembe ya kujua lipi lenye manufaa kwa wananchi,kazi ndiooo!ndiooo!kwa kila jambo,na kugonga meza tu,wengine kuzunguka zunguka kwenye viti,nina hasira sana aisee!
 
Unafikiri nini kifanyike!?
Uzalendo ni swala mtambuka,kwanza ujipende na ujitambue . Uijue nchi yako na uithamini.Uheshimu sheria zake na watu wengine uwajali. Sasa kama mtu anatamani kuzaliwa mbwa ulaya ni wazi hajitambui na hutegemei uzalendo kwake.
Chakufanya hapa turekebishe aina ya elimu tunayopeana,iwe ya kutuwezesha kumudu mazingira yetu siyo kufaulu tu mtihani. Hakuna kitu kinachoitwa maana duniani,kila kitu ni fursa. Kukosea ni fursa ya kujifunza.
 
Wewe utakuwa ni muhamiaji haramu. Tanzania ndio nchi bora kabisa katika dunia hii. Wazalendo tunajivunia kuwa na nchi kubwa yenye kila kitu kizuri. Proud Tanzania. Hakuna kama Tanzania.
mimi ni mzawa haswa wa hii nchi!huenda nchi hii ilikuwa bora kabla sijazaliwa,hii ni kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kuona lolote la kufurahisha,hebu jiulize,ni raia wangapi wakimuona polisi au mtu yeyote mwenye wadhifa kwenye dola huogopa?kwanini iwe hivyo?
 
hakutakuwa na uzalendo kama hakutakuwa na viongozi wazalendo...
angalia swala la madini toka mwaka 98! na hapo kuna mambo kedekede tu rushwa,ubinafsi,upindishwaji wa sheri + sheria kutofuatwa,ukandamizaji wa maskini... hlf uje uniambie niwe mzalendo! utanisaidia nini huo uzalendo mahali pasipo na wazalendo..?

huku mtaani mimi nijifanye mzalendo huko majuu wanapiga mpunga tu wa maana huo utakuwa uzalendo au uboya!
mkuu kawafundishe viongozi kwanza kuwa wazalendo hlf ndo uje kwetu ndo itakuwa rahisi maana kama nikujisifia nitajisifu kwani nchi itakuwa na wazalendo ambao najua zile sifa mbaya zitakuwa zimekoma! hivyo nitakuwa mzalendo hata kuipeperusha bendera ya nchi yangu kwani najua kodi yangu,kiwanja changu vipo salama,huduma za kijamii zipo gud everything kipo gud.. hapo nisipoipeperusha bendera yangu nitastahili kuitwa gaidi!
 
Uzalendo ni swala mtambuka,kwanza ujipende na ujitambue . Uijue nchi yako na uithamini.Uheshimu sheria zake na watu wengine uwajali. Sasa kama mtu anatamani kuzaliwa mbwa ulaya ni wazi hajitambui na hutegemei uzalendo kwake.
Chakufanya hapa turekebishe aina ya elimu tunayopeana,iwe ya kutuwezesha kumudu mazingira yetu siyo kufaulu tu mtihani. Hakuna kitu kinachoitwa maana duniani,kila kitu ni fursa. Kukosea ni fursa ya kujifunza.
Ni kweli binafs ningefurahia kama hii kitu ingeanzia ngazi ya familia
 
Uzalendo ulikufa siku maslahi ya chama (Ccm) yakiwekwa mbele zaidi ya utaifa. Nyerere ndie aliua uzalendo wa watanzania kwa kukiinua chama badala ya taifa.
Ukishaathiriwa na siasa za vyama utaona uzalendo haupo, ila uzalendo upo. Tunaipenda Tanzania bila kujali siasa za nchi zikoje kwa sababu ndio nchi yetu. Silaha ya kukomesha upumbavu wa wanasiasa ni kuwa mzalendo tu. Popote ulipo jivunie u-Tanzania, waambie watu wewe ni m-Tanzania, tembea kifua mbele. Tuna mlima mrefu wa kipekee mlima Kilimanjaro, tuna mbuga kubwa za wanyama, tuna maziwa na bahari, tuna ardhi ya kututosha yenye rutuba, tuna mito na hifadhi kubwa za misitu nk. Hakuna kama Tanzania, uzalendo ndio asili yetu. Proud TANZANIA.
 
Ishu siyo chama tu,mdudu anayeitwa demokrasia ndiye adui namba moja,huyu mdudu ndo analeta mgawanyiko kati ya raia wa nchi hii,watu wanatambuana kwa itikadi za vyama.Mzungu alitushika pabaya sana.Kwenye uchaguzi tu nchi inapoteza mabilioni ya pesa kuchagua watu wasiokuwa na hata chembe ya kujua lipi lenye manufaa kwa wananchi,kazi ndiooo!ndiooo!kwa kila jambo,na kugonga meza tu,wengine kuzunguka zunguka kwenye viti,nina hasira sana aisee!
Unafikiri ilo ndio tatizo kuu!?
 
Ukishaathiriwa na siasa za vyama utaona uzalendo haupo, ila uzalendo upo. Tunaipenda Tanzania bila kujali siasa za nchi zikoje kwa sababu ndio nchi yetu. Silaha ya kukomesha upumbavu wa wanasiasa ni kuwa mzalendo tu. Popote ulipo jivunie u-Tanzania, waambie watu wewe ni m-Tanzania, tembea kifua mbele. Tuna mlima mrefu wa kipekee mlima Kilimanjaro, tuna mbuga kubwa za wanyama, tuna maziwa na bahari, tuna ardhi ya kututosha yenye rutuba, tuna mito na hifadhi kubwa za misitu nk. Hakuna kama Tanzania, uzalendo ndio asili yetu. Proud TANZANIA.
Huo mlima umekufaidisha nini wewe binafsi?bahari na maziwa yamekufaidisha nini?kama hakuna ndugu yako ambaye aliwahi/ni kiongozi serikalini sahau kunufaika na hivyo vitu!mfano mzuri hebu angalia chuo cha usimamizi wa wanyama pori namna ada zao zilivyo kubwa,unafikiri wamemlenga mtoto wa masikini wa nchi hii?
 
Ni kweli binafs ningefurahia kama hii kitu ingeanzia ngazi ya familia
Na mwalimu mkuu duniani ni familia,huko utajifunza kuwajibika,kuheshimu,kujali,kuona haya,kuthamini, kutunza na karibu kila kitu. Bila hayo hakuna uzalendo. Mama anapiga hela ya ada,baba anapiga pato la familia na mtoto anakuwa muongomuongo tu..
 
mimi ni mzawa haswa wa hii nchi!huenda nchi hii ilikuwa bora kabla sijazaliwa,hii ni kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kuona lolote la kufurahisha,hebu jiulize,ni raia wangapi wakimuona polisi au mtu yeyote mwenye wadhifa kwenye dola huogopa?kwanini iwe hivyo?
Nilijua ni peke angu tu kumbe tuko wengi aisee
 
mimi ni mzawa haswa wa hii nchi!huenda nchi hii ilikuwa bora kabla sijazaliwa,hii ni kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kuona lolote la kufurahisha,hebu jiulize,ni raia wangapi wakimuona polisi au mtu yeyote mwenye wadhifa kwenye dola huogopa?kwanini iwe hivyo?
Kwaiyo swala linaweza kuwa mfumo mbovu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom