Akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma, Kikwete alitoa kauli yenye maana, busara, inayoelekeza na inayobeba ujumbe mkubwa kwa rais kuzingatia hali inavyokwenda nchini. Alisema "WATU WENGINE HAWARIDHIKI NA MAMBO YANAVYOKWENDA. WENGINE WANASEMA NI MKALI SANA NA HAWAELEWI STYLE YAKE. LAKINI MI NASEMA NI MTU MAKINI ATAPIMA NA KUREKEBISHA".
Kama kawaida ya tabia ya watanzania na magazeti yetu tukatafuta headline za vijembe na mipasho. Tukaandika MIKIA iliyokatika, mipasho ya mzee Makamba kwa Askofu Gwajima, story za wazee waliofilisika kisiasa (Mzee wa Njii hii na Mzee wa Mapesa). Tukaacha busara kama hii ya mtu anayeondoka kwa mtu anayebaki na aliyekiri siku hiyo hiyo kwamba si mvumilivu.
Hivi nani anapenda minyukano inayoendelea na kuifanya nchi ionekane iko kwenye hali tete? Hivi kweli sote hatukusikia kauli hiyo? Au hatukuiona ya maana? Hivi mlitaka Kikwete atumie kauli gani kuonyesha na yeye haridhiki na mambo yanavyokwenda? Mlitaka atoe kauli kavu kama za huyu mwingine?