Kwanini watanzania, Magufuli na vyombo vyote vya habari havikuisikia kauli hii ya Kikwete?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma, Kikwete alitoa kauli yenye maana, busara, inayoelekeza na inayobeba ujumbe mkubwa kwa rais kuzingatia hali inavyokwenda nchini. Alisema "WATU WENGINE HAWARIDHIKI NA MAMBO YANAVYOKWENDA. WENGINE WANASEMA NI MKALI SANA NA HAWAELEWI STYLE YAKE. LAKINI MI NASEMA NI MTU MAKINI ATAPIMA NA KUREKEBISHA".

Kama kawaida ya tabia ya watanzania na magazeti yetu tukatafuta headline za vijembe na mipasho. Tukaandika MIKIA iliyokatika, mipasho ya mzee Makamba kwa Askofu Gwajima, story za wazee waliofilisika kisiasa (Mzee wa Njii hii na Mzee wa Mapesa). Tukaacha busara kama hii ya mtu anayeondoka kwa mtu anayebaki na aliyekiri siku hiyo hiyo kwamba si mvumilivu.

Hivi nani anapenda minyukano inayoendelea na kuifanya nchi ionekane iko kwenye hali tete? Hivi kweli sote hatukusikia kauli hiyo? Au hatukuiona ya maana? Hivi mlitaka Kikwete atumie kauli gani kuonyesha na yeye haridhiki na mambo yanavyokwenda? Mlitaka atoe kauli kavu kama za huyu mwingine?
 
Kumbe alisema ATAPIMA NA KUREKEBISHA! Haya tuone kama atarekebisha.
 
kikwete alivyoingia na yale majina matano mfukoni alitegemea nini?he brought this on us,bad or good,he is a part of what is going on.
Najua aliingia nayo lakini kwa maono yake kwamba hawezi halikuwa chaguo lake
 
Kikwete alisema tutamkumbuka na tutasema bora utawala wake na hili nazidi kuliona sasa hivi.Bora Kikwete angetawala hata kwa miaka kumi zaidi kuliko hali hii tunayoenda nayo sasa hivi.Mzee alikuwa anajua jinsi kuzimudu temper za wapinzani lakini leo hii mtu akikosolewa anahisi kama anataka kupokwa utawala wake. Hiyo kauli ilikuwa na maana kubwa sana aliposema kuwa jamaa atapima na kurekebisha ila waandishi wetu hawakuitilia maanani ndio maana haikutiliwa mkazo na yoyote yule.

TIME WILL TELL
 
Waandishi wetu bhana!
 
Pamoja na madhaifu lakini alikuwa bora angalau
 
Kaka waTz ni waswahili na uswahili ni sehemu ya maisha yao , kwao (waTz) vioja vya Makamba na Cheyo yalikuwa big deal . Bahati mbaya kabisa nchi hii hatukuwahi kujua kuwa siku moja tutatofautiana kiitikadi na hata ki katiba. Leo hii hakuna tafsiri nzuri ya nani anayevunja au hata kukanyaga katiba. TUNGEKUWA NA MAHAKAMA YA KI KATIBA
 
Tumepitwa na usemi wa kale sana usemao "hutoijua thamani ya kitu kabla ya kukitupa jalalani na mwenye kuijua thamani halisi kukiokota na kukipa thamani yake halisi". Historia ya amani na utangamano wa taifa hili haitamwandika vibaya Kikwete. Perception yetu ilitugawa lakini uhalisia na hekima yake ya kuruhusu uhuru wa kusema na kusikika uliturudisha na kutufanya wamoja tena kama taifa. Mara nyingi mbwa ang'atae habweki na hii ndiyo tunayoumbiwa sasa kuwa tung'ate bila kubweka. Tukifika huko kurudishwa kwenye kubweka kabla ya kung'ata itatuchukua miongo miwili na zaidi.
Kaeni, zungumzeni na kubalianeni mbinu bora za kuondoa hizi sintofahamu zinazolikabili taifa kwa sasa. Ubabe na vitisho huzoeleka haraka kuliko na mwisho wa siku vyote hivyo hupuuzwa sana. Rejeeni pambano la Daud na Goliati au Musa na Farao. Twapata dhima yao katika maisha ya leo na kesho? Kikwete was a man of people and he still be.
 
Ni kweli kuwa hujaielewa hiyo kauli ama umeamua kwa makusudi kupotosha tu ukweli? Hayo maneno ya kikwete ni ujumbe kwa magufuli au ni ujumbe kwa watu kama nyinyi kutwa kumsema maguful? Aiseee
 
Akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma, Kikwete alitoa kauli yenye maana, busara, inayoelekeza na inayobeba ujumbe mkubwa kwa rais kuzingatia hali inavyokwenda nchini. Alisema "WATU WENGINE HAWARIDHIKI NA MAMBO YANAVYOKWENDA. WENGINE WANASEMA NI MKALI SANA NA HAWAELEWI STYLE YAKE. LAKINI MI NASEMA NI MTU MAKINI ATAPIMA NA KUREKEBISHA".

Kama kawaida ya tabia ya watanzania na magazeti yetu tukatafuta headline za vijembe na mipasho. Tukaandika MIKIA iliyokatika, mipasho ya mzee Makamba kwa Askofu Gwajima, story za wazee waliofilisika kisiasa (Mzee wa Njii hii na Mzee wa Mapesa). Tukaacha busara kama hii ya mtu anayeondoka kwa mtu anayebaki na aliyekiri siku hiyo hiyo kwamba si mvumilivu.

Hivi nani anapenda minyukano inayoendelea na kuifanya nchi ionekane iko kwenye hali tete? Hivi kweli sote hatukusikia kauli hiyo? Au hatukuiona ya maana? Hivi mlitaka Kikwete atumie kauli gani kuonyesha na yeye haridhiki na mambo yanavyokwenda? Mlitaka atoe kauli kavu kama za huyu mwingine?
Umenigusa! Hivi tunaweza kupata wapi
hotuba hiyo ya JK tuisome tena na kutafakari! Kauli hiyo kama aliitoa kweli ina maana kubwa sana, ni kama alikuwa anampa JPM ujumbe kwenye mabano kwamba "jirekebishe"! B4 its too late!
 
Kikwete alisema tutamkumbuka na tutasema bora utawala wake na hili nazidi kuliona sasa hivi.Bora Kikwete angetawala hata kwa miaka kumi zaidi kuliko hali hii tunayoenda nayo sasa hivi.Mzee alikuwa anajua jinsi kuzimudu temper za wapinzani lakini leo hii mtu akikosolewa anahisi kama anataka kupokwa utawala wake. Hiyo kauli ilikuwa na maana kubwa sana aliposema kuwa jamaa atapima na kurekebisha ila waandishi wetu hawakuitilia maanani ndio maana haikutiliwa mkazo na yoyote yule.

TIME WILL TELL
YOU NEVER KNOW,PENGINE ZILE HAMSINI NA NANE HAZIKUWA ZAKE..
 
Huyu hawezi kupima na kujirekebisha ndiyo maana vyombo mbalimbali vya habari havikuipa uzito kauli hiyo, kwanza sidhani kama aliulewa ujumbe wenyewe
 
Akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma, Kikwete alitoa kauli yenye maana, busara, inayoelekeza na inayobeba ujumbe mkubwa kwa rais kuzingatia hali inavyokwenda nchini. Alisema "WATU WENGINE HAWARIDHIKI NA MAMBO YANAVYOKWENDA. WENGINE WANASEMA NI MKALI SANA NA HAWAELEWI STYLE YAKE. LAKINI MI NASEMA NI MTU MAKINI ATAPIMA NA KUREKEBISHA".

Kama kawaida ya tabia ya watanzania na magazeti yetu tukatafuta headline za vijembe na mipasho. Tukaandika MIKIA iliyokatika, mipasho ya mzee Makamba kwa Askofu Gwajima, story za wazee waliofilisika kisiasa (Mzee wa Njii hii na Mzee wa Mapesa). Tukaacha busara kama hii ya mtu anayeondoka kwa mtu anayebaki na aliyekiri siku hiyo hiyo kwamba si mvumilivu.

Hivi nani anapenda minyukano inayoendelea na kuifanya nchi ionekane iko kwenye hali tete? Hivi kweli sote hatukusikia kauli hiyo? Au hatukuiona ya maana? Hivi mlitaka Kikwete atumie kauli gani kuonyesha na yeye haridhiki na mambo yanavyokwenda? Mlitaka atoe kauli kavu kama za huyu mwingine?
Hiyo ni kauli nzito sana.. Kama kweli yule mzee wa magogoni hatabadilika cjui...??
 
Kikwete alisema tutamkumbuka na tutasema bora utawala wake na hili nazidi kuliona sasa hivi.Bora Kikwete angetawala hata kwa miaka kumi zaidi kuliko hali hii tunayoenda nayo sasa hivi.Mzee alikuwa anajua jinsi kuzimudu temper za wapinzani lakini leo hii mtu akikosolewa anahisi kama anataka kupokwa utawala wake. Hiyo kauli ilikuwa na maana kubwa sana aliposema kuwa jamaa atapima na kurekebisha ila waandishi wetu hawakuitilia maanani ndio maana haikutiliwa mkazo na yoyote yule.

TIME WILL TELL
Sina uhakika kama unajua unachoongea. Hao Tembo si wangeisha huko mbugani? Kuna dili zilikuwa zinapigwa nchi hii za hatari. Kuna ishu ya deni la taifa karibu pesa zote hazikutumika kwenye miradi ya maendeleo zimeisha kufanya matumizi. Hizo hela tutazilipaje? Jionee huruma wewe na kizazi chako. Katika maisha ukitaka kupata chochote kizuri lazima ukubali kuumia. Raisi hana hata miaka miwili madarakani mnaongea ushuzi.Watu wanakopa kwa ajili ya matumizi. Tunakopa kufanya starehe yaani hiyo lazima tungefika mahali tusingekopesheka tena na ndo mgeanza kuona uchungu wa nchi kuendeshwa kama shamba la bibi. Hiyo hela zaidi ya trillion arobaini zilizokupwa ujiulize zipo wapi mbona hatujaona kitu tangible? Sasa unasema angeendelea miaka kumi ili aendelee kukopa na hela mzione mtaani ili deni la taifa lifike trillioni 100?? Hivi mnajua mnachoongea anu ni kuhemka tu muda wote. Nendeni hata nchi za watu mpate hata exposure ya kuwapa wivu wa maendeleo maana kwa uongeaji wako tu inaonekana tu unadhani maendeleo yanakuja kwa kupiga soga na kunywa kahawa.. Tunahitaji kwenda uchumi wa kati. Na ili twende uchumi wa kati zinahitajika reforms za hatari na lazima tutaumia tu. Tuna miaka michache ya ku hustle ila uelekeo ni mzuri sema vijana sababu hamna maono mnaona yanapoishia makende yenu tuu.
 
Back
Top Bottom