Kwanini wasomi wengi akili zao ni Madudu

switch Off

Member
Oct 30, 2019
48
186
Habari wakuu,

(R & L kwangu ni tatizo )

Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa Kitanzania ambae elimu yangu ni kidato cha nne, yaani nilifeli kidato cha nne.

Kwa sasa naishi maisha ya kawaida. Nimekuwa nikishangazwa sana na hawa binadamu ambao elimu zao zimefikia chuo.

Nimekuwa nikiwaajiri hawa viumbe katika kazi zangu lakini mambo wanayoyafanya naona ni bora nifanye kazi na kijana wa mtaani ambaye hana elimu yoyote lakini ana uelewa mzuri. Wamekuwa wanipa hasara na wamekuwa hawafanyi kazi vizuri kulingana na elimu yao.

Sasa Leo ndio nimeamini hawa viumbe ni madishi kabisa. Kuna kijana mpya ambae nimempa ajira ya muda mfupi kwa kipindi hiki cha corona "yeye ni mwanachuo wa UDOM"

Kwakuwa vyuo vimefungwa na kijana alikuwa anataka kufanya kazi na mimi nikaona sio mbaya acha nifanye nae kazi.

Tunavyofanya kazi, jioni huwa nampatia laptop ili kazi zingine akazifanyie nyumbani. Leo linanipigia simu eti nimepatwa na dharura ya ghafla nimesafiri kwaiyo nitarudi baada ya siku 4. Kibaya zaidi ameondoka na laptop, na ndani yake kuna kazi muhimu sana ambazo kabla ya hizo siku nne zinatakiwa ziwe tayari.

Ninacho jiuliza ni kwamba, huyu kiumbe alishindwa nini kurudisha PC ili watu wengine wafanye kazi.

Sina hofu kuwa anaweza kunitapeli PC "kijana sio tapeli na hawezi kufanya ivyo" ila ndio amekwamisha kazi zangu kwa uzembe wake.

Ndugu zangu naomba mniambie hawa viumbe kwanini akili zao hazieleweki.


NB Sipo kwaajili ya kuwatukana watu kama hawa.

Kuhusu Laptop.nimemwambia kesho anitumie Kweye basi ili ifike kabla ya yeye kurudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wewe ulitaka mtu akiwa msomi asikosee na akikosea basi anakuwa mjinga.
 
Back
Top Bottom