Matumizi ya akili

Tman900

Senior Member
May 30, 2017
175
345
Dar es Salaam watu Wanafanya kazi maeneo Mbalimbali.

Sehemu ambayo mtu anaishi na anakofanyia Harakati zake za kiuchumi anatumia usafiri kurudi Nyumbani.

Na Kila nikitazama Matukio ya watu kupigwa mtaani.

Kuna Dada anauza Miogo usiku kuazia saa Moja usiku mpaka saa 4.

Amepigwa ktk Mbavu. Na Kuna Kijana mwingine amepigwa kichwani Hali yake si nzuri, ingawa Baadhi ya watu wanasema kutoboa huu Mwaka Ni ngumu kwake, Huyo kijana Alikua anatoka kazi anashuka tu ktk Boda Boda kala kichapo Yeye na Boda Boda wake.

Kwa Maneno ya wagawa kichapo Ni kipigo mpaka Mwaka uishe.

Baada ya kuuliza kua Hao Waga Kichapo wanapiga watu kwa sababu gani jibu nikua mwenzao Ameibiwa simu.

Kwa uelewa wangu Mdogo Inamaana Hakuna Technology ya kuitafuta hiyo Simu zaidi ya kuathiri Maisha ya watu ambao Wala hawausiki.

#Hili Tatizo la kupiga watu Ni la miaka Mingi na Ni Kama mazoea.

Kwa Mtazamo wangu ingetakiwa Kua na maeneo maalu kwa ajiri yao. sisi makabwela tue na maeneo yetu kwa shughuri zetu.
Kusiwe na Muingiliano wa chochote.

* Makazi, sehemu za starehe usafiri. Ingependeza wakakaa wao Kama wao sisi Kivyetu. Hii itaondoa mazingira ya kupigwa mtu ambae Hata Tukio halijui anakula kichapo.

SWALI: Kwa watu mliowai kutembea mataifa Mengine nje ya Africa je Uko nako Soldger huwa wanapiga watu ikitokea kaibiwa Simu/ laptops, Saa nk.

Vipi kuhusu Technology Yao wanayoitumia kukabiliana na matukio.
 
Back
Top Bottom