Kwanini wanawake/wasichana wakishaolewa wanajisahau?

Kujisahau kupo kwa wote, na ukiona hayo yametokea jua hata wewe unamchango mkubwa kwalo, sema ndio vile makosa yote huwa ni ya wanawake!!
 
Jamani nina hoja fupi sana hapa, ni kwa nini wanawake/wasichana karibia wote wakishaolewa wanajisahau sana, yaani wanapunguza upendo na mumewe, wanaanza mambo ya kiburi,jeuri,dharau kibao, wanajibu hovyo hovyo.

Yaani kwa kifupi wana change na wanasahau kuwa walikua wanakesha wanasali na kwenda kwa waganga ili waolewe na wakiachwa sasa wataanza, oooh! nina mkosi, nimerogwa, kuna mkono wa mtu.
Aiseeee hivi kuolewa kwa sasa ni bahati? Imekuwa ajira nikeshe nasali nikiomba maana nikipata nitapata mshahara kila mwezi na utanisaidia kwa mambo mengi, sasa nikeshe kuomba kuolewa kuna faida gani zaidi ya kujiongezea majukumu? Wanaume wote wa Kiafrika wanataka wao kila kitu wafanyiwe , na sio kumfanyia mwanamke au kufanyiana na wakosoaji wazuri kwa kila kitu. Mbona unataka kumfanya mwanaume kama ni mtu wa kipekee sana mpaka watu wamwendee kwa mganga? Hayo uliyosema wanafanya wanawake wasiojiamini na maisha tu na sio vinginevyo,kuolewa kuolewa yaani imekuwa dili sana nini?
 
Si wote wasiojitambua labda wale wanaoa vitoto, ila wanawake wote wanaojitambua huwa hawajisahau majukumu yao kwa waume zao..!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom