Hii ni kwa wasichana ambao hawajaolewa

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Amani iwe kwenu wandugu!

Ningependa kuongea na dada na wadogo zangu ambao hawajaolewa ama kwasababu hawajabahatika tu kuolewa au bado muda wao haujafika lakini wana matarajio kwa siku za baadaye. Lengo la kuandika uzi huu ni kuwataka kuwa makini ili mwisho wa siku wasije wakajutia au kuanza kwenda kwa waganga au wachungaji kuombewa wapata waume.

Kwanza nianze na hili, ukifuatilia wale wasichana ambao kila jumapili wako kanisani huku nia zao kuu ni kumuomba Mungu awapatie mume bora, au kila mahubiri na semina lazima wahudhurie huku nia yao kuu ni kuomba wapate waume bora utagundua kwamba hao wadada kipindi fulani katika maisha yao ya usichana waliwahi kupendwa na mtu/ watu waliokuwa serious , wenye nia na malengo ya kuwaoa. Walio wengi walipendwa na watu kwa viwango vya juu sana, kuna wanaume walihangaika kwa ajili yao kwa nguvu , akili na moyo wote lakini waliambulia patupu.

Sitaki kusema hapa kwamba kila mwanaume anayekuja kwako kwamba anataka kukuoa anamaanisha au wewe umkubalie tu just kwasababu ameonesha njia. Sisemi hivi kwasababu unaweza kupendwa na mtu kwa nguvu nyingi lakini wewe kwakweli hujamkubali kulingana na vigezo vyako. Lakini shida ya wadada huwa moja na hili ndilo nataka nilizungumzie kwa kina.

Shida kubwa ya wadada hawa ni kwamba, wakati huo wanapendwa na wanaume wao huenda kwa kujua au kutokujua walishindwa kutambua kwamba Mungu hakupi siku zote uombacho bali hukupa kinachokufaa. Unaweza kuomba mwanaume mweupe mrefu mwenye six pack lakini Mungu anaona huyu atakuua kwa UKIMWI muda mfupi baada ya ndoa hivyo anakuletea mtu kama mimi Hamoragae. Kwahiyo wadada hawa kwa kuona huyo mtu hana sifa anazozihitaji basi wanajibu wanaume hao kwa jeuri na dharau ya hali ya juu. Hapa ndipo kiini cha tatizo yanini kumjibu mwanaume kwa maneno ya kashfa na dharau hata kama humpendi au hajakuvutia. Kwanini umdharau na kumjibu mwanaume majibu mabovu eti kwasababu kakutongaza au kwasababu amesema uwe mchumba wake na wewe ukaona hakufai?. Kwanini usimjibu tu majibu mazuri hata kama atakuwa king'ang'anizi ili mradi tu umuache kwa amani ya moyo?.

MAKOSA HAYA NDIYO KIGEZO CHA BAADHI YA WADADA KUSHINDWA KUOLEWA
1. Unakubaliana kutoka out na mtu wako au mtu aliyekuomba mtoke ili muweze kuongea machache lakini mkifika wewe na simu, simu na wewe. Mnatumia masaa mawili sehemu huku nisali zima unamaliza unachat na wengine awe shoga yako/ mama au ndg. Mara unachat, mara unapiga , mara hivi au vile yaani hutulii ukaweka mawazo yako kwenye mazungumzo yenu. Hata kama humtaki mtu just kuwa mpole kwa muda huo.
2. Umetoka out lakini stori zako ni za instagramu, facebook, na bongo fleva. Yaani huwezi kuongea vitu nje ya hapo. Ni mwanaume gani atakuona wa maana kama stori zako ni za akina Hamisa, Zari, Wema nk. Lazima mwanamke uwe presentable mbele za mwanaume. Ongea yako na matendo yako lazima yakuonesha unafaa kweli kuwa mke wa mtu.
3. Kupiga stori za familia zenu hasa zilizo tofauti na familia nyingi za kiafrika, tabia na mtindo wa maisha ya kwenu usipende kuyaweka mbele sana. Kama kwenu kuna magari, trekta au bombadier au wazazi wako wako hivi au vile au kama kaka /dada zako wako mbele huko kwa Trump si lazima uyaweke mbele unapokuwa unaongea na mwanaume.
4. Tabia ya kuomba omba na kutegemea mwanaume kwa kila jambo hata kama mwenyewe una uwezo. Wadada wengi wanapokuwa na wachumba au wapenzi basi huwafanya ndiyo suluhisho la matatizo yao. Mara babe leo sina hata nauli, babe sina voucher,babe natamani sausage leo, baby nimepungukiwa ada ya chuo, baby nguo zimeniishia, baby nikuambie kitu ....baby unajua ..hadi unakuwa kero.

Tabia hizi na nyingine humfanya mwanaume kukujua mapema kwamba hufai kuwa mke. Mwanamke gani hana stori za future life wewe stori zako ni za instagram, fb, bongo fleva na bongo movie. Ukienda mbali sana stori za kwenu na stori za rafiki zako na wapenzi wao. Ni mwanaume gani ataoa omba omba ambaye leo ana uhitaji hili ,kesho lile kesho kutwa lingine. Ni mwanaume gani ataoa mwanamke ana dharau ambaye uko naye huku akiwa anachat, mara apige , mara yuko instagram yaani hutulii mbele za mtu japo kwa dakika chache. Mwanaume gani ataoa mwanamke anayeishi jana yake yaani stori zako ni za wakati wa shule na chuo huko , mara ooh Mzumbe cjui Kamzora alikuwaje, mara Itika alikuwa hivi ,Namkumbuka Mbegalo au Haruni au UDSM ilikuwa hivi wakati nasoma, cjui fulani alikuwa na akili sana.

Namalizia kwa kusema , ili uweze kuolewa lazima ujiweke kwenye hali ya kuoleweka, lazima ujifunze kuanza kusihi maisha ya mtu ambaye yuko kwenye ndoa, lazima vaa yako, mwendo wako, majibu yako zifanane na mtu anayeishi kwenye ndoa. Usijione wewe ndiwe wewe kumbuka hata mama yako alikuwa kama ulivyo leo wakati fulani katika maisha yaKe.

SINA LENGO BAYA ZAIDI YA KUWAKUMBUSHA , NAWAHESHIMU SANA WANAWAKE AWE MDOGO AU MKUBWA MAANA NAJUA ROLE YAO KATIKA JAMII.
 
Back
Top Bottom