Fahamu kuhusu magonjwa ya kina mama yanayodhaniwa kuwa mapepo

musicarlito

Senior Member
Dec 29, 2020
176
289
Neno kuhusu magonjwa ya akinadada na akinamama;

"Magonjwa ya akinamama yameuchachafya ulimwengu tangu zamani sana"

Nadhani tumejipatia muda mrefuna wa kutosha kujadili mada iliyopita. Leo nawaleteeni nyingine kwamba kesi za magonjwa yanayowahangaisha zaidi akina dada na akinamama ni KESI ZA ZAMANI SANA, TENA ZAMANI MNO kuliko tunavyodhani wengi wetu.

Namaanisha hasa kesi za kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo. Yaani kitaalamu namaanisha nurosisi na hysteria.

Ilitosha akinadada na akinamama kulielewa vyema jambo hili na wao kukataa kutumiwa na wengine, hususan, akina baba “wenye hila” kama shamba la kuchumia matumbo yao. Unajua akinababa chungu nzima hujipatia kipato na riziki kwa kujitangaza na kuojinasibu kuweza kuwasaidia akinadada na akinamama katika matatizo yao ya afya.

Acha leo nikupitisheni katika historia upate kujua kwamba watu hawajaanza jana kuyashughulikia magonjwa hayo isipokuwa zamani sana. Nafanya hivi kwa sababu historia ni mwalimu. Historia huwaonesha watu walikotoka, walipo na wanakoweza kwenda. Basi, historia fupi ya magonjwa ya akinadada na akinamama ni hii ifuatavyo:

Enzi za Hippocrates
Ndugu zanguni, kesi za akinamama, si kwamba zimeanza katika karne yetu hii. Nimeshasema kwamba zina historia ya miaka mingi sana. Kumbe, tuwe macho tusisahaulishwe usomi wetu hasa wa ushauri kwa kadiri ya mwendo wa historia ulivyokwenda.

Ni hivi, kesi za akina mama zilijulikana na kuwatinga watu tangu enzi za akina Hippocrates, yaani hata kabla Yesu hajazaliwa. Hiyo ni katika Ugiriki au Uyunani. Wanaume yaliwatinga magonjwa ya akinamama ya kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo.

Kwa kitendawili hicho, Hippocrates alikuja na jawabu la aina yake. Yeye alidai akina mama wanaonesha magonjwa ambayo wanaume hawaoneshi kwa sababu walikuwa wanasumbuliwa na tumbo la uzazi (hystera) linalorandaranda miili mwao. Alisema walikuwa wanachanganyikiwa zaidi tumbo la uzazi linapofika kooni katika safari zake za kuhamahama mwilini mwa mwanamke. Hapo ndipo ulipozaliwa msamiati wa “hysteria”, kwa Kiswahili, umanyeto).

Kama unataka kuniuliza dalili za hysteria, naomba usijisumbue maana nakuletea sasa hivi. Dalili zake ni hizi: kuzimiazima, kukosa usingizi, kuchachatika mwili, kutokutulia , wasiwasi na msukumo au hamu ya kitendo cha ngono.

Hadi hapa nakupa muhtasari. Hippocrates ndiye aliyetoa jina “hystera” au “uterus”, yaani “tumbo la uzazi”. Neno “hytera” ndiyo iliyozaa jina “hysteria”. Alidai kwa kuwa linatembeatembea mwilini mwao na linapofika shingoni, wanawake huugua magonjwa ya ajabu kabisa, magonjwa ambayo wanaume hawaugui kwa vile hawana tumbo la uzazi. Ndipo bwana huyu alisema hysteria ni ugonjwa wa akinamama kwani ndio wenye tumbo la uzazi lenye kuwarabu.

Enzi za Aretaeus
Pite pite akaja Bw. Aretaeus. Kati yote aliyosema, kubwa ni kauli yake kwamba hysteria ni “mnyama ndani ya mnyama” yaani mwanamke. Kwa mtazamo wake alipendekeza kuwasaidia akinamama kwa dawa ya manukato mawili, ya kunukia vizuri kuwekwa chini ya sehemu za siri na ya kunuka au kuchoma kumnusisha mwanamke puani kusudi mwanamke anayetibiwa akipiga chafya tumbo la uzazi literemke na kurudi mahali pake.

Basi, ndivyo walivyokuwa wanatibiwa wanawake waliokuwa wanaweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo.

Enzi za Galen na Wenzake
Katika karne ya pili, Baada ya Kristo, wakaja watu kama akina Galen walioendeleleza matibabu ya kuwawekea akinamama wagonjwa manukato mawili, yale ya chini ya via vya uzazi na ya kunuka puani ili wakipiga chafya tumbo la uzazi literemke na kurudi sehemu yake.

Pamoja na dawa hiyo Bw. Galen akaongeza upakaji mafuta juu ya sehemu za siri pamoja na “kulala nao” kwa vile aliamini walikuwa wahangaishwa na kukosa msisimko wa tendo la ndoa, hususan, wagonjwa waliokuwa wajane na wale wasioolewa pamoja na wanawake tasa. Lakini sikiliza vyema, huko “kulala nao” alikuwa anawaagiza wasaidizi wake wafanye.

Kimuhtasari, katika karne ya pili, B.K., Bw. Galen alisema hysteria inawasumbua wanawake wasioolewa, wasioozaa pamoja na wajane ambao walizoea tendo la ndoa lakini kwa wakati huo walikuwa wanalikosa (“wanalimiss”) na wao kusumbuliwa na hamu kubwa. Bw. Galen alipendekeza dawa ya aina yake ndiyo kuwapaka akinamama wagonjwa mafuta sehemu za siri, na kwa kupitia wasaidizi wake kuwafanyia tendo la ndoa.

Enzi za Karne za Kati
Katika enzi za kati, yaani karne 5-15 B.K., ikaongezwa sababu nyingine moja, ndiyo “kupagawa na mapepo”. Kufuatia sababu hii, shughuli za uwingaji pepo zikapamba moto sana. Kifupi, katika karne za kati (karne 5-15 B.K.) iliongezwa sababu moja kupagawa na mapepo. Ndipo dawa ikaongezwa pia yaani kuwinga pepo (exorcism).

Enzi ya Karne 16-17
Katika karne ya 16-17, ziliongezwa sababu mbili mpya, mosi, kuwako kwa majimaji kwenye tumbo la uzazi na pili, kukosa tendo la ndoa. Kwa kufuatia sababu hizo ile dawa ya “kulala nao” wagonjwa ili kuwapa raha ilishika chati ya aina yake.

Enzi za Sigmund Freud
Katika karne ya 19, alikuja daktari wa madawa, Bw. Sigmund Freud (1856-1939). Mtu huyu wa pekee alikuja na nadharia ya “tatizo la Oedipus” na “libido”. Kwa tatizo la Oedipus alisema watoto huwaelekea wazazi wa jinsia tofauti, binti humwelekea baba, na mtoto wa kiume humwelekea mama. Kwa dhana ya “libido” akidai wanadamu, yaani pamoja na akinamama, walikuwa wanahangaishwa na kukosewa kwa nguvu za uzazi katika utoto wao.

Kwa maoni hayo akapendekeza kuwasaidia akinamama kwa kuzungumza nao kusudi kujua lini mambo yalipowaendea mrama. Mwenyewe alikuwa akikaa na wagonjwa wachache kwa kusudi la kuwasaidia na wakati huo huo kuwafanyia utafiti.

Kwa yale aliyokuwa akiyagundua akatoa hotuba tano ambazo zilihudhuriwa na watu wachache sana kwani alikuwa akipuuzwa. Kwa kweli, watu wengi walimpinga na kumpuuza lakini watu wachache kama akina Carl Jung walimuunga mkono.

Kwa vyovyote ilivyokuwa, Sigmund Freud ndiye baba wa elimu ya kutibu magonjwa kwa mpambanuo wa kisaikolojia (psychoanalysis). Huu ndio msingi wa namna nyingi za kisasa za kuwasaidia akinamama wanaoweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu yao.

Kimuhtasari, katika karne ya 19 alitokea Daktari Sigmund Freud akatoa sababu ya “Oedipus complex” na “libido” na akaanzisha pia utafiti wa nafsi (psychoanalysis).

Enzi za Leo
Hapa Afrika, tumeingia sisi. Namaanisha sisi zamu yetu ndiyo siku hizi. Kwa kweli sisi hatuna jibu lenye mashiko kwa tatizo la akinamama kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo.

Hata hivyo, kitu cha kushangaza ni kwamba wengi wetu tumejichimbia kwenye sababu ya mapepo na kupagawa tu huku tukisahau kabisa nyenzo za kiushauri na mipambanuo ya kisaikolojia (psychoanalysis). Mimi nawasihini kwa heshima na taadhima, tutaalamike japo kidogo. Haiwezekani kesi za binti zetu, dada zetu na mama zetu, kwa wingi wake wote huo kuwa ni kupagawa na mapepo. Haiwezekani, nakataa.

Wewe jiulize tu, kwa nini Shetani awarabu wao zaidi? Tuseme Shetani anawaogopa wanaume? Zaidi ya hayo, “wanawake wanaosemekana kupagawa” wengi wao ni wenye rangi nyeusi. Sasa mambo yanapokuwa hivyo tangu lini Shetani akawa moto wa kuotea mbali kwa akinamama yaani kwa Kiingereza “womanizer?” Kumbe, nawasihini, ndugu zangu tusiwe watu wa nyuma hivi.

Tufunguke macho lau kidogo! Ni karne ya ishirini na moja hii. Ebu tutilie pia maanani utaalamu maana maarifa na elimu ya kisasa ni pia karama zitokazo kwa Roho Mtakatifu. Tusidharau utaalamu na weledi, kwa kufanya hivyo tunamkufuru Roho Mtakatifu aliye nyuma ya pazia.

Hitaji la Elimu ya Saikolojia na Ushauri
Elimu ya Saikolojia inahitajika sana siku hizi. Kwa hili, mimi nawaaseni nyote. Si vizuri ulimwengu uende mbele katika elimu na sisi hapa barani Afrika tuishi kwa elimu kama ya waganga wa kienyeji. Wakati umebadilika na sisi tubadilike. Hii ni karne ya sayansi na teknolojia.

Nazisihi seminari zetu ziongeze nguvu katika masomo ya Saikolojia na Ushauri Nasaha. Kishapo, majimbo yetu yafikirie kuwa na mapadre mabingwa wa Saikolojia na Ushauri Nasaha kusudi kesi zingine zinazosemekana kuwa za kupagawa ziangaliwe vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo nyingi zinatiwa katika kapu la kazi ya Shetani pasipo hata tafakari na utafiti.

Wengi wanaojitosa katika kuwasaidia akinamama wanaoweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo, wanakimbilia kusema ni kupagawa na mapepo au pengine “majini” kwa fikra za Kiislamu na hivyo kuwa na dawa mbili: kuwamwagia wagonjwa maji ya baraka na kukemea.

Hapo hapo wapo wengine wanathubutu kuwapaka akinamama mafuta kwenye sehemu za siri kama walivyokuwa wanafanya akina Galen. Lakini, kwa jinsi hali ya hewa inavyokwenda, nadhani bado kama inchi moja hivi wengine waende kwenye suluhisho la “kulala na wagonjwa” kama zama za kale. Ole wetu tufikie hapo tena!

Lakini Kesi Nyingi si Mapepo
Nina hoja nzito. Kesi za watu kupagawa, hususan, kati ya Wakristo LAZIMA ziwe chache sana kwa sababu Kristo amemshinda Shetani kwa niaba yetu. Mmoja (Shetani) aliyeshindwa hawezi kuwa na nguvu au kutamba kama kwanza.

Jambazi aliyevunjwa kiuno hawezi kuwa jeuri kama kabla hajavunjwa kiuno. Kumbe, siku hizi, ndiyo enzi za Agano Jipya, tukidai kwamba Shetani ana nguvu sana, labda eti “amejiinua” tunaikufuru kazi ya Kristo kwa sababu tutakuwa tunamaanisha kazi yake haikuwa na mapato yoyote ya maana, jambo ambalo si kweli.

Hivi kesi nyingi ni za kisaikolojia au tuseme ni magonjwa tunayoyakosea kwa kudhani ni mapepo. Magonjwa tunayoyakosea na kudhani ni kupagawa ni pamoja na saikosisi, nurosisi, hysteria (umanyeto), skizofrenia, “multi personality”, mania (wazimu) na phobia (hofu).

Narudia. Kesi za kupagawa hasa LAZIMA ziwe chache duniani kwa sababu ya ushindi wa Kristo. Tena anayekutwa na mkasa huo wa kupagawa na Shetani LAZIMA AWE MDHAMBI kwa sababu kama mtu ni safi rohoni, ANA YESU, na kama mtu ana Yesu ndani yake, Shetani hawezi kuja na kufanya makazi katika mtu huyo huyo. Haiwezekani Yesu na Shetani wakae katika mtu mmoja. Haiwezekani kabisa! Haiwezekani mtu mmoja yule yule awe “MKRISTO” na “MSHETANI”.

Tena tukikumbuka kwamba Wakristo ni viungo katika Mwili wa Fumbo wa Yesu Kristo (1Kor 12), yaani wewe labda ni mguu, mimi ni mkono na mwengine ni pua au macho, Shetani anawezaje kuja na kukaa katika kiungo cha Kristo? Shetani ana ubavu gani kuja kukaa kwenye mguu, mkono, pua au macho ya Kristo? Thubutu yake hawezi! Hawezi labda kiungo hicho kiwe kimejiondoa chenyewe kutoka Mwili wa Kristo kwa dhambi ya mauti asiyotaka kuiungama.

Tuwasaidieje Akinamama?
Sasa kama tunataka kuwasaidia akinamama waliopagawa, kazi ya awali kabisa ni kubaini kesi zipi ni za Shetani (mapepo) kweli. Ili kuzibaini kesi zipi ni za mapepo na zipi sizo kunahitajika ujuzi wa kuzipambua kesi kama Yesu Kristo alivyokuwa akizipambua.

Hakuna haraka katika kuwatibu. Kunahitajika kuzunguzumza na mgonjwa na kuchunguza vizuri katika ushauri (counseling) historia na mazingira ya ugonjwa na kisha kupeleka kesi zinazoonesha kupagawa kwa kweli kwa mwinga pepo padre au Askofu aliyeruhusiwa rasmi (Sheria ya Kanisa namba 1172 paragrafu 1 na 2).

Sheria inasema anayeweza kuruhusiwa na kufanya kazi ya kuwinga pepo kihalali ni padre au Askofu na si kila mtu kujifanyia kazi hiyo atakavyo. Hivi wanavyofanya Karismatiki ni uvunjaji sheria wa wazi na wanaowaunga mkono ni watu wanaolipuuza Kanisa pasipo simile.

Padre au Askofu huruhusiwa kuwinga pepo akikidhi masharti manne: uchaji, busara, ujuzi na uadilifu, la sivyo, anaweza kufedheheshwa na Shetani kama walivyofedheheshwa watoto wa Skewa (soma mwenyewe Mdo 19:11-19).

Kuwatibu akinadada na akinamama waliopagawa kweli, kwa vyovyote wachache tu, si suala la kuwamwagia au kuwaogesha maji ya baraka, wala kuwachapa kwa rozari, wala kuwadanganya kwa kuwatia matumaini feki, wala kuwaamuru waruke au walambe chumvi ya kiganga, wala kuwapaka mafuta sehemu zao za siri, sembuse kuwafanyia tendo la ndoa.

Ni kutulia nao kwanza na halafu kuchunguza kinachowasababishia shida. Wagonjwa wa kweli waombewe kwa sala zilizoidhinishwa na Kanisa na katika upweke wa kuwastahi. Sikiliza, uwingaji pepo hadharani unaweza kuvunja heshima mbele ya watu.

Haiwezekani kuwa M-KRISTO na M-SHETANI Wakati Mmoja
Nisikilize vyema. Mtu hawezi kuwa MKRISTO na MSHETANI wakati mmoja. Wimbi la umeme haliwezi kuwa chanya na hasi wakati ule ule. Namba haIwezi kuwa shufwa na ninii sijui wakati ule ule. Mkristo madhubuti hawezi kukaliwa na Shetani.

Kwa nini? Ni kwa kutokana na mambo sita au niseme saba yafuatayo, mosi, kutokana na Yesu kumshinda shetani (Mt 12:29); pili, kila mwanadamu kuwa na malaika mlinzi mmoja (Kut 23:20-23); tatu, watu kubatizwa na kupakwa mafuta ya kumkinga na pepo; nne, watu kuwa na vinywani mwao majina wanayoogopa mashetani yaani Yesu na Maria (Mdo 19:11-19); tano, watu kupata ulinzi wa pekee kutoka kwa Yesu (Yn 10:27-30); sita, watu kumvalia shetani silaha za kumpinga (Efe 6:13-17) na saba watu kutumia akili na utashi wao kumpinga shetani na kumkaribia Mungu (Yak 4:7-8).

Kutokana na haya, kesi za watu kupagawa na shetani LAZIMA ziwe chache kabisa. La sivyo, Yesu hakushinda au mtu binafsi ametia dosari katika mambo yote saba niliyotaja. Narudia, haiwezekani mfuasi kamili wa Yesu kukaliwa na Shetani maana alipo Yesu Shetani hakai na anapokaa Shetani Yesu amewekwa kando. Yesu anakaaje zizi moja na adui wake wa jadi?

Kwa kisa hiki, ninakiri kesi za akina mama zinaongezeka lakini nakataa haiwezekani kesi zote hizi zikawa za mapepo au mashetani. Ndipo ukitazama jinsi akinadada na akinamama wetu weusi wanavyohangaika makanisani wakianguka, kulialia na kugaagaa, wengi wao, kama si kwa kuombwa na wachungaji wafanye hivyo kwa usanii, wana matatizo ya kijamii, kiuchumi, kisaikolojia au ya kiakili.

Hata ukienda Amerika ya Kusini, nchi za Karibiki na Marekani utakaowaona wakianguka anguka na kuweweseka wengi ni akinadada na akinamama wenye ngozi nyeusi au machotara. Ni hivi, ni nadra kuwakuta akinadada na akinamama Wazungu na Wahindi wenye nafasi zao wakiweweseka, kugaagaa, kulialia na kuangukaanguka hadharani. Ukifanya utafiti kwa haraka haraka utakuta wahanga ni akinadada au akinamama waliotemwa na wachumba wao, wasiooleka, walioachika au wenye hali ngumu kiuchumi.

Kwa upande wa wasichana utawaona wengi wanaoshambuliwa ni hasa mabinti wenye umri kati ya miaka 12 na 18, ambao kwa kweli huwa katika wakati wao wa wanasumbuliwa na nurosisi na hysteria kutokana na mabadiliko ya mwili pamoja na kufadhaishwa na kuingizwa kwao kwenye mambo ya wakubwa, nadhani mnanielewa. Akinadada, hasa wale wenye umri wa kuoleka, walio vyuoni au makazini, huanza matatizo hayo, pale zinapoanza kesi za kutelekezwa na wapenzi wao au kufadhaishwa na utoaji mimba.

Mambo haya yote ndiyo yanayoniambia mimi kwamba kesi za siku hizi nyingi zinahusika na matatizo nje ya kupagawa na shetani wa kweli. Ni kesi za saikosisi, nurosisi, skizofrenia, “multipersonality” na kadhalika, magonjwa tunayoyakosea tukidhani ni mapepo wakati ni zaidi magonjwa ya kisaikolojia na kiakili. Hapo tupambanue mambo kwa akili yetu pia.

Kwa kuhitimisha hivi, Waafrika na wote wenye ngozi nyeusi, tunajiabisha na akinadada na akinamama kataeni kufedheheshwa. Na chonde chonde msikubali kutumika na wachungaji katika “uwingaji pepo wa kisanii”. Mnacholipwa ni takataka mkilinganisha na ufalme wa mbinguni mtakaoukosa. Jiondoeni katika “kutumika”.

Kumbe kwa hali hii ya mambo, akinadada na akinamama wetu, mimi nawasihi mara kuwasihi, kataeni kabisa. Kwangu mimi kukataa huku kungekuwa sehemu ya uhuru wenu. Msigombee uhuru kisiasa na kiuchumi tu, kuna uhuru kiroho na kifikra vile vile.

Maswali machache tu yangewatosha kuwaambieni kwamba mnatumika na mnakubalishwa aibu. Hebu jiulizeni, tangu lini Shetani akawa “womanizer” tena akawa anawapenda akinamama wetu weusi zaidi? Iweje Shetani awapende ZAIDI akina mama weusi tena fukara?

Shetani gani huyo mbaguzi? Uende Jimbo lolote, hata padre wetu wa mwisho kabisa kwa tabia mbaya, yaani hata mlevi wetu wa mwisho anayelewa na kurudishwa Parokiani na waamini kwenye toroli, hana mapepo. Kinyume chake, akinadada na akinamama wazuri na wenye kuheshimika sana, utasikia wana eti mapepo, wanalialia na kuangukaanguka!

Mnadhani jambo hili maana yake nini? Hakika jambo hili linasema kwamba kesi za mapepo kati ya akinamama wetu nyingi si halisi. Kinyume chake zinaambatana na dhiki binafsi pamoja na “hali ngumu ya maisha”. Nahoji tena. Kama ni Shetani mbona anatuogopa akinababa hata tulio waovu kabisa?

Tuyaelewe Magonjwa ya Saikosisi, Nurosisi na Hysteria
Kwa kesi za mashuleni, ukiona wasichana, hasa wa kati ya miaka 12- 18 wanaweweseka na kuanguka anguka ujue ni nurosisi ambayo kuenea kwake hufanyika kwa hysteria.

Lakini dawa yake si kuwaita Karismatiki, wachungaji au waganga wa kienyeji isipokuwa kutafuta chanzo cha mkasa huo kwa kuwahoji vizuri, kuwaimarisha kwa kuwaelimisha na kuwashauri pamoja na kuwashirikisha wazazi washiriki kuwaimarisha binti zao wanaopitia mabadiliko makubwa ya kimwili, kijinsia na kijamii. Kwa akinadada na akinamama, tusiyapuuze matatizo ya saikosisi na nurosisi.

Kwa Nini Akinamama Ni Wahanga Wakubwa?
Kuna sababu tatu kwa nini akinadada na akinamama huzuka kirahisi wahanga wa magonjwa ya ajabu. Mosi, malepe mawili ya ubongo wa akinadada na akinamama yanafanya kazi karibu sawasawa. Kwa namna hiyo, wana namna ya mlango wa sita wa ufahamu.

Kwa mlango huu wanaona vinaganaga vingi vya mambo, baadhi ya vinaganaga hivyo vikiwatisha wenyewe. Kinyume chao, ubongo wa akinakaka na akinababa hufanya kazi vizuri upande moja, wa kushoto au wa kulia, na hivi si rahisi kwao kuvibaini na kutishika na vinaganaga vya mambo. Pili, akinadada na akinamama wana mfumo wa hisia tofauti na akinakaka na akinababa.

Kifupi, kuna mifumo miwili ya hisia MNS na TPS. MNS – Mirror Neuro System (kuonja tatizo) na TPS – Temporal Parietal System (kufahamu tatizo). Akina dada na akinamama mfumo wao hasa ni MNS, mfumo unaowafanya waonje ugonjwa na kuathirika nao wenyewe.

Akinakaka na akinababa mfumo wao ni huo wa pili. Sababu ya tatu ni kwamba huwachukua muda mwingi akinadada na akinamama kutuliza mawimbi ya ubongo (alpha, beta, gamma, delta na theta) yakitiswa na matatizo au adha za dunia. Wanabeba matatizo, wanaume hawabebi. Wanaume ni mabingwa wa kuupuza na kudharau mambo. Kwa wanaume mambo hupita kirahisi. Wanawake sivyo.

Dawa ya Ajabu
Ni ajabu, lakini ni kweli kwamba wakati mwingine na katika kesi zingine, vitisho ni dawa ya kufaa sana. Yaani, katika kushughulikia kesi za saikosisi, nurosisi na hysteria, mara nyingine kuwatisha wahanga kwamba watakong’otwa au labda watafukuzwa shule ni bora zaidi kuliko kulidekeza na kuliogopa tatizo.

Hatima
Namalizia kwa kukuwekeeni mbele yenu, hasa ninyi mabinti , dada na mama zangu, tabia kumi za kuacha kusudi kukwepa au kujiponya na matatizo yanayowasonga. Ni hivi:

i. ACHA kusimulia hadithi za kutisha, utajitisha mwenyewe.

ii. ACHA kusikiliza hadithi za kutisha, utatishwa nazo.

iii. ACHA kuziamini hadithi za kutisha, utabeba hofu ya kudumu.

iv. ACHA kuhudhuria mikutano ya uponyaji na utoaji mapepo, utaanguka kwa hysteria.

v. ACHA kwenda kuomba ushauri kwa wachungaji, utashauriwa vibaya ili uwe muumini wao wapate kukuvuna kila siku, kila juma, kila mwezi na kila mwaka.

vi. ACHA kuwaruhusu watu wanaowatisha wengine kuwafundisha hasa mabinti shuleni. Kwa kufanya hivyo utawazalisha “vilaza” na waoga wasioweza kuthubutu chochote. Mabinti wa aina hiyo wameingia hasarani, hawatajiamini tena na wala hawataoleka. Kwa nini? Kwa sababu wanaume hawawaoi wanawake wagonjwa ikiwa wanajua. Kumbuka, wao hutafuta “wasaidizi wa kufaa” siyo wagonjwa wa kuwavumilia (Mwa 2:18).

vii. ACHA kulialia kwenye mikutano. Ukizoea utakuwa nani? Hutaoleka na ukiolewa hutakawia kuachwa. Wanaume hawapendi kuoa akinadada au akinamama wanaowajua tangu mwanzo kwamba ni wagonjwa wa kuweweseka, kulialia au kuangukaanguka.

viii. ACHA kunung’unika kwenye mazungumzo na jirani, utazoa kunung’unika na kuhuzunika na hivyo kuharibu kujiamini kwako kwa kujizusha mwenyewe kiumbe kilichojazwa uchungu na huzuni na huzuni inaangamiza.

ix. ACHA kukosa maelewano na ndugu wa familia, jambo litakalokunyima maisha ya furaha, wakati furaha ni dawa ya maisha marefu.

Tutafakari sote! Ni mzee wenu Pd. Titus Amigu
 
NENO KUHUSU MAGONJWA YA AKINADADA NA AKINAMAMA
- MAGONJWA YA AKINAMAMA YAMEUCHACHAFYA ULIMWENGU TANGU ZAMANI SANA

Nadhani tumejipatia muda mrefuna wa kutosha kujadili mada iliyopita. Leo nawaleteeni nyingine kwamba kesi za magonjwa yanayowahangaisha zaidi akina dada na akinamama ni KESI ZA ZAMANI SANA, TENA ZAMANI MNO kuliko tunavyodhani wengi wetu. Namaanisha hasa kesi za kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo. Yaani kitaalamu namaanisha nurosisi na hysteria. Ilitosha akinadada na akinamama kulielewa vyema jambo hili na wao kukataa kutumiwa na wengine, hususan, akina baba “wenye hila” kama shamba la kuchumia matumbo yao. Unajua akinababa chungu nzima hujipatia kipato na riziki kwa kujitangaza na kuojinasibu kuweza kuwasaidia akinadada na akinamama katika matatizo yao ya afya.

Acha leo nikupitisheni katika historia upate kujua kwamba watu hawajaanza jana kuyashughulikia magonjwa hayo isipokuwa zamani sana. Nafanya hivi kwa sababu historia ni mwalimu. Historia huwaonesha watu walikotoka, walipo na wanakoweza kwenda. Basi, historia fupi ya magonjwa ya akinadada na akinamama ni hii ifuatavyo:

Enzi za Hippocrates
Ndugu zanguni, kesi za akinamama, si kwamba zimeanza katika karne yetu hii. Nimeshasema kwamba zina historia ya miaka mingi sana. Kumbe, tuwe macho tusisahaulishwe usomi wetu hasa wa ushauri kwa kadiri ya mwendo wa historia ulivyokwenda. Ni hivi, kesi za akina mama zilijulikana na kuwatinga watu tangu enzi za akina Hippocrates, yaani hata kabla Yesu hajazaliwa. Hiyo ni katika Ugiriki au Uyunani. Wanaume yaliwatinga magonjwa ya akinamama ya kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo. Kwa kitendawili hicho, Hippocrates alikuja na jawabu la aina yake. Yeye alidai akina mama wanaonesha magonjwa ambayo wanaume hawaoneshi kwa sababu walikuwa wanasumbuliwa na tumbo la uzazi (hystera) linalorandaranda miili mwao. Alisema walikuwa wanachanganyikiwa zaidi tumbo la uzazi linapofika kooni katika safari zake za kuhamahama mwilini mwa mwanamke. Hapo ndipo ulipozaliwa msamiati wa “hysteria”, kwa Kiswahili, umanyeto).

Kama unataka kuniuliza dalili za hysteria, naomba usijisumbue maana nakuletea sasa hivi. Dalili zake ni hizi: kuzimiazima, kukosa usingizi, kuchachatika mwili, kutokutulia , wasiwasi na msukumo au hamu ya kitendo cha ngono.

Hadi hapa nakupa muhtasari. Hippocrates ndiye aliyetoa jina “hystera” au “uterus”, yaani “tumbo la uzazi”. Neno “hytera” ndiyo iliyozaa jina “hysteria”. Alidai kwa kuwa linatembeatembea mwilini mwao na linapofika shingoni, wanawake huugua magonjwa ya ajabu kabisa, magonjwa ambayo wanaume hawaugui kwa vile hawana tumbo la uzazi. Ndipo bwana huyu alisema hysteria ni ugonjwa wa akinamama kwani ndio wenye tumbo la uzazi lenye kuwarabu.

Enzi za Aretaeus
Pite pite akaja Bw. Aretaeus. Kati yote aliyosema, kubwa ni kauli yake kwamba hysteria ni “mnyama ndani ya mnyama” yaani mwanamke. Kwa mtazamo wake alipendekeza kuwasaidia akinamama kwa dawa ya manukato mawili, ya kunukia vizuri kuwekwa chini ya sehemu za siri na ya kunuka au kuchoma kumnusisha mwanamke puani kusudi mwanamke anayetibiwa akipiga chafya tumbo la uzazi literemke na kurudi mahali pake. Basi, ndivyo walivyokuwa wanatibiwa wanawake waliokuwa wanaweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo.

Enzi za Galen na Wenzake
Katika karne ya pili, Baada ya Kristo, wakaja watu kama akina Galen walioendeleleza matibabu ya kuwawekea akinamama wagonjwa manukato mawili, yale ya chini ya via vya uzazi na ya kunuka puani ili wakipiga chafya tumbo la uzazi literemke na kurudi sehemu yake. Pamoja na dawa hiyo Bw. Galen akaongeza upakaji mafuta juu ya sehemu za siri pamoja na “kulala nao” kwa vile aliamini walikuwa wahangaishwa na kukosa msisimko wa tendo la ndoa, hususan, wagonjwa waliokuwa wajane na wale wasioolewa pamoja na wanawake tasa. Lakini sikiliza vyema, huko “kulala nao” alikuwa anawaagiza wasaidizi wake wafanye. Kimuhtasari, katika karne ya pili, B.K., Bw. Galen alisema hysteria inawasumbua wanawake wasioolewa, wasioozaa pamoja na wajane ambao walizoea tendo la ndoa lakini kwa wakati huo walikuwa wanalikosa (“wanalimiss”) na wao kusumbuliwa na hamu kubwa. Bw. Galen alipendekeza dawa ya aina yake ndiyo kuwapaka akinamama wagonjwa mafuta sehemu za siri, na kwa kupitia wasaidizi wake kuwafanyia tendo la ndoa.

Enzi za Karne za Kati
Katika enzi za kati, yaani karne 5-15 B.K., ikaongezwa sababu nyingine moja, ndiyo “kupagawa na mapepo”. Kufuatia sababu hii, shughuli za uwingaji pepo zikapamba moto sana. Kifupi, katika karne za kati (karne 5-15 B.K.) iliongezwa sababu moja kupagawa na mapepo. Ndipo dawa ikaongezwa pia yaani kuwinga pepo (exorcism).

Enzi ya Karne 16-17
Katika karne ya 16-17, ziliongezwa sababu mbili mpya, mosi, kuwako kwa majimaji kwenye tumbo la uzazi na pili, kukosa tendo la ndoa. Kwa kufuatia sababu hizo ile dawa ya “kulala nao” wagonjwa ili kuwapa raha ilishika chati ya aina yake.

Enzi za Sigmund Freud
Katika karne ya 19, alikuja daktari wa madawa, Bw. Sigmund Freud (1856-1939). Mtu huyu wa pekee alikuja na nadharia ya “tatizo la Oedipus” na “libido”. Kwa tatizo la Oedipus alisema watoto huwaelekea wazazi wa jinsia tofauti, binti humwelekea baba, na mtoto wa kiume humwelekea mama. Kwa dhana ya “libido” akidai wanadamu, yaani pamoja na akinamama, walikuwa wanahangaishwa na kukosewa kwa nguvu za uzazi katika utoto wao. Kwa maoni hayo akapendekeza kuwasaidia akinamama kwa kuzungumza nao kusudi kujua lini mambo yalipowaendea mrama. Mwenyewe alikuwa akikaa na wagonjwa wachache kwa kusudi la kuwasaidia na wakati huo huo kuwafanyia utafiti.

Kwa yale aliyokuwa akiyagundua akatoa hotuba tano ambazo zilihudhuriwa na watu wachache sana kwani alikuwa akipuuzwa. Kwa kweli, watu wengi walimpinga na kumpuuza lakini watu wachache kama akina Carl Jung walimuunga mkono. Kwa vyovyote ilivyokuwa, Sigmund Freud ndiye baba wa elimu ya kutibu magonjwa kwa mpambanuo wa kisaikolojia (psychoanalysis). Huu ndio msingi wa namna nyingi za kisasa za kuwasaidia akinamama wanaoweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu yao.

Kimuhtasari, katika karne ya 19 alitokea Daktari Sigmund Freud akatoa sababu ya “Oedipus complex” na “libido” na akaanzisha pia utafiti wa nafsi (psychoanalysis).

Enzi za Leo
Hapa Afrika, tumeingia sisi. Namaanisha sisi zamu yetu ndiyo siku hizi. Kwa kweli sisi hatuna jibu lenye mashiko kwa tatizo la akinamama kuweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo. Hata hivyo, kitu cha kushangaza ni kwamba wengi wetu tumejichimbia kwenye sababu ya mapepo na kupagawa tu huku tukisahau kabisa nyenzo za kiushauri na mipambanuo ya kisaikolojia (psychoanalysis). Mimi nawasihini kwa heshima na taadhima, tutaalamike japo kidogo. Haiwezekani kesi za binti zetu, dada zetu na mama zetu, kwa wingi wake wote huo kuwa ni kupagawa na mapepo. Haiwezekani, nakataa.

Wewe jiulize tu, kwa nini Shetani awarabu wao zaidi? Tuseme Shetani anawaogopa wanaume? Zaidi ya hayo, “wanawake wanaosemekana kupagawa” wengi wao ni wenye rangi nyeusi. Sasa mambo yanapokuwa hivyo tangu lini Shetani akawa moto wa kuotea mbali kwa akinamama yaani kwa Kiingereza “womanizer?” Kumbe, nawasihini, ndugu zangu tusiwe watu wa nyuma hivi. Tufunguke macho lau kidogo! Ni karne ya ishirini na moja hii. Ebu tutilie pia maanani utaalamu maana maarifa na elimu ya kisasa ni pia karama zitokazo kwa Roho Mtakatifu. Tusidharau utaalamu na weledi, kwa kufanya hivyo tunamkufuru Roho Mtakatifu aliye nyuma ya pazia.

Hitaji la Elimu ya Saikolojia na Ushauri
Elimu ya Saikolojia inahitajika sana siku hizi. Kwa hili, mimi nawaaseni nyote. Si vizuri ulimwengu uende mbele katika elimu na sisi hapa barani Afrika tuishi kwa elimu kama ya waganga wa kienyeji. Wakati umebadilika na sisi tubadilike. Hii ni karne ya sayansi na teknolojia.

Nazisihi seminari zetu ziongeze nguvu katika masomo ya Saikolojia na Ushauri Nasaha. Kishapo, majimbo yetu yafikirie kuwa na mapadre mabingwa wa Saikolojia na Ushauri Nasaha kusudi kesi zingine zinazosemekana kuwa za kupagawa ziangaliwe vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo nyingi zinatiwa katika kapu la kazi ya Shetani pasipo hata tafakari na utafiti. Wengi wanaojitosa katika kuwasaidia akinamama wanaoweweseka weweseka, kulialia, kuanguka anguka, kufadhaika na kuzimia na kishapo mwingine au wengine kudakia masaibu hayo hayo, wanakimbilia kusema ni kupagawa na mapepo au pengine “majini” kwa fikra za Kiislamu na hivyo kuwa na dawa mbili: kuwamwagia wagonjwa maji ya baraka na kukemea.

Hapo hapo wapo wengine wanathubutu kuwapaka akinamama mafuta kwenye sehemu za siri kama walivyokuwa wanafanya akina Galen. Lakini, kwa jinsi hali ya hewa inavyokwenda, nadhani bado kama inchi moja hivi wengine waende kwenye suluhisho la “kulala na wagonjwa” kama zama za kale. Ole wetu tufikie hapo tena!

Lakini Kesi Nyingi si Mapepo
Nina hoja nzito. Kesi za watu kupagawa, hususan, kati ya Wakristo LAZIMA ziwe chache sana kwa sababu Kristo amemshinda Shetani kwa niaba yetu. Mmoja (Shetani) aliyeshindwa hawezi kuwa na nguvu au kutamba kama kwanza. Jambazi aliyevunjwa kiuno hawezi kuwa jeuri kama kabla hajavunjwa kiuno. Kumbe, siku hizi, ndiyo enzi za Agano Jipya, tukidai kwamba Shetani ana nguvu sana, labda eti “amejiinua” tunaikufuru kazi ya Kristo kwa sababu tutakuwa tunamaanisha kazi yake haikuwa na mapato yoyote ya maana, jambo ambalo si kweli. Hivi kesi nyingi ni za kisaikolojia au tuseme ni magonjwa tunayoyakosea kwa kudhani ni mapepo. Magonjwa tunayoyakosea na kudhani ni kupagawa ni pamoja na saikosisi, nurosisi, hysteria (umanyeto), skizofrenia, “multi personality”, mania (wazimu) na phobia (hofu).

Narudia. Kesi za kupagawa hasa LAZIMA ziwe chache duniani kwa sababu ya ushindi wa Kristo. Tena anayekutwa na mkasa huo wa kupagawa na Shetani LAZIMA AWE MDHAMBI kwa sababu kama mtu ni safi rohoni, ANA YESU, na kama mtu ana Yesu ndani yake, Shetani hawezi kuja na kufanya makazi katika mtu huyo huyo. Haiwezekani Yesu na Shetani wakae katika mtu mmoja. Haiwezekani kabisa! Haiwezekani mtu mmoja yule yule awe “MKRISTO” na “MSHETANI”.

Tena tukikumbuka kwamba Wakristo ni viungo katika Mwili wa Fumbo wa Yesu Kristo (1Kor 12), yaani wewe labda ni mguu, mimi ni mkono na mwengine ni pua au macho, Shetani anawezaje kuja na kukaa katika kiungo cha Kristo? Shetani ana ubavu gani kuja kukaa kwenye mguu, mkono, pua au macho ya Kristo? Thubutu yake hawezi! Hawezi labda kiungo hicho kiwe kimejiondoa chenyewe kutoka Mwili wa Kristo kwa dhambi ya mauti asiyotaka kuiungama.

Tuwasaidieje Akinamama?
Sasa kama tunataka kuwasaidia akinamama waliopagawa, kazi ya awali kabisa ni kubaini kesi zipi ni za Shetani (mapepo) kweli. Ili kuzibaini kesi zipi ni za mapepo na zipi sizo kunahitajika ujuzi wa kuzipambua kesi kama Yesu Kristo alivyokuwa akizipambua. Hakuna haraka katika kuwatibu. Kunahitajika kuzunguzumza na mgonjwa na kuchunguza vizuri katika ushauri (counseling) historia na mazingira ya ugonjwa na kisha kupeleka kesi zinazoonesha kupagawa kwa kweli kwa mwinga pepo padre au Askofu aliyeruhusiwa rasmi (Sheria ya Kanisa namba 1172 paragrafu 1 na 2). Sheria inasema anayeweza kuruhusiwa na kufanya kazi ya kuwinga pepo kihalali ni padre au Askofu na si kila mtu kujifanyia kazi hiyo atakavyo. Hivi wanavyofanya Karismatiki ni uvunjaji sheria wa wazi na wanaowaunga mkono ni watu wanaolipuuza Kanisa pasipo simile. Padre au Askofu huruhusiwa kuwinga pepo akikidhi masharti manne: uchaji, busara, ujuzi na uadilifu, la sivyo, anaweza kufedheheshwa na Shetani kama walivyofedheheshwa watoto wa Skewa (soma mwenyewe Mdo 19:11-19).
Kuwatibu akinadada na akinamama waliopagawa kweli, kwa vyovyote wachache tu, si suala la kuwamwagia au kuwaogesha maji ya baraka, wala kuwachapa kwa rozari, wala kuwadanganya kwa kuwatia matumaini feki, wala kuwaamuru waruke au walambe chumvi ya kiganga, wala kuwapaka mafuta sehemu zao za siri, sembuse kuwafanyia tendo la ndoa. Ni kutulia nao kwanza na halafu kuchunguza kinachowasababishia shida. Wagonjwa wa kweli waombewe kwa sala zilizoidhinishwa na Kanisa na katika upweke wa kuwastahi. Sikiliza, uwingaji pepo hadharani unaweza kuvunja heshima mbele ya watu.

Haiwezekani kuwa M-KRISTO na M-SHETANI Wakati Mmoja
Nisikilize vyema. Mtu hawezi kuwa MKRISTO na MSHETANI wakati mmoja. Wimbi la umeme haliwezi kuwa chanya na hasi wakati ule ule. Namba haIwezi kuwa shufwa na ninii sijui wakati ule ule. Mkristo madhubuti hawezi kukaliwa na Shetani. Kwa nini? Ni kwa kutokana na mambo sita au niseme saba yafuatayo, mosi, kutokana na Yesu kumshinda shetani (Mt 12:29); pili, kila mwanadamu kuwa na malaika mlinzi mmoja (Kut 23:20-23); tatu, watu kubatizwa na kupakwa mafuta ya kumkinga na pepo; nne, watu kuwa na vinywani mwao majina wanayoogopa mashetani yaani Yesu na Maria (Mdo 19:11-19); tano, watu kupata ulinzi wa pekee kutoka kwa Yesu (Yn 10:27-30); sita, watu kumvalia shetani silaha za kumpinga (Efe 6:13-17) na saba watu kutumia akili na utashi wao kumpinga shetani na kumkaribia Mungu (Yak 4:7-8).

Kutokana na haya, kesi za watu kupagawa na shetani LAZIMA ziwe chache kabisa. La sivyo, Yesu hakushinda au mtu binafsi ametia dosari katika mambo yote saba niliyotaja. Narudia, haiwezekani mfuasi kamili wa Yesu kukaliwa na Shetani maana alipo Yesu Shetani hakai na anapokaa Shetani Yesu amewekwa kando. Yesu anakaaje zizi moja na adui wake wa jadi?

Kwa kisa hiki, ninakiri kesi za akina mama zinaongezeka lakini nakataa haiwezekani kesi zote hizi zikawa za mapepo au mashetani. Ndipo ukitazama jinsi akinadada na akinamama wetu weusi wanavyohangaika makanisani wakianguka, kulialia na kugaagaa, wengi wao, kama si kwa kuombwa na wachungaji wafanye hivyo kwa usanii, wana matatizo ya kijamii, kiuchumi, kisaikolojia au ya kiakili.

Hata ukienda Amerika ya Kusini, nchi za Karibiki na Marekani utakaowaona wakianguka anguka na kuweweseka wengi ni akinadada na akinamama wenye ngozi nyeusi au machotara. Ni hivi, ni nadra kuwakuta akinadada na akinamama Wazungu na Wahindi wenye nafasi zao wakiweweseka, kugaagaa, kulialia na kuangukaanguka hadharani. Ukifanya utafiti kwa haraka haraka utakuta wahanga ni akinadada au akinamama waliotemwa na wachumba wao, wasiooleka, walioachika au wenye hali ngumu kiuchumi.

Kwa upande wa wasichana utawaona wengi wanaoshambuliwa ni hasa mabinti wenye umri kati ya miaka 12 na 18, ambao kwa kweli huwa katika wakati wao wa wanasumbuliwa na nurosisi na hysteria kutokana na mabadiliko ya mwili pamoja na kufadhaishwa na kuingizwa kwao kwenye mambo ya wakubwa, nadhani mnanielewa. Akinadada, hasa wale wenye umri wa kuoleka, walio vyuoni au makazini, huanza matatizo hayo, pale zinapoanza kesi za kutelekezwa na wapenzi wao au kufadhaishwa na utoaji mimba.

Mambo haya yote ndiyo yanayoniambia mimi kwamba kesi za siku hizi nyingi zinahusika na matatizo nje ya kupagawa na shetani wa kweli. Ni kesi za saikosisi, nurosisi, skizofrenia, “multipersonality” na kadhalika, magonjwa tunayoyakosea tukidhani ni mapepo wakati ni zaidi magonjwa ya kisaikolojia na kiakili. Hapo tupambanue mambo kwa akili yetu pia.

Kwa kuhitimisha hivi, Waafrika na wote wenye ngozi nyeusi, tunajiabisha na akinadada na akinamama kataeni kufedheheshwa. Na chonde chonde msikubali kutumika na wachungaji katika “uwingaji pepo wa kisanii”. Mnacholipwa ni takataka mkilinganisha na ufalme wa mbinguni mtakaoukosa. Jiondoeni katika “kutumika”.
Kumbe kwa hali hii ya mambo, akinadada na akinamama wetu, mimi nawasihi mara kuwasihi, kataeni kabisa. Kwangu mimi kukataa huku kungekuwa sehemu ya uhuru wenu. Msigombee uhuru kisiasa na kiuchumi tu, kuna uhuru kiroho na kifikra vile vile.

Maswali machache tu yangewatosha kuwaambieni kwamba mnatumika na mnakubalishwa aibu. Hebu jiulizeni, tangu lini Shetani akawa “womanizer” tena akawa anawapenda akinamama wetu weusi zaidi?
Iweje Shetani awapende ZAIDI akina mama weusi tena fukara? Shetani gani huyo mbaguzi? Uende Jimbo lolote, hata padre wetu wa mwisho kabisa kwa tabia mbaya, yaani hata mlevi wetu wa mwisho anayelewa na kurudishwa Parokiani na waamini kwenye toroli, hana mapepo. Kinyume chake, akinadada na akinamama wazuri na wenye kuheshimika sana, utasikia wana eti mapepo, wanalialia na kuangukaanguka! Mnadhani jambo hili maana yake nini? Hakika jambo hili linasema kwamba kesi za mapepo kati ya akinamama wetu nyingi si halisi. Kinyume chake zinaambatana na dhiki binafsi pamoja na “hali ngumu ya maisha”. Nahoji tena. Kama ni Shetani mbona anatuogopa akinababa hata tulio waovu kabisa?

Tuyaelewe Magonjwa ya Saikosisi, Nurosisi na Hysteria
Kwa kesi za mashuleni, ukiona wasichana, hasa wa kati ya miaka 12- 18 wanaweweseka na kuanguka anguka ujue ni nurosisi ambayo kuenea kwake hufanyika kwa hysteria. Lakini dawa yake si kuwaita Karismatiki, wachungaji au waganga wa kienyeji isipokuwa kutafuta chanzo cha mkasa huo kwa kuwahoji vizuri, kuwaimarisha kwa kuwaelimisha na kuwashauri pamoja na kuwashirikisha wazazi washiriki kuwaimarisha binti zao wanaopitia mabadiliko makubwa ya kimwili, kijinsia na kijamii. Kwa akinadada na akinamama, tusiyapuuze matatizo ya saikosisi na nurosisi.

Kwa Nini Akinamama Ni Wahanga Wakubwa?
Kuna sababu tatu kwa nini akinadada na akinamama huzuka kirahisi wahanga wa magonjwa ya ajabu. Mosi, malepe mawili ya ubongo wa akinadada na akinamama yanafanya kazi karibu sawasawa. Kwa namna hiyo, wana namna ya mlango wa sita wa ufahamu. Kwa mlango huu wanaona vinaganaga vingi vya mambo, baadhi ya vinaganaga hivyo vikiwatisha wenyewe. Kinyume chao, ubongo wa akinakaka na akinababa hufanya kazi vizuri upande moja, wa kushoto au wa kulia, na hivi si rahisi kwao kuvibaini na kutishika na vinaganaga vya mambo. Pili, akinadada na akinamama wana mfumo wa hisia tofauti na akinakaka na akinababa.

Kifupi, kuna mifumo miwili ya hisia MNS na TPS. MNS – Mirror Neuro System (kuonja tatizo) na TPS – Temporal Parietal System (kufahamu tatizo). Akina dada na akinamama mfumo wao hasa ni MNS, mfumo unaowafanya waonje ugonjwa na kuathirika nao wenyewe. akinakaka na akinababa mfumo wao ni huo wa pili. Sababu ya tatu ni kwamba huwachukua muda mwingi akinadada na akinamama kutuliza mawimbi ya ubongo (alpha, beta, gamma, delta na theta) yakitiswa na matatizo au adha za dunia. Wanabeba matatizo, wanaume hawabebi. Wanaume ni mabingwa wa kuupuza na kudharau mambo. Kwa wanaume mambo hupita kirahisi. Wanawake sivyo.

Dawa ya Ajabu
Ni ajabu, lakini ni kweli kwamba wakati mwingine na katika kesi zingine, vitisho ni dawa ya kufaa sana. Yaani, katika kushughulikia kesi za saikosisi, nurosisi na hysteria, mara nyingine kuwatisha wahanga kwamba watakong’otwa au labda watafukuzwa shule ni bora zaidi kuliko kulidekeza na kuliogopa tatizo.

Hatima
Namalizia kwa kukuwekeeni mbele yenu, hasa ninyi mabinti , dada na mama zangu, tabia kumi za kuacha kusudi kukwepa au kujiponya na matatizo yanayowasonga: NI HIVI:
i. ACHA kusimulia hadithi za kutisha, utajitisha mwenyewe.
ii. ACHA kusikiliza hadithi za kutisha, utatishwa nazo.
iii. ACHA kuziamini hadithi za kutisha, utabeba hofu ya kudumu.
iv. ACHA kuhudhuria mikutano ya uponyaji na utoaji mapepo, utaanguka kwa hysteria.
v. ACHA kwenda kuomba ushauri kwa wachungaji, utashauriwa vibaya ili uwe muumini wao wapate kukuvuna kila siku, kila juma, kila mwezi na kila mwaka.
vi. ACHA kuwaruhusu watu wanaowatisha wengine kuwafundisha hasa mabinti shuleni. Kwa kufanya hivyo utawazalisha “vilaza” na waoga wasioweza kuthubutu chochote. Mabinti wa aina hiyo wameingia hasarani, hawatajiamini tena na wala hawataoleka. Kwa nini? Kwa sababu wanaume hawawaoi wanawake wagonjwa ikiwa wanajua. Kumbuka, wao hutafuta “wasaidizi wa kufaa” siyo wagonjwa wa kuwavumilia (Mwa 2:18).
vii. ACHA kulialia kwenye mikutano. Ukizoea utakuwa nani? Hutaoleka na ukiolewa hutakawia kuachwa. Wanaume hawapendi kuoa akinadada au akinamama wanaowajua tangu mwanzo kwamba ni wagonjwa wa kuweweseka, kulialia au kuangukaanguka.
viii. ACHA kunung’unika kwenye mazungumzo na jirani, utazoa kunung’unika na kuhuzunika na hivyo kuharibu kujiamini kwako kwa kujizusha mwenyewe kiumbe kilichojazwa uchungu na huzuni na huzuni inaangamiza.
ix. ACHA kukosa maelewano na ndugu wa familia, jambo litakalokunyima maisha ya furaha, wakati furaha ni dawa ya maisha marefu.

Tutafakari sote! Ni mzee wenu Pd. Titus Amigu
Yote uliyoyasema ni sahihi hasa historia ya ugonjwa huu! Kongole kwako! Kwasasa ugonjwa huu hauitwi tena HYSTERIA bali unaitwa Conversion Disorder.

Chanzo kikuu sio tena tumbo la uzazi bali ni MSONGO WA MAWAZO (Stress). Tatizo hili humkumba mtu ambaye hana mbinu sahihi/nzuri za kukabiliana ma msongo wa mawazo. Mungu katupatia mwili wa ajabu ambao unafanya kazi vema ila unahitaji usaidizi wetu. Hivyo basi, unapokosa mbinu za kukabiliana na msongo wa mawazo, mwili unachanganyikiwa unashindwa kujua ufanye nini! Hivyo, mwili unaamua kuzibadili stress hizo kwa namna mbili: 1. Zinakuwa maumivu (Somatoform Disorder). Utapata maumivu, maumivu ya kweli ambayo hayaelezeki kitabibu bali yanaelezeka kisaikolojia. Ndio maana utaenda hospitali zote utaambiwa hawaoni tatizo japo maumivu yapo. 2. Misuli ambayo una uwezo wa kui-control inaathirika (Conversion Disorder), unaweza onekana kama miguu/mikono imepooza, kupoteza uono, kushindwa kumeza, kuanguka/kuzimia, kupagwa......

Ni vema tujitahidi kutafuta mbinu sahihi za kukabiliana na changamoto tunazokabiliana nazo maishani vinginevyo ni bora ukaonana na wanasaikolojia kwa msaada zaidi.
 
Ukienda kwa nchi zilizoendela kidogo kuna hawa madaktari wa akili "Psychiatrist" na kuna sehemu ama majengo mengi ya watu wenye matatizo ya akili. Matatizo haya yanajitokea because of pressure, anxiety, depression, pain, trauma etc. Mie naamini yako kisayansi na yanatibika.

Kuna kipindi ubongo wangu ulikuwa unajenga fear wenyewe nikiwa ndotoni na hormones zinakuwa secreted mwilini za kutosha inanipelekea napata sana dizness usiku. Hali hii bado hunitokea ila nikiwa relaxed or sina stress huwa inapita mbali sana. .

Huo ugonjwa wa Hysteria nadhani ina male form sio kwa wanawake tu. Naamini ni magonjwa kama magonjwa mengine yanatibika unapopata tiba ya akili. Ila halisababishwi na TUMBO LA UZAZI si kweli hayo maoni nayakataa. Shida inapotokea kichwani ndani ya ubongo basi matatizo hayo uhutokea. Ingekuwa tumbo la uzazi linatembea basi kuna vifaa vingi kama ultrasound, x rays machine, MRI, scans tungeliona hii. . 🧐

Tumbo la uzazi linajumuisha na ****, sasa kama likiwa linatembea linaachaje K nyuma? Inafikirisha eti. .
 
Umeanza vizuri mada yak mpaka hapo ulipoanza kuingiza mambo ya "kristo " wengine tukaishia hapo kusoma, ttzo kama linawasbu kina mama basi lizungumze kwa jumuishi, usipendekeze solution ambayo itawagawa watu,kwa hio nkuulize, wakina mama wa kiislamu wao wafanye nini kupona?
 
Ukienda kwa nchi zilizoendela kidogo kuna hawa madaktari wa akili "Psychiatrist" na kuna sehemu ama majengo mengi ya watu wenye matatizo ya akili. Matatizo haya yanajitokea because of pressure, anxiety, depression, pain, trauma etc. Mie naamini yako kisayansi na yanatibika.

Kuna kipindi ubongo wangu ulikuwa unajenga fear wenyewe nikiwa ndotoni na hormones zinakuwa secreted mwilini za kutosha inanipelekea napata sana dizness usiku. Hali hii bado hunitokea ila nikiwa relaxed or sina stress huwa inapita mbali sana. .

Huo ugonjwa wa Hysteria nadhani ina male form sio kwa wanawake tu. Naamini ni magonjwa kama magonjwa mengine yanatibika unapopata tiba ya akili. Ila halisababishwi na TUMBO LA UZAZI si kweli hayo maoni nayakataa. Shida inapotokea kichwani ndani ya ubongo basi matatizo hayo uhutokea. Ingekuwa tumbo la uzazi linatembea basi kuna vifaa vingi kama ultrasound, x rays machine, MRI, scans tungeliona hii. . 🧐

Tumbo la uzazi linajumuisha na ****, sasa kama likiwa linatembea linaachaje K nyuma? Inafikirisha eti. .
Huu ugonjwa huwapata zaidi akina mama/wanawake kuliko wanaume zaidi. Hupatikana zaidi vijijini kuliko mijini. Japo kwasasa cases zipo nyingi za mijini pia.
 
Huu ugonjwa huwapata zaidi akina mama/wanawake kuliko wanaume zaidi. Hupatikana zaidi vijijini kuliko mijini. Japo kwasasa cases zipo nyingi za mijini pia.
Trust me I just read it online sometimes this disease its called PSTD for men. Kuna waliojitambua wana matatizo haya na kuna wale ambao wanashinda kwa waganga. As you most know some diseases are inherited and sometimes are popular with one race. .

Matatizo ya akili ni janga kitaifa, unaweza ongozwa na mtu mwenye matatizo ya akili bila yeye kujijua anaingiza nchi kwenye giza moja kubwa. Kuna haja ya kuwa na katiba imara na sio kuongozwa na viongozi wenye matatizo ya akili. .
 
Daa bora umeliangazia.
kuna maswali mengi yanabaki kichwani kwangu,
Je,hata biti mdogo 10,12yrs nao wanaweza kuwekwa ktk kundi hili la wanawake.
Kuna mabinti/wasichana wawili nipo karibu nao pia kwasasa wanasumbuliwa na tatizo kama hili.Zaidi wao wanakuwa na nguvu saa nyinge hukimbia ovyo ovyo,je,nao tuseme tatizo laweza kuwa hili.
Mbali na hao,mke wangu kipindi cha umri kama huo aliwahi ugua,baadae anasema maombi yalimponya!

Kwa kiasi kikubwa hili ni tatizo na limekuwa likiwagharimu pesa wazazi wa watoto hawa na wengine list nnayo ndefu.
Kama taifa na wizara yake lifanyike jambo.
Kuna shule flani mabinti walikuwa wakidondoka ovyo,afisa elimu alipochunguza akabaini shule hiyo haina miti ya vivuli,taarifa zinadai baada ya watoto kuanza kupumzishwa vivulini na kupunguziwa kazi hali ilitulia.
Kama ni hivyo basi wanawake/wasichana ni dhaifu kiakili kiasi hiki!
Inashangaza lakini inahitaji utafiti wa kutosha!
 
Miaka 12 tayari mtoto wa kike ameanza kuathiriwa na hormones na wengine huingia hata kuvunja ungo...njia sahihi ni hii ya kukutana na pyschologists
 
Trust me I just read it online sometimes this disease its called PSTD for men. Kuna waliojitambua wana matatizo haya na kuna wale ambao wanashinda kwa waganga. As you most know some diseases are inherited and sometimes are popular with one race. .

Matatizo ya akili ni janga kitaifa, unaweza ongozwa na mtu mwenye matatizo ya akili bila yeye kujijua anaingiza nchi kwenye giza moja kubwa. Kuna haja ya kuwa na katiba imara na sio kuongozwa na viongozi wenye matatizo ya akili. .
No, PTSD ni ugonjwa mwingine kabisa. PTSD chanzo chake chaweza kuwa vita, ajali, na matukio mengine mabaya.
 
Daa bora umeliangazia.
kuna maswali mengi yanabaki kichwani kwangu,
Je,hata biti mdogo 10,12yrs nao wanaweza kuwekwa ktk kundi hili la wanawake.
Kuna mabinti/wasichana wawili nipo karibu nao pia kwasasa wanasumbuliwa na tatizo kama hili.Zaidi wao wanakuwa na nguvu saa nyinge hukimbia ovyo ovyo,je,nao tuseme tatizo laweza kuwa hili.
Mbali na hao,mke wangu kipindi cha umri kama huo aliwahi ugua,baadae anasema maombi yalimponya!

Kwa kiasi kikubwa hili ni tatizo na limekuwa likiwagharimu pesa wazazi wa watoto hawa na wengine list nnayo ndefu.
Kama taifa na wizara yake lifanyike jambo.
Kuna shule flani mabinti walikuwa wakidondoka ovyo,afisa elimu alipochunguza akabaini shule hiyo haina miti ya vivuli,taarifa zinadai baada ya watoto kuanza kupumzishwa vivulini na kupunguziwa kazi hali ilitulia.
Kama ni hivyo basi wanawake/wasichana ni dhaifu kiakili kiasi hiki!
Inashangaza lakini inahitaji utafiti wa kutosha!
Ndio, tatizo hili laweza kuwapata watoto wadogo kama ulivyoainisha. Ni kweli kutokana na uelewa duni, wengi hukimbila kwa waganga wa kienyeji au kudhani ni mapepo!
 
Nasubir mwanamke aseme huwa anajiskiaje. Inaonekana kuna wakati sheria inakataana na nature.
Mf ni hili la kuzuia ngono kisheria lakin nature inadai ngono kwa umri chini ya sheria.
Kumbe mtume Mohammad alikuwa sahihi kuhusu kigezo cha kuolewa kuwa ni kuvunja ungo.
Bas wazaz wajiongeze kuwachanganya bint zao wasijepatwa disorder.
 
Dunia ina mambo
mengi sana,inaoyesha ngono ni tiba tena siyo kwa hili tu!
 
Nahoji tena. Kama ni Shetani mbona anatuogopa akinababa hata tulio waovu kabisa?
Kwa sababu wanaume mmeumbwa kwa mfano wa Mungu! hawezi thubutu hapo! na yeye shetani anajua vyema pa rahisi pa kuchezea!! kwa sababu kina Mama wakiombewa mapepo si yanatoka wanakuwa wazima!!

sasa shida iko wapi jameni???....au mleta mada unafurahi wanavo hangaika?? ni kweli hawaolewi sababu shetani limeshikilia maisha yake!! tangu zama za Yesu ke ndo wana shikiliwa na mapepo!

ke ndo destiny ya mwanadamu awaye yeyote! tumbo la ke ndo wanazaa manabii km Musa, ma-Rais, watu maarufu nk, kumbuka Bibi yake Yesu alikuwa kahaba wa jericho! shetani alimchelewesha maksudi!

na alijua kuna mtu mzito atazaliwa hapo!....Musa alipo karibiwa kuzaliwa zikapitishwa sheria za ajabu ajabu tu! ili wana wa israel wasifikie lengo! bila shaka weye umetumwa na shetani! ....tutakuombea usijali!

Kama ni hayo maradhi unayo yasema ni kweli mbona Hospitalini walishindwa mpaka leo??.......km huko kanisani wanapona hayo maradhi kwa kutumia saikolojia basi itakuwa ni nzuri pia waache!

hakuna ubaya wachungaji kutuombea acha wivu!! nyie mlikuwa wapi kutupatia dawa?? acheni tuombewe kwani inakunyima/kupunguzia usingizi?? tunachotaka akina Mama ni amani ya moyo na faraja ya mwili baaasi!

Psychology ya wachungaji pia ni dawa, km vile panadol, aspirin nk!....Yes! kuna Manabii wa uongo tunajua hilo!! na tutawajua kwa matendo yao! lkn hili halina maana kwamba hakuna Manabii wa ukweli!!

Na Mungu ametoa rhuksa tuwajaribuni hao! Manabii! na akasema tutawajua kwa matendo yao! km ni hivo ni lazima twende kwao/walipo ili kuwajaribu! tatizo liko wapi hapo??

Manabii wa uongo wapo kama weye unayetoa Unabii wa uongo hapa kwa kutumia vifungu vya Biblia ambavyo hata Shetani anayekutumia anavijua sana! alivitumia ivo ivo! kumjaribu Yesu palee calvary!!

Manabii wa uongo Mungu hajawateketeza ivo walikuwepo wapo watakuwepo! bila weye Mwanadamu kuwa na Roho Mtakatifu! utaingia chaka tu!...utapotea Mazimaaa!

Kusema Mapepo yanawaingia ke wachanga, wasioolewa, wajane nk! ni kweli kwa sababu hao hao! wa ivo ndo wana Potential kuuubwa sana ktk Ulimwengu wa Roho!

Nilikupa mfano Mariamu Magdalena alikuwa na Mapepo saba lkn huyo huyo baada ya kutolewa hayo Mapepo na kutembea na yesu ndo alikuwa wa kwanza kujua Yesu amafufuka lkn wliokuwa hawana mapepo hawkupata hiyo banati!

Kwa muktadha huo ukisema wanawake hawana Mapepo una dhihirisha kuwa Mungu ni muongo hakumtoa M/magdalena hayo mapepo saba, ni wazi kuwa wewe umetumwa na Shetani! kusamabaz ahuu uongo!

Mapepo/shetani ni live na pia Malaika na Mungu yupo!! shetani ana njia nyingi sana ya kurubuni wanadamu na weye umerubunika kwa siasa za shetani! ni sawa wala haitupi shida! kwakuwa tunajua kwa

Watu/mana bii wa uongo na watu km weye hamuna budi kuja ktk ulimwengu wa walio hai!.....cha Msingi kamwambie aliye kutuma wadada sisi hatutaacha kuombewa kamwe weye endelea na zako tu!

hao ke unao waona leo ni matajiri hwana mapepo. Maofisa wasio kuwa na mapepo! manake hao hawana potential ktk ulimwengu wa Roho ni Maskini wa kutupwa!...

Sasa wenye mapepo leo wale unaoona wakijigalagaza mavumbini ndo wazaa Manabii hatare! Wa kweli wamecheleweshwa tu na shetani tena maksudi! Kumbuka Mariam Magdalena aliombewa akapona!

Acha hizo Theorojia za kipepo bana tunajua sana! kuliko unavo dhania nenda kaseme Makristu yamestuka........wakupe nguvu uje kivingine!
 
Back
Top Bottom