Kwanini wanawake/wasichana wakishaolewa wanajisahau?

Kwanini wanawake/wasichana wakishaolewa wanajisahau?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
419
Jamani nina hoja fupi sana hapa, ni kwa nini wanawake/wasichana karibia wote wakishaolewa wanajisahau sana, yaani wanapunguza upendo na mumewe, wanaanza mambo ya kiburi,jeuri,dharau kibao, wanajibu hovyo hovyo.

Yaani kwa kifupi wana change na wanasahau kuwa walikua wanakesha wanasali na kwenda kwa waganga ili waolewe na wakiachwa sasa wataanza, oooh! nina mkosi, nimerogwa, kuna mkono wa mtu.

Binafsi nampongeza mke wangu kwani anajitambua sana.
 
Usifikir mkeo tu ndo anajitbua tupo tunaojua thamani ya mme anae fanya jeur kwenye ndoa huyo bado anataka kuuza vocha

Dah!ningekupata wewe wa nyumbani Ndali nahisi maisha yangu yangekuwa marefu zaidi!Unaonekana unajua thamani halisi ya mume!
 
jamani nina hoja fupi sana hapa, ni kwa nini wanawake/wasichana karibia wote wakishaolewa wanajisahau sana, yaani wanapunguza upendo na mumewe, wanaanza mambo ya kiburi,jeuri,dharau kibao, wanajibu hovyo hovyo, yaani kwa kifupi wana change na wanasahau kuwa walikua wanakesha wanasali na kwenda kwa waganga hili waolewe na wakiachwa sasa wataanza, oooh! nina mkosi, nimerogwa, kuna mkono wa mtu. binafsi nampongeza wife kwani anajitambua sana

Hasa wakishakuwa na kipato ndo shida zaidi!
 
Usitegemee kupendwa kama wewe umepunguza upendo na kuona kumuoa kwako ni kama umemsaidia maisha.
 
Hili ni kweli unaloongea ila labda huwa hatupati muda wa kuwafahamu vizuri hawa viumbe. Wengine huficha makucha yao na baadae kujidhihirisha wakati tayari wako kwenye ndoa. Ila wewe la kufanya kadri anavyokuwa kichwa ngumu ni kumuonyesha hupendezwi na hili ma kisha hata wewe unaweza anza kum neglect. Kwa anayejitambua atajirekebisha.
 
Wasichana umri wa kuolewa bado,

wanawake ndio wanaolewa kwa kua wanaweza kubeba majukumu ya familia
 
kabla ya ndoa tabia yake haiwezi kujidhihirisha kwako baada ya ndoa ndo utajua tabia halisi ya mkeo hasa ukifilisika
 
Wewe ulijuaje amebadilika wakati wewe mwenyewe umebadilika
 
upendo ni pande. mbili.japo wapo unaosema..ila kwa uandishi wako inaonesha kama unaona kumuoa huyo mwanamke kama umemsaidia so unataka usujudiwe
.
 
Kwanza ni vizuri tukajua suala la kusahau kila binadamu ni msahaulifu, si wanawake tu pekee.hata mwanaume anaweza kutafuta kazi mda mrefu lakin akipata husahau alipotoka. Hilo suala lipo kwa watu wote. Tukija kwenye mada yako, kweli nakiri kwamba wanawake kitu ndoa kwao ni something special. Na suala la kusahau huja automatically baada ya kujihakikishia nafasi ya kudumu katika moyo wa mwanaume, na hiyo mara nyingi hutokea katika ndoa za namna mbili. Ya kwanza ni ile yenye mapenzi ya hali juu kutoka pande zote mbilia.zile raha hupelekea kukusahaulisha shida zako za zamani. Na kuna ile aina ya ndoa mke ndo kila kitu. Mwanaume hana kauli. Hii hupelekea mwanamke kuwa na kiburi na kusahau alipotoka na kujiona hawezi kuachwa. Amesahau kwamba alikua ana kesha kwenye maombi kwa ajili apate ndoa. Lakini ndoa ambayo itamfanya asisahau alipotoka, ni ile ndo iliyojaa vipigo, mateso na kila aina ya manyanyaso kutoka kwa mume au ndugu wa mume. Hii humfanya ajute na kujiuliza kwa nini nimeolewa. Haweza kusahau alipotoka. Nimalizie kwa kusema. Binadamu yoyote huwa msahaulifu zaidi anapokuwa kwenye raha kuliko akiwa kwenye dhiki.
 
Halafu subiri kutokee msukosuko wa kipesa na kipato chako kishuke, utajuta kwa nini ulioa.
 
Jamani nina hoja fupi sana hapa, ni kwa nini wanawake/wasichana karibia wote wakishaolewa wanajisahau sana, yaani wanapunguza upendo na mumewe, wanaanza mambo ya kiburi,jeuri,dharau kibao, wanajibu hovyo hovyo.

Yaani kwa kifupi wana change na wanasahau kuwa walikua wanakesha wanasali na kwenda kwa waganga ili waolewe na wakiachwa sasa wataanza, oooh! nina mkosi, nimerogwa, kuna mkono wa mtu.

Binafsi nampongeza mke wangu kwani anajitambua sana.

Hongera zako...
 
Kama anajitambua haya yote uliyajuaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom