Mkuu, kwanza umewahi kumuona mwanaume au mkaka gani hapa Bongo amesuka kwa kutumia Rasta au Kanekalon material kwa style za pick and drop au yeboyebo ya kike kabisa alafu anatembea barabarani au anaingia ofisini kufanya kazi? Hakuna kitu kama hicho mkuu kwani hizo ni style za kike kabisa mkuu wangu...tunachoongelea hapa na ninachokitetea mimi ni hizi style za cornrow hair za kiume...tena kwa kutumia nywele zake za asili.
Lakini kinachoonekana hapa ni baadhi ya wachangiaji kuonyesha au kuaminisha kama hao wakaka au wavulana wanakaa chini kama wanawake na wanasuka yebo yebo au Salsa hair style kama za wanawake...hakuna mwanaume rijali anayeweza fanya hicho kitu na akikifanya basi ni kweli mwanaume huyo atakuwa shoga.