Kwanini wanajeshi na Polisi hawalipi nauli?

Ivi askari akienda kupanda ndege ya binafsi na sare za kazi pale airport ati anaenda kuona familia Mwanza bila malipo ataruhusiwa?.
 
Nimeisoma hii kwa dalubini kali..iko poa sna nakufuata pm

Ninaamini wanajeshi wengi wangependa kuzalisha kwani ndio taasisi wangalau nina imani nayo sio ya wapigaji. Wangepewa combine harvesters, matractor makubwa na serekali itenge maeneo makubwa, jeshi hili lingekuwa ni taasisi inayozalisha kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano sasa kuna sera ya viwanda. Vingeanzishwa viwanda kisha jeshi lipewe kipaombele kwenye kuzalisha malighafi hasa za kilimo kwa ajili ya kiwanda husika. Ni dhahiri hata bidhaa za kiwanda husika zingekuwa za gharama nafuu kwani ni malighafi zilizozalishwa kwa bei nafuu.
 
Kwa hiyo..
1/Wakiingia baa wanywe pia bure.
2/Wakiingia Hotelini wale bure.
3/Wakiingia gesti walale bure.
4/Ndege pia wapande bure.
5/Sokoni wapewe mboga bure.
6/Madukani wapewe bure.

Kama logic ya kupanda mabasi bure ni kuwa maaskari ni watu muhimu sana na wametoa maisha yao kwa ajili ya taifa letu, basi itumike katika nyanja zote za kimaisha ili iwe na mantiki.
 
Kwa Nini unakaa nyumba ya serikali bure wakati unalipwa mshahara? (Kiujumla hizo zinaitwa motisha).
 
Kaulize pale Central Police au Lugalo Military Camp ama pale Ngome utapewa majibu mubashara kabisa.

Ila usisahau kuleta mrejesho hapa JF.
Mwache akarushwe kichura, wala hatakuja kukupa mrejesho wowote.
 
Acha wivu na wewe si uvae gwanda??kama huna njoo nikupe langu na wewe upande free
 
Watu wengine pia wanakazi sensitive.. Basi hii haikuangaliwa kwa macho mawili.hta daktari nae ana kazi sensitive.
 
Acha wivu na wewe si uvae gwanda??kama huna njoo nikupe langu na wewe upande free
Kwanini bure kwenye daladala tu?hiyo Pia ni biashara Kama duka,tax,bodaboda,n.k ambako huwa mnalipa. Acheni kuwaonea wenye daladala
 
Mkuu umesema yote
Ni utaratibu mbovu ndio maana tunazidi kuwa masikini
Nchi za Magharibi kazi ya Police ni sawa na kazi zingine tu.
Police atalipa nauli kama raia wengine uzuri wenzetu huruhusiwi kutembea na vazi la police ovyo ovyo only if upo kazini. Wanajilipia nyumba na gharama zingine si wanalipwa mishahara

Bora Mkoloni arudi black point period!....... tumeshindwa kujiendesha
 
Kwa hiyo sisi tunaolipa nauli hatuna heshima?
 
Ndugu yangu askari yeyote anapokua kwny sare za kazi hawezi kulipa nauli sababu yuko kazini dhahiri,anakulinda wewe na mali mnazomiliki.
Sababu ya pili kuwa wananchi wote wanatakiwa kuheshimu ile kofia yenye nembo huwez kuidai nauli crown.hapo hakuna suala la motisha.
Askar anapokua hayupo kwny sare za kazi atalipa nauli kama raia wengine na hapaswi kujitambulisha ovyo sabab kitambulisho chake hakionyeshwi bila sababu za msingi.wapo askari wengi ambao hawavai sare wao hulipa kama kawaida.
 
Mwache akarushwe kichura, wala hatakuja kukupa mrejesho wowote.

Majimengi ,
Mkuu,
Acha kumtisha jamaa bure.
Wala hakuna kichura wala kimbuzi.

Yeye, aende tu ofisi yao yoyote ile atapata majibu sahihi.

Kisha atuletee mrejesho mubashara hapa JF.
 
Wanaulizaga "Hivi kuna Nafasi Humu"??

Hapo ujue ukisema Ndio .... Hiyo ndo lift yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…