Kwanini wanajeshi na Polisi hawalipi nauli?

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,987
Polisi na wanajeshi ni watumishi kama watumishi wengine. Wakati mwingine wao wanalipwa mishahara mikubwa na marupurupu mengi kuliko watumishi wengine.
Swali langu ni kuwa kwanini watu hawa wanasafiri bure hasa kwenye madalalada? Lengo la kuwafanya wasafiri bure ninini?
Je lengo ni kuwamotisha? Mbona huduma nyingine wanalipa?
Ni kuwazubaisha? Ili waone wanapendelewa huku haki zao zikibinywa?
Inakuaje wanafunzi ambao hawaingizi kipato chochote walipe nauli na wanajeshi wanaolipwa mishara wasilipe nauli? Hii ni sawa kweli?
 
Hili jambo linafikirisha sana ila nafikiri kunamengi ndani yake!

Huenda nikatika hali yakuwaliwaza ili wasisumbuesumbue na kuibua mengi kuhusu kipato chao kwani kiuhalisia wafanyakazi wengi wenye vyeo vya kaaida nchini mshahara wao hauendani na hali za maisha halisi
 
Mkuu mimi hata sishangai, unakuta mtu kama waziri anapata mshahara wa zaidi ya 20m@month lakini anakaa nyumba, ya bure huduma kama umeme, maji na mlinzi analipiwa na serekali. Wakienda hata sehemu za burudani wanaingia bure, kibaya zaidi hata wapambe wanaokuwa nao pia wanaingia bure. Halafu eti wanasimama mbele ya watu pila aibu wanasema wamejitolea kupigania wanyonge. Pumbavu kabisa unapata mshahara wote huo na huduma za bure kisha unasema umejitolea kupigania wanyonge!?
 
Fanya mpango uwe waziri mkuu
 
Polisi na wanajeshi ni watumishi kama watumishi wengine. Wakati mwingine wao wanalipwa mishahara mikubwa na marupurupu mengi kuliko watumishi wengine.
Swali langu ni kuwa kwanini watu hawa wanasafiri bure hasa kwenye madalalada? Lengo la kuwafanya wasafiri bure ninini?
Je lengo ni kuwamotisha? Mbona huduma nyingine wanalipa?
Ni kuwazubaisha? Ili waone wanapendelewa huku haki zao zikibinywa?
Inakuaje wanafunzi ambao hawaingizi kipato chochote walipe nauli na wanajeshi wanaolipwa mishara wasilipe nauli? Hii ni sawa kweli?

Ni kama motisha kwa sababu ya majukumu yao..Ukumbuke au tukumbuke kuwa kazi za Jeshi na polisi ni sensitive na ambapo muda wote anakuwa kazini kwa hiyo ukimuona askari ujue yupo kazini.. Na wasiotozwa nauli, ninavyofahamu mimi, ni wale ambao wako kwenye uniform au sare za kazi...ukivaa kama raia yaani pasipo kuwa na sare askari atalazimika kulipa nauli labda yeye mwenyewe ajitambulishe na kwa staha na siyo kushurutisha...Polisi na jeshi ni vyombo vya dola na vina heshima kubwa...ukivaa uniform ya jeshi au polisi ni heshima kubwa...wanajeshi wamejitolea kufa kwa ajili ya nchi, na wameapa kufa kuilinda nchi...hivyo ni lazima tuwape somesort of motisha...tunawaheshimu...tunasema wewe askari wa JWTZ unatulinda, kazi yako ni kubwa na uko tayari kufa kwa ajili yetu, kwa hiyo hatukutozi nauli...Mtu wa TRA hajaapa kufa kwa ajili ya nchi, wala mwanasiasa, wala mwandishi wa habari, wala mcheza sinema...Kuapa kufa kwa ajili ya nchi siyo suala la mchezo hata kidogo...Askari yupo kazini mahali pote au popote pale...jambazi akiibuka ndani ya daladala na kutaka kupora watu askari au polisi anakuwa kazini immediately kumdhibiti jambazi huyo....wahuni na magaidi wakitaka kuleta fyoko fyoko ndani ya basi la mwendokasi kama yupo askari wa JW au polisi analazimika kujitoa mhanga kuwalinda raia wengine. Raia anakuwa salama pale askari anapokuwepo karibu. Ni vizuri tuwapende askari wetu. Ni kazi sensitive.

Wanafunzi wetu wana utaratibu wa kulipa nauli kwa punguzo....ila kama mambo yakiwa mazuri wanaweza pia kupanda bure kwa utaratibu mzuri wa kuwa na mabasi yao....kuna kazi nyingine nazo ni muhimu kama vile waalimu wanaoelimisha jamii yetu...nao tunawaheshimu...nao tunaweza tukasema, kama alivyojaribu kufanya RC Makonda kwa Dar es Slaam, kwamba ninyi waalimi ni watu muhimu, tunawamotisha kwa kazi yenu nzuri kwa nchi na taifa letu...msilipe nauli...ni lazima tuheshimu profession muhimu...tusizidharau...

Kuwa askari ni kazi kubwa...Askari haogopi ovyo ovyo..siyo kama mwanamuziki mmoja wa kizazi kipya alipooneshwa bastola tu mahali fulani alikimbia na kupotea kwa muda katika eneo hilo
 
Ni kama motisha kwa sababu ya majukumu yao..Ukumbuke au tukumbuke kuwa kazi za Jeshi na polisi ni sensitive na ambapo muda wote anakuwa kazini kwa hiyo ukimuona askari ujue yupo kazini.. Na wasiotozwa nauli, ninavyofahamu mimi, ni wale ambao wako kwenye uniform au sare za kazi...ukivaa kama raia yaani pasipo kuwa na sare askari atalazimika kulipa nauli labda yeye mwenyewe ajitambulishe na kwa staha na siyo kushurutisha...Polisi na jeshi ni vyombo vya dola na vina heshima kubwa...ukivaa uniform ya jeshi au polisi ni heshima kubwa...wanajeshi wamejitolea kufa kwa ajili ya nchi, na wameapa kufa kuilinda nchi...hivyo ni lazima tuwape somesort of motisha...tunawaheshimu...tunasema wewe askari wa JWTZ unatulinda, kazi yako ni kubwa na uko tayari kwa ajili yetu, kwa hiyo hatukutozi nauli...Mtu wa TRA hajaapa kufa kwa ajili ya nchi, wala mwanasiasa, wala mwandishi wa habari, wala mcheza sinema...Kuaapa kufa kwa ajili ya nchi siyo suala la mchezo hata kidogo...Askari yupo kazini mahali pote...jambazi akiibuka ndani ya daladala na kutaka kupora watu askari au polisi anakuwa kazini immediately kumdhibiti jambazi huyo....wahuni na magaidi wakitaka kuleta fyoko fyoko ndani ya basi la mwendokasi kama yupo askari wa JW au polisi analazimika kujitoa mhanga kuwalinda raia wengine. Raia anakuwa salama pale askari anapokuwepo karibu. Ni vizuri tuwapende askari wetu. Ni kazi sensitive.

Wanafunzi wetu wana utaratibu wa kulipa nauli kwa punguzo....ila kama mambo yakiwa mazuri wanaweza pia kupanda bure kwa utaratibu mzuri wa kuwa na mabasi yao....kuna kazi nyingine nazo ni muhimu kama vile waalimu wanaoelimisha jamii yetu...nao tunawaheshimu...nao tunaweza tukasema, kama alivyojaribu kufanya RC Makonda kwa Dar es Slaam, kwamba ninyi waalimi ni watu muhimu, tunawamotisha kwa kazi yenu nzuri kwa nchi na taifa letu...msilipe nauli...ni lazima tuheshimu profession muhimu...tusizidharau...

Kuwa askari ni kazi kubwa...Askari haogopi ovyo ovyo..siyo kama mwanamuziki mmoja wa kizazi kipya aliponeshwa bastola tu mahali fulani alikimbia na kupotea kwa muda katika eneo hilo

Sipingi utetezi wako lakini ni utetezi mwepesi sana. Kila kazi ya mtu ina heshima kwakuwa ina mchango katika nchi hii. Hao askari wanapewa upendeleo huo sio kwasababu eti wameapa kufa kuilinda nchi, bali ndio wanaolinda mamlaka ya watawala. Ukiangalia hizo sekta nyingi hata kama ni muhimu watawala hawazijali sana kwani hizina uhusiano wa moja kwa moja na wewe kukaa madarakani kwa amani. Sasa watawala kwakuwa wengi wanalipwa hela nyingi kuliko hao wanaowalinda, ndio unaona wanawapunguzia ugumu wa maisha kwa kutunga sheria ya upendeleo. Kwa mfano toka baada ya vita vya Iddi Amini ni vita gani nyingine iliyolazimu hao wanajeshi wetu kuonekana wanaifia nchi?

Hao wanajeshi wanapata upendeleo wa wazi hata kwenye maisha ya kawaida sio kwa kuwa ni walinzi wa nchi bali ni walinzi wa watawala. Kila mara nashauri hilo jeshi letu wakati huu wa amani ni bora wangeshiriki kwenye uzalishaji mali hasa kwa serekali kuwapa pembejeo za kilimo, ili walime mashamba makubwa na kuzalisha chakula kitakachokaa kwenye maghali ya serekali ili kupambana na njaa, na sisi wakulima tuachwe tuuze kokote duniani bila usumbufu. Mambo ya kutaka wapakie magari bure eti wanaenda kazini huku hakuna uzalishaji wowote mkubwa na hakuna vita ni kutotundea haki walipa kodi wengine na kutowatendea haki wanajeshi wenyewe.
 
Dah...sitaki kuijadili hoja yako kwani tayari una msimamo kuwa JWTZ au polisi jukumu lao ni kulinda mamlaka...dah...Ipo kazi kweli kweli kuelimisha mtu mwenye msimamo wa aina hii...thanks Ndugu..
 
Sikulazimishi kujadili msimamo wangu hasa kama umejiona huna hoja zenye ushawishi za kuweza kusawazisha huo msimamo wangu. Nina uwezo wa kutosha kuelewa pindi mtu anapokuja na hoja zenye ushawishi. Hao polisi wala sijawataja popote na wala sijaacha kuwataja kwa bahati mbaya kwani wao wapo kazini kila siku kwakuwa ni ulinzi wa raia na mali zao hivyo wao wanaweza kupata kisingizio cha kuwa kazini kila siku. Niliowazungumzia hapa ni JWTZ hasa wakati huu ambao taifa limekaa miaka zaidi ya 30 bila vita vya kulinda mipaka yetu. Hivi unajua mwanajeshi aliyeingia jeshini mwaka mmoja baada ya vita vya uganda anavuka umri wa miaka 50 sasa hajawahi kupigana vita na hajawahi kuzalisha chochote kinachokuza uchumi, zaidi ya kufanya mazoezi ya kijeshi?
 
Na wenyewe wameridhika kupewa huduma kandamizi, hawahoji wala kudadisi (vya bure kudoroja) msemo wa kimakonde wenye maana "Bure ghali".
 
Hili jambo lilishajadiliwa humu na majibu yalitolewa ya kuridhisha ila wewe wadai mkuu wanalipa sana tu try it for own risk
 
Sipingi utetezi wako lakini ni utetezi mwepesi sana. Kila kazi ya mtu ina heshima kwakuwa ina mchango katika nchi hii. Hao askari wanapewa upendeleo huo sio kwasababu eti wameapa kufa kuilinda nchi, bali ndio wanaolinda mamlaka ya watawala. Ukiangalia hizo sekta nyingi hata kama ni muhimu watawala hawazijali sana kwani hizina uhusiano wa moja kwa moja na wewe kukaa madarakani kwa amani. Sasa watawala kwakuwa wengi wanalipwa hela nyingi kuliko hao wanaowalinda, ndio unaona wanawapunguzia ugumu wa maisha kwa kutunga sheria ya upendeleo. Kwa mfano toka baada ya vita vya Iddi Amini ni vita gani nyingine iliyolazimu hao wanajeshi wetu kuonekana wanaifia nchi?

Hao wanajeshi wanapata upendeleo wa wazi hata kwenye maisha ya kawaida sio kwa kuwa ni walinzi wa nchi bali ni walinzi wa watawala. Kila mara nashauri hilo jeshi letu wakati huu wa amani ni bora wangeshiriki kwenye uzalishaji mali hasa kwa serekali kuwapa pembejeo za kilimo, ili walime mashamba makubwa na kuzalisha chakula kitakachokaa kwenye maghali ya serekali ili kupambana na njaa, na sisi wakulima tuachwe tuuze kokote duniani bila usumbufu. Mambo ya kutaka wapakie magari bure eti wanaenda kazini huku hakuna uzalishaji wowote mkubwa na hakuna vita ni kutotundea haki walipa kodi wengine na kutowatendea haki wanajeshi wenyewe.
Mkuu jitahidi uchukue nchi ili uondoe utaratibu wa askari kupanda bure mabasi!! Au unasema hivyo kwa kuwa haupo kwenye madaraka??
 
Askari waboreshewe mishahara yao nao walipe nauli. Ama serekali ijitahidi iwanunulie usafiri wao. Ninaamini jeshi lingeweza kuwa na miradi yake likajitosheleza kwa mambo kama ya usafiri. Kusema wapande magari bure hilo linapaswa kuwa suluhisho la muda mfupi, lakini kwa watu waliojipanga vizuri wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hivyo. Nasema hivi kwakuwa sipo kwenye madaraka, na ningekuwa kwenye madaraka ningehakikisha haya mawazo yangu ya kulifanya jeshi lizalishe mali wakati wa amani linatendeka.
 
Back
Top Bottom