Kwanini wanafunzi wengi wenye uwezo mkubwa darasani huwa watundu na wasumbufu?

DAN LOKOMOTIVE

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,503
1,906
Mara nyingi sana katika safari yangu ya elimu, walimu wamekuwa na tabia ya kusema kwamba uwezo wa mwanafunzi darasani lazima awe anawahi namba, hapigi kelele, awe mara hivi mara vile lakini unakuta wale vipanga wanaokuwa na uwezo (sio wa kariri) na maanisha wale waliokua wanaweza kusolve kila mtego wa maswali hata mwalimu alinyonge vipi, unakuta mara nyingi hawana sifa hizo tajwa.

Mfano;

O-Level kuna jamaa mmoja alikuwa kipanga, ila sikuwahi kumuona akiwa class anasoma mwenyewe. Yeye mwalimu akija ndio anajua kushika daftari, alikua anapiga kelele, anajichanganya na watukutu, kwenye namba kila siku tunachapwa naye, ila kwenye pepa alikuwa anakimbiza. Kuna siku walimu walitushtukiza mitihani siku moja huyu jamaa alichapa A.

A-Level hapa ndo nilishangaa, wengi waliokuwa na uwezo mkubwa walikua madoja. Hakuna kuwahi namba, hivi huwa imakaaje hii?
 
Mara nyingi sana katika safari yangu ya elimu, walimu wamekuwa na tabia ya kusema kwamba uwezo wa mwanafunzi
Wanaelewa haraka, wengine wakimsikiliza tu ticha au kusoma kidogo vinanasa, so hatumii mda mwing kutulia na kusoma soma notes, creative mind, wana active brain, wana apetite ya kujaribu vitu vingi, wana confidence na uwezo wao, ma genius wengine wana history ya kuzingua shuleni ila badae wakaja kufanya maajabu.
 
Tukishaelewa concept inatosha, tutatumia muda kidogo tu kusoma kwa ajili ya kufaulu mitihani........tunahitaji muda mwingi wa ziada ku-relax, kula bata na kufanya ishu zingine kama michezo. Tukirudi kutoka huko tunakuwa fit zaidi kujifunza vitu vipya na siyo kuendelea kukariri mambo yaleyale.
 
Kuna mwanafunzi tulisoma naye sekondari tokea form one kumkuta darasani ni mara moja kwa wiki tena ijumaa.alipiga one ya maana.kwenda six one tena na huko alipochaguliwa shule za serikali kuonekana ni mara mbili kwa mwezi na mitihani tu.
Yupo zake USA sasa na huko kapata uraia na GPA ya maana.
Bahati mbaya mdogo wake alikataa kuishi na mimi sababu ya dini.
 
Akili zao zina uwezo mkubwa na kama unataka kuwakeep busy kuwatuliza wape vitu vigumu saanaaa...maana hivi vya kawaida wanavimaliza mapema wanavielewa wanashindwa kutumia akili zao zote hence wanaboeka ndo maana wanakuwa watukutu
 
Back
Top Bottom