Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 361,154
- 831,823
Dunia imeachwa njia panda kuhusiana na kifo na mazishi ya the world most wanted creature Osama bin laden.... Mpaka sasa kuna pande mbili... Upande wa kwanza ukiamini kuwa Osama ni kweli aliuawa na upande wa pili ukiwa na mashaka juu ya kifo hicho.
Mimi nimechagua upande wa kuamini kifo chake hivyo nitaenda na bit hiyo hata kama mojawapo ya dhana za kijasusi za CIA ni kupenda kuaminisha uma kinyume cha uhalisia na ukweli
na nitaendelea kuamini hivyo mpaka hapo ukweli mwingine wenye ithibati zisizotia shaka utakapoanikwa.
Osama ni pando na zao la wamarekani kwenye vita ile ya wasoviet kwenye milima mirefu na mabonde ya Afghanistan... Osama akiwa ni jasusi aliyefanya kazi yake kwa mafanikio na umahiri mkubwa dhidi ya warusi, akiwafanyia kazi wamarekani miaka ile ya 80.
Ni mpaka pale alipokuja kuwageuka mwaka 1991, pengine ni baada ya kumtelekeza (kama kawaida yao wamarekani ), akiwa ni askari command na jasusi mbobezi mwenye maarifa mengi juu ya vita na propaganda zake, lakini pia akiwa na cash ya kutosha Osama aliwageuka wamarekani. Yaliyofuatia yote yanajulikana..
Pigo lile la majengo pacha ya THE WORLD TRADE CENTER.... vita ya Afghanistan na kumsaka Osama kwenye milima ya Tora bora na tani za mabomu ya kila aina yaliyoshushwa kule, mashambulizi mbalimbali yaliyofuatia duniani kwenye mashina ya wamarekani na kumsaka kwa gharama kubwa na muda mrefu...
Wamarekani walifikia kumdhani huyu si kiumbe wa kawaida bali jini... Yani Osama bin laden ni jinimtu.
CIA wana kila nyenzo kwenye mapambano na kupata habari, wana mpaka kitengo cha siri sana cha mambo ya giza na huwa hawapuuzi dhana yoyote ile mpaka waithibitishe vinginevyo.
Mengi yaliyofanyika kwenye msako wake hayajasimuliwa, muda ukifika yatasimuliwa.. Lakini hili la kudhani ni kiumbe jini lilipata nguvu kubwa kwakuwa pamoja na kuwa na nguvu kubwa za kijasusi, tech, mitambo ya kijeshi nknk lakini walishindwa kumpata
Jini makazi yake ni baharini, lakini jini mkorofi makazi yake ni ndani ya chupa iliyofungwa vizuri na kutupwa baharini
kuna simulizi kuhusu jini ndani ya chupa/kibuyu cha ajabu.
Walichokifanya wamarekani hakina tofauti na hekaya za jini ndani ya chupa... Baada ya kumpata walimuua na kumfungia kwenye chupa ngumu (jeneza).. Kisha likafungwa vifaa vya mawasiliano na kwenda kulichimbia baharini kwenye kina kirefu cha maji na wanapajua.
Hadithi za kusema walitaka kupoteza kumbukumbu zake sio za kweli kabisa, wangeweza kumchoma moto(cremation) ama hata kumtumbukiza kwenye pipa la acid nknk ... Tabu yote ya nini kwenda kumzika baharini?
Japo hawawezi kukubali kwa sasa lakini wamarekani waliamini Osama ni jini korofi na akipatikana panapomfaa ni ndani ya chupa baharini