Kwanini wamama ni wahanga sana wa Makanisa?

Bonesmen

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
929
991
Kiukweli wateja wakubwa kabisa ya makanisa ni wakina mama yani Base ya Sadaka wanategemewa wao ,Mwana mama yuko radhi auze vitu vyake vya ndani apeleke kanisani. Yani hawasikii na ni kushinda kutwa kucha ktk majumba ya ibada bila kujali wana familia majumbani hili limekaaje kwa hawa ndugu zetu waliotokea ubavuni kwetu ni upeo mdogo wa kupambanua mambo au ni wingi wa matatizo ndo maana wanajiweka sana ktk imani za dini?
 
Ila ukijaribu kuwaangalia hao kina mama walioko wengi kwenye makanisa utakuta mikononi wamebeba picha za wanaume zao, watoto wao ama hata nguo za mume wake na watoto wake pia..Sasa unaweza ona wengi hawaendi kwa matatizo yao binafsi ila ni matatizo yetu sisi wanaume tuache Ulevi, Uasherati ama hata familia iinuke kiuchumi..
 
babu umesema ukweli kuna baadhi ya watu wamewafanya mtaji mama zetu kwa jili ya matatizo ya kidunia na si tu kanisani hata waganga wa kienyeji wamewafanya kina mama ni wateja wa kudumu
 
Kuna tatizo kubwa nadhani kina mama ni wepesi kuamini na ni rahisi kudanganyika, sina tatizo na nia zao lakini tatizo linakuja kwamba hata mchungaji/kanisa lipate scandal kiasi gani bado hawapambanui mambo na kukimbia wataishia kusema ni shetani tu etc sadaka ndo usiseme bora ale dagaa ila sadaka akatoe kubwa kuliko kipato chake kwa siku.
 
WanaJF kina dada/mama (Housegirl, Valentina, Evelyn Salt, Victorie, nk) fanyeni tafiti ya hili mtupe matokeo. Ni suala la kijamii au hata la kiuchumi ambalo linahitaji majibu sahihi.
 
Ni Vyema Kumkimbilia Mungu, siku zote Ndiyo Maana wakina Mama wamepata Neema Kubwa Kutoka kwa Mungu, Natunapoelekea wakina Mama watakuwa na Nguvu kubwa ya Kiuchumi maana Mungu uwapa Neema Wamtafutao.

Angalia nyumba nyingi utakuta Baba ameshafariki Kamwacha Mama, wanaume Hamshangai? Ni kutokana na Madharau kiburi na majivuno na Kutokumtafuta Mungu, Kazi kukesha Mabaa na Nyumba ndogo.

Waacheni wakina Mama wamtafute Mungu, Maana Hakuna Aliye Matafuta Mungu, Mungu Akamwacha, Nyie wadhiakini kwa kila neno baya lakini Mtalia na kusaga Meno.
 
Endelea kuota tuu kwanza amka kumekucha ukafanye usafi leo ni siku ya usafi.
 
Ila ukijaribu kuwaangalia hao kina mama walioko wengi kwenye makanisa utakuta mikononi wamebeba picha za wanaume zao, watoto wao ama hata nguo za mume wake na watoto wake pia..Sasa unaweza ona wengi hawaendi kwa matatizo yao binafsi ila ni matatizo yetu sisi wanaume tuache Ulevi, Uasherati ama hata familia iinuke kiuchumi..
Asante mkuu!

Wanawake ndo wameachiwa jukumu la kuhakikisha vitu katika familia vinasonga mbele. Mama huhakikisha mumewe na watoto wake wako katika hali nzuri.

Na nitamshangaa mtu anayemkataza "mkewe" kushiriki IBADA. Huyo ni mpumbavu, na atakuwa anachezea bahati bila kujua impact yake.

Kutokana na majukumu hayo ya kifamilia, Mungu anawasisitiza wanawake kuwa washiriki Ibada ili wapate maongozo sahihi.

Hekima iliyo ya kweli wataipata kutoka kwa Mungu pekee.

"Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe." - Mithali 14:1

"Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa." - Mithali 31:30

Kwa kumalizia, niliwahi kufundisha kuhusu nafasi ya mwanamke katika familia kama lango. Hii ni kwa sababu wanawake wanabeba "womb" na kizazi hupitia kwake. Hivyo, ni muhimu kwa mwanamke kutojiingiza kwenye maagano yatakayoharibu uzao wake. Suluhisho ni moja, kuingia Agano na Mungu aliye hai.

"Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke ATAMLINDA mwanamume." - Yeremia 31:22

Ninategemea waume/watoto mfurahie wake/mama zenu wakifanya ibada.

Kama isingelikuwa MAMA yangu, familia yetu ingekuwa wapi?! Aliokoka mwanzoni na sacrifices zake KIIMANI zilisababisha baba kuacha pombe na uhuni mwingine na kuwa a great dady and husband.

Na sisi watoto, tume enjoy malezi hayo kwa sababu yake. Alikuwa anakwenda kuhudhuria camps za maombi kwa ajili ya Familia. Kwa wakati huo ni ngumu kuelewa, ila IMPACT/MATUNDA yake tunayaona sasa. Familia ni moja na yenye upendo japokuwa watoto tupo mbali katika kujitegemea.

MAMA yangu ndiye "prayer warrior" wangu. Her prayers keeps me moving.

Mungu awabariki akina MAMA wote wacha Mungu.
 
Makanisa ya kilokole yanajua shida nyingi ziongoza kwa wanawake
Matatizo ya uzazi
Matatizo ya ndoa n. K
WANAJUA mtaji mkubwa ni wao
Wanafahamu wakimshika mama hapo tayari na watoto pia wamewashika,wataanza kuja kusali nyumbani huku wamekulenga wewe baba mwenye mji, usipokuwa stable hata ndoa yako itakuwa majaribuni kwa kuitwa wewe ndiye chanzo cha matatizo kwenye hiyo familia.
 
Back
Top Bottom