Kwanini 'Wajinga' wanatoboa kimaisha haraka kuliko sisi 'Great Thinkers’?

Kwanini 'Wajinga' wanatoboa kimaisha haraka kuliko sisi 'Great Thinkers’?

Ujinga ni nini,? Kutokusoma mpaka level ya chuo huyu mtu tumuite mjinga.

Kuna vitu vina kaukweli, kuna kwingine sio sahihi

Maisha hayana formula.. muhimu kupambana, katika wa3 unaona wametoboa kuna maelfu wamebuma?
Ujinga ni ile hali ya kutokujua jambo au kitu flani.

Hakuna mtu asiye mjinga maana hakuna mtu ajuaye kila kitu.

Watu huchanganya ujinga na upumbavu.

Hata Julius Nyerere alikuwa na ujinga.

Hata Albert Einstein alikuwa na ujinga.

Ujinga kwa Kiingereza ni ignorance.
 
Ujinga ni ile hali ya kutokujua jambo au kitu flani.

Hakuna mtu asiye mjinga maana hakuna mtu ajuaye kila kitu.

Watu hucanganya ujinga na upumbavu.

Hata Julius Nyerere alikuwa na ujinga.

Hata Albert Einstein alikuwa na ujinga.

Ujinga kwa Kiingereza ni ignorance.
Uko sahihi, kibongo bongo mjinga imezoeleka mtu ambae hana elimu, amefeli shule.
 
Leo naomba tuweke vyeti vyetu vya chuo na zile "A" zetu za sekondari pembeni, tuzungumze ukweli unaouma. Nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi na kugundua jambo moja la kushangaza sana mitaani:

Asilimia kubwa ya watu tunaowachukulia kama 'watu wa kawaida' au wasio na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, wanapiga hatua kubwa sana za kifedha kuliko sisi ambao vichwa vyetu vimejaa "critical thinking".

Hapa nimejaribu kuchambua kwanini hawa jamaa wanatuacha kwenye mataa, huku sisi tukiendelea kubishana kuhusu sera za uchumi na siasa za kimataifa:

  • Ugonjwa wa 'Analysis Paralysis': Msomi akitaka kufungua genge la nyanya, atafanya SWOT Analysis, atachora Business Plan ya kurasa 40, ataangalia Market Volatility, na kusoma vitabu vya Robert Kiyosaki. Mwisho wa siku, anaona mradi una hatari (Risk) asilimia 60%, anaacha. Yule 'mjinga' asiyejua SWOT analysis, anaamka asubuhi, ananunua nyanya, anapanga kwenye fungu, anauza. Baada ya miaka miwili, msomi bado anasoma Rich Dad Poor Dad, yule jamaa anamiliki maduka matatu.
  • Utumwa wa 'Brand' na Hadhi: Sisi watu wenye akili tuna shida moja—tunaogopa kuonekana wa kawaida. Mtu mwenye digrii yake anaona aibu kuuza mitumba kariakoo kwa sababu "haishabihiani na hadhi yake". Yuko tayari kukaa ofisini na kiyoyozi, akilipwa laki tano kwa mwezi na bosi ambaye aliishia kidato cha pili, lakini bosi huyo ndiye anayemiliki ghorofa anayopanga huyo msomi. Sisi tunalinda Brand isiyolipa, wao wanasaka pesa.
  • Kizungu Kingi, Salio Dogo: Kwenye mitandao na majukwaa kama haya, tunajua sana kupanga hoja. Tukianza kuchambua Macro-economics au makosa ya serikali, unaweza kudhani sisi ni washauri wa Benki ya Dunia. Lakini ukiingia kwenye Mobile Banking zetu, salio linasoma elfu kumi na mbili. Wakati sisi tunabishana kwa Kiingereza kinyoofu, kuna 'machinga' yupo busy anapokea oda za maelfu ya dola kutoka China kwa kutumia "Google Translate". Pesa haitambui Grammar, inatambua mzunguko.
  • Hatari ya 'Perfectionism' (Kutaka Kukamilika Kila Kitu): Sisi "Great Thinkers" tunataka kila kitu kikae kwenye mstari kabla ya kuanza. Tunataka mtaji kamili, ofisi nzuri, na mazingira rafiki. Watu wa mtaani wana falsafa ya kikatili: "Tuanze, tutarekebisha mbele ya safari." Na mara nyingi, mitaani ndiyo shule halisi. Wanakosea, wanajifunza, wanapata hela. Sisi tunasubiri wakati sahihi ambao haufiki kamwe.
Hitimisho:Sijasema tusome au tusiwe watu wa kufikiri. Lakini huu uzito wetu wa kiakili (Critical Thinking) mara nyingi unageuka kuwa gereza letu la hofu. Tunajua sana hatari za kushindwa kiasi kwamba tunaogopa hata kujaribu.

Je, wakuu mnakubaliana na hili? Au ni mimi tu nimeamka na mawazo ya kifukara leo? Tiririkeni.

View attachment 3562994
Siku zote Mungu hakunyimi vyote. Anaweza akakunyima akili ya darasani, halafu akakupatia uwezo wa kujiamini (self confidence)!! Hakika hii kitu imewasaidia vilaza wengi kupata mafaniki wanayo tulingishia sasa.
 
Maisha yanahitaji risk takers kitu ambacho mwenye akili nyingi hawezi kukifanya! Mfano mzuri angalia ndoa, wengi hawaingii kwa sababu wana-calculate kuanzia mwanzo hadi mwisho itakavyokuwa bila kuingia!
Siyo mwenye akili nyingi sema aliyekaririshwa mawazo ya ambao walifel kama yeye wakajikusanya kijikundi mahali wakatunga walichokiita maarifa wakawauzia watu ndiyo tunayoishi nayo hadi leo

La saba B anayesaini cheque ya 50mill huku mtaani anazungusha zaidi ya mill 500 na PhD holder anayezurura Makumbusho na Kariakoo pale Uhuru akitapeli simu na laptop kwako nani mwenye akili nyingi?nenda UDSM professor anafundisha biashara kwenye makaratasi ukimpa mtaji mill 100 akakifanye anachokifundisha hajui hata aanzie wapi.
 
Siyo mwenye akili nyingi sema aliyekaririshwa mawazo ya ambao walifel kama yeye wakajikusanya kijikundi mahali wakatunga walichokiita maarifa wakawauzia watu ndiyo tunayoishi nayo hadi leo

La saba B anayesaini cheque ya 50mill huku mtaani anazungusha zaidi ya mill 500 na PhD holder anayezurura Makumbusho na Kariakoo pale Uhuru akitapeli simu na laptop kwako nani mwenye akili nyingi?nenda UDSM professor anafundisha biashara kwenye makaratasi ukimpa mtaji mill 100 akakifanye anachokifundisha hajui hata aanzie wapi.
Well said comrade!
 
1. Ugonjwa wa "Analysis Paralysis"
"Great thinkers" huwa na tabia ya kuchambua kila kitu kwa undani sana. Wanawaza hatari zote zinazoweza kutokea (risks), hali ya uchumi, na uwezekano wa kufeli. Hii inawafanya washindwe kuanza.
Wajinga: Mara nyingi huwa hawawazi madhara ya mbali. Wao "hukurupuka" na kuanza, na matokeo yake wanajifunza wakiwa ndani ya mchakato.
2. Imani ya "Kujua Kila Kitu" dhidi ya "Kujifunza kwa Vitendo"
Watu wenye akili nyingi mara nyingi wanataka kuwa na mpango uliokamilika kwa 100% kabla ya kuchukua hatua.
Wajinga: Wanakubali kuwa hawajui, hivyo hawana aibu kuuliza au kufanya makosa. Maisha yanatunuku zaidi vitendo (action) kuliko nadharia (theory).
3. Hofu ya Kushindwa na "Image"
"Great thinkers" mara nyingi wanaogopa kuonekana wamefeli kwa sababu wana "brand" au heshima ya kulinda kama watu wenye akili.
Wajinga: Hawana cha kupoteza. Wakifeli leo, wanaamka kesho na kujaribu kitu kingine bila hofu ya watu watasema nini. Uhusiano wao na kushindwa ni rafiki zaidi.
4. Dunning-Kruger Effect
Hii ni kanuni ya kisaikolojia ambapo watu wenye uwezo mdogo hujiamini kupita kiasi (overconfidence), wakati wenye uwezo mkubwa hujitilia shaka (self-doubt).
Kujiamini huku (hata kama ni kwa upungufu wa maarifa) huwapa msukumo wa kuingia kwenye fursa ambazo "mwenye akili" angeziona ni hatari sana.
5. Kurahisisha Mambo (Simplicity)
Biashara na mafanikio mengi yanahitaji kanuni rahisi: "Nunua kwa 5, uza kwa 10."
Mwenye akili nyingi ataanza kuwaza kuhusu mfumuko wa bei, kodi za kimataifa, na mzunguko wa fedha mpaka fursa inapotea. Yule anayeonekana mshamba anapiga hesabu ya haraka na kuingia mtaani.
Muhtasari: Dunia haimlipi anayejua mengi, inamlipa anayefanya mengi na kutatua matatizo ya watu. Siri ni kuchanganya ufikiri wa "Great Thinker" na uthubutu wa yule unayemuita "Mjinga."
huo mstari wa dunia inmlipa anaefanya mengi na sio anaejua mengi unapiga juu na chini kaa nao kwa umakini🤣🤣🤣🤣🤣
 
Maisha hayategemei sana huo u "Great thinker" wako. Maisha ni mambo mengi, kuna nyota, stadi za maisha, kipaji, bidii, bahati na maarifa sahihi n.k.

Nyongeza: Afrika na bongo kwa ujumla, mambo mengi ya kijinga ndio waga yanaleta hela na kutoboa kimaisha. Huu ni uzoefu wangu. 😁
 
Hakuna mjinga aliyefanikiwa. Ili ufanikiwe lazima uwe na maarifa au taarifa fulani ambayo wengi hawana.
Mfanya biashara anaweza kupata faida kwa kununua bidhaa sehemu kwa bei ndogo kisha akaja kukuuzia kwa bei kubwa ukanunua kwa sababu hujui bidhaa inapatikana wapi au hutaki usumbufu wa kuipata huko kwa bei nafuu. Mteja akipata ufahamu ujue mfanya biashara faida yake inapungua, chukulia mfano wa biashara ya wazi kama bolt au taxify
 
Mtu anakuambia kujenga Guest house ni kuzika tu pesa!😁 huyo ataajiriwa milele!!😁

Dangote kawekeza $20M kwenye kiwanda kikubwa zaidi Africa cha kusindika nyanya (tomato sauce) halafu mara kibao kinafungwa kwa kukosa nyanya (malighafi)!!😁 ama kuzalisha kwa 20% tu ya uwezo wake wa tani 400,000/mwaka.

Hiyo Dangote cement ya Mtwara nayo kawekeza $500M kwa kupigwa kabobo tu na JK kwamba angepewa na mgodi bure wa makaa ya mawe na angejengewa reli mara msamaha wa kodi etc

Katika mazingira hayo,hawa wasomi wa Jf wangekokotoa vitu kibao mwishowe wangeona uchuro tu.
 
Maisha hayategemei sana huo u "Great thinker" wako. Maisha ni mambo mengi, kuna nyota, stadi za maisha, kipaji, bidii, bahati na maarifa sahihi n.k.

Nyongeza: Afrika na bongo kwa ujumla, mambo mengi ya kijinga ndio waga yanaleta hela na kutoboa kimaisha. Huu ni uzoefu wangu. 😁
Sio bongo tu hata ulaya na amerika.
 
Kuna siku nilikuwa nasikiliza podcast moja ya masuala ya kijasiriamali. Kuna mtoa mada mmoja mtu mwenye biashara zake kubwa tuu Kenya. Akasema katika mwekezaji hakikisha biashara/miradi yako 10, miradi miwili unaiwekeza kwenye kundi kubwa la WAJINGA. 😁
Akasema Afrika wenye hela na mafanikio wengi ni wajinga, na hawana kwa kuzipeleka. Akasema hakikisha unateka mindsets za wajinga ili wawe wateja wa bidhaa/huduma yako.
Biashara za mtandao na content creators wanatengeneza fedha nyingi kwa branding za huduma zao, sababu mwafika anatumia mtandao kuburudika. Akasema mwafrika ndie mtu anaetaka kufanya kazi kidogo na kupata mafanikio makubwa na kujistarehesha na kujipa utukufu.
Akasema Afrika matajiri wa kweli wanatumia kila mbinu kuficha utajiri wao, na maskini wa kiafrika wanatumia kila mbinu kuonyesha "utajiri" wao. Mwafrika ndie mtu pekee anaetumia muda mwingi kusali na kuabudu kuliko kufanya kazi.
Niliona kama ana hoja hivi yule bwana.
 
Back
Top Bottom