Kwanini Waisrael walikataa kuja Uganda?

Siyo kweli kuwa ilikuwa Uganda, bali walikuwa wamepewa kule kwenye nyanda za juu za rift valley huko Kenya. Walikataa kwa sababu waliitaka ardhi ya Israeli ya King David. Kuna sehemu nyingine nzuri zaidi ya Israel wakati huo walizopewa lakini wao waliitaka hiyo hiyo Kanaan yao. Kwa mfano walipewa sehemu fulani ya Urusi, sehemu fulani ya Australia, sehemu fulani Argentina, sehemu fulani ya Japan, Sehemu fulani ya Ethiopia, na sehemu fulani Guiyana lakini zote wailizikataa wakaamua kurudo kwao jangwani.
 
Waisraeli asili yao ni Israel ndio nchi yao ya ahadi chimbuko lao na mtu kwao hata kama kunamazingira magumu kiasi gani, ndio maana wao walikataa kupelekwa Uganda kwenye ardhi yenye rutuba na mito na hiyo ilitokana na matendo walioyapata ugenini GERMANY kwa Hitler. Na hii sio ajabu mfano mdogo: Somalia 1991 vilivozuka vita MAREKANI iliamua kuwachukua wakimbizi wa Somalia wenye asili ya Tanzania(WAZIGUA) kuwapatia uraia wa marekani, baadhi yao wakakataa kwenda USA na kuomba warudi kwenye nchi yao ya asili Tanzania tanga, na mpaka sasa hivi wapo
 
anhaa, ahsante kwa elimu hii. inaonekana hawataki kupoteza hata chembe ya asili yao!
 
🙏🙏🙏
 
Walipewa Uganda au Argentina walikataa maana walitaka sehem yenye asili yao nadhani ndio maana walipewa jangwa la Negeb wakiamini wangekata tamaa jamaa David akakubali na kuahidi atalisha dunia kutoka jangwani
 
Walipewa Uganda au Argentina walikataa maana walitaka sehem yenye asili yao nadhani ndio maana walipewa jangwa la Negeb wakiamini wangekata tamaa jamaa David akakubali na kuahidi atalisha dunia kutoka jangwani
Jamaa david ndo nani mkuu
 
Story zingine bwana hazina kichwa wala miguu,kwa miaka hiyo yote 1947 iliyopita walipo ondoka wake warejeshwe 1948 yani miaka yote 1947 hawakuona umuhimu wa kurudi kwao?
Kumbuka hata walipokuwa Misri walikaa utumwani miaka 430 ndiyo wakarudi kwao
 
Waisraeli sio makaburi, wanajua nchi yao ilipo na wanao ushahidi wa kutosha kuwa mahali walipo ndio kwao. Kama Jerusalem ingeweza kuhamishiwa Uganda, wangekubali kwenda Uganda.

Vv
Haa haa hawakutaka kuitwa wakuja
 
Ni Uganda
 
Siyo Uganda, ni maeneo ya Rift valley Kenya. Eneo lote lile la Kenya na Uganda lilikuwa ni koloni la waingereza wakiitwa Britrish East Africa Hakukuwa na Kenya au Uganda wakati huo.
Sawa
 
Kama wewe ni muislam au ni mkristo unajua kabisa kwamba israelites kwao ni pale Jerusalem na huo ugomvi wao na hao ndugu zao wa kambo ni 5000 iliyopita unless una mashaka na imani yako
Hizi story za imani fake za ajabu sana. Ni sawa wangoni watake kurudi south Afrika eti kudai ardhi mababu zao walipokuwa wanaishi. Au aje mtu hapo kwenu adai ni kwake eti Mungu wake kasema hilo eneo ni nchi yake ya ahadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…