Kwanini Waislam hawajifunzi?

Kwanini Waislam hawajifunzi?

wakati wa kikwete makamu alikuwa wao. wakati wa Jpm makamu ni wao na waziri mkuu pia lakini hilo hawalioni. 🙁
 
Au Mkulu amemsahau katika Ufalme wake nini?
 
Usipoiunga mkono CCM unamuunga nani na vyama vyenyewe vya upinzani ndio hivi ambavyo havina malengo ya kwenda IKULU? Vinaacha Sera zao za msingi, havina wagombea wenye sifa na vimejijenga katika Propaganda rahisi ambazo hata mtoto mdogo atashtuka tu!!

Tulieni basi simmeshawachagua hao wenye sifa MALALAMIKO ya nini????? tena hawana propaganda za kitoto
 
Wapinzani ndo hawajifunzi,mwaka 2000,mrema sijui kwa kutojua kuwa atawaogopesha waislamu,akamtanguliza kakobe na kuzunguka nae nchi nzima,waislamu wakawa alarmed wakapigia ccm,


mwaka 2010,maskofu wakaporomosha matamko kama hawana akili nzuri dhidi ya jk,waislamu wakawa alarmed wakajiuliza hivi tuchaguwe padri kweli agaisnt jk?,no fking way,,wakachagua ccm.

Mwaka 2015,wagombea wote christian,
hamad,tukashuhudia lowasa akiandamana na ngwajima kila kona huku ngwajima akitetema cheche,watu wakaona hii haijakaa sawa,kugeuka upande wa jpm,amekazana,"NITAKUWA RAIS WA WATU WOTE,DINI ZOTE,KABILA ZOTE"

Wakaona labda hapa kidogo kuna ka unafuu,

so khalifa kukiunga mkono ccm katika chaguzi za nyuma kwa mtizamo wangu,ccm walionekana nafuu kuliko hao wapinzani,sababu upinzani mfano cdm walionekana kuwa na hostility attitude towards muslims.
 
Kuhama chama si suluhisho. Kwanini hao wa kwenye chama wasibadilike.umesema mwenyewe sheikh wakati wa utawala wa JK alikaa kimya labda aliridhishwa na utawala huo sasa kama mambo hayaendi sawa asiseme?
Mtoto akiunyea mkono suluhisho siyo kuukata ccm ipo na utaendelea kuwepo watakuja marais waislam na wasio waislam miaka ijayo so madaraka yanapita lakini chama kitabaki.
 
Unapo muunga mkono mgombea basi kwanza yawepo makubaliano
sio unamuunga mkono mgombea halafu unaanza kulialia akishashinda...
Wagombea matapeli wanadanganya wakati wa kampeni.wakishaingia ikulu wanabadilika.
 
Boss umeongea point sana.sema hawa jamaa hawaaminiki ni wanafiki,hawana umoja,wanasalitiana kila kukicha.mfano ishu ya Zanzibar wote wanaabudu nyumba moja ya ibada.lakini wanafanyiana unafiki bila kificho.huku Bara kuna Bakwata iliyokubali kuwa Tawi la Chama/Serikali mpaka wanajengewa ofisi.wanaombewa msaada wa mskiti kwa Mfalme kama kipaumbele cha taifa, Wapo waislam wanaojimbua ila hawana platform ya kueleweka.pia Hawaweki vipaumbele kujenga mashule ili waelimike.wanakomalia miskiti kwanza watoto wao Elimu muhimu kwao ni vyuo vya Dini.sasa ukuu wa mkoa/wilaya/ukurugenzi na Elimu za madrasa wapi na wapi.
Tafadhali bwana.
Usitusemee waislam, huo unafiki , hatuaminiki, tunasalitiana kila kukicha haya yote umeyatoa wapi?
Usitake kutufarakanisha bwana.waislam tu wamoja ila kwa Tanzania tumekuwa wavumilivu kupitiliza.
 
Usipoiunga mkono CCM unamuunga nani na vyama vyenyewe vya upinzani ndio hivi ambavyo havina malengo ya kwenda IKULU? Vinaacha Sera zao za msingi, havina wagombea wenye sifa na vimejijenga katika Propaganda rahisi ambazo hata mtoto mdogo atashtuka tu!!!!
Haya basi hatutaki kusikia malalamiko kwasababu CCM mmeipenda wenyewe.
 
Hii mada bwana Boss unataka kuichkulia kama kete ya kuwahamisha waislam kutoka CCM kwenda chadema.
Nimekustukia tutabaki CCM watabadilika wao hata kama si leo Kama kesho.madaraka yanapita CCM itabaki.
 
wakati wa kikwete makamu alikuwa wao. wakati wa Jpm makamu ni wao na waziri mkuu pia lakini hilo hawalioni. 🙁
Mlivyokuwa mnatoa matamko kila wiki mlikuwa hamlijuwi hilo?
Kikwete aliwavumilia sana nyie.sidhani kama JPM angeweza kuvumilia yale matamko ya baraza la maaskofu.
 
TATIZO MBADALA WA CCM HAKUNA, CHADEMA WANA ALERGY NA WAISLAM, CUF CHAMA CHA KIKANDA ZAIDI, TUNABAKIA NA ZIMWI TULIJUALO MAANA HATA LIKITUTAFUNA LITATUACHA HAI JAPO HOIIIIII
 
Sina hakika ninachokiandika kitawafikia wahusika lakini baada ya kuona threads mbili zinazomhusu Sheikh Khalifa akimlaumu Magufuli kwa udini wa kupendelea wakristo wenzie nimeona nichangie kidogo.

Sheikh Khalifa amekuwa akizungumza haya toka wakati wa Mwinyi ndio Rais
cha ajabu alipoingia Kikwete Ikulu sheikh Khalifa akanyamaza kimyaa
kuzungumzia msalahi ya waislam na mara kwa mara alikuwa
akimualika Kikwete msikitini na alishiriki kuwapigia kampeni wote
Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Sasa leo anaanza kuongea haya haya aliyo yaongea zaidi ya miaka 20 iliyopita
na watu wanamshangilia.

Maswali ya kujiuliza ni haya?

Je, ni lazima waislam waiunge mkono CCM?

Why kila mara malalamiko haya haya lakini ukija uchaguzi hawa hawa kina Khalifa wanaipigia debe CCM?

Je, masuala ya uteuzi hasa teuzi za wakuu wa mikoa na wilaya si masuala ya kikatiba?

Si katiba ya Warioba kwa mfano ilipinga Rais kuteua wakuu wa wilaya?
Je, kina Khalifa walikuwa wapi kuwashawishi waislam waunge mkono katiba ingine ambayo itaondoa Rais kufanya teuzi na wananchi wakiwemo waislam kuja kuchagua viongozi moja kwa moja?

Nionavyo mimi badala ya kumbembeleza Magufuli au Rais yeyote kuteua wakuu wa wilaya, waislam na wakuu wa mikoa waislam ni bora hizo nafasi ziwe za kuchaguliwa kwa kura na wananchi wachague wanaeona anawafaa.

Suluhisho la madai ya teuzi kwa waislam ni katiba ambayo itawapa wananchi nguvu ya kuchagua wanao wataka ngazi za mikoa na wilaya.

Rais apunguziwe mamlaka ya kuteua watu wengi ambao wengine ndo kama hivyo asilimia 95 ni wa dini yake.

Hivyo ili hilo lifanyike waislam waungane na wote wanaopenda demokrasia kudai katiba mpya ambayo wananchi watakuwa na nguvu na katiba itakayoleta tume huru ya uchaguzi.

Hili la kumlalamikia Magufuli linapaswa kukomeshwa. Nyerere alalamikiwe
na Magufuli pia? Madai yale yale miaka zaidi ya 30?

Waislam hawajifunzi kitu?
Tatizo letu kubwa viongozi wetu wa Kiislam ndio wanafki wakubwa , watu wa kila siku kulia lia na kujipendekeza wenzetu wakristo kidogo wana misimamo yao
 
Mkuu wangu The Boss naomba unifahamishe kiduchu nimekusoma hapo juu unasema Sheikh Khalifa alikuwa anamualika Kikwete Msikitini ni Msikiti upi huo?
 
Back
Top Bottom