hii kitu inaniumiza sana. ndio maana nasikiliza south african gospel sababu Bongo hakuna kitu. yani PC yangu ukiichek nina nyimbo za kizulu zaidi ya 1000 maana jamaa wanajua kuabudu na kusifu sijui sisis waswahili tunakwama wapi,
japokuwa John Lisu anajitahidi kufanya live DVD recording lakini hatuwezi kumsikiliza yeye tuu tuna hitaji Tamasha kubwa kama la SPIRIT OF PRAISE la south africa ambapo utaona wasanii/ waimbaji wengi zaidi ya 15 wakifanya live DVD recording na wanauza sana hadi kufikia Platinum sell, sio kazi ndogo. pia wenzetu wa Zimbabwe wameanza kama mchezo lakini sasahivi wapo vizuri sana. nafuatilia tamasha lao la ZIMPRAISE ambalo ni zuri sana. sijui sisi waswahili shida ni nini? kazi porojo tuuu
Mr. Msama Alex alianzisha Tamasha la Pasaka lakini nalo naona halifanyi vizuri sana najua sababu ya low budget na technology lakini ilikuwa ni Idea nzuri sana. Natamani hii kitu kingefanyiwa muundo mpya a kupewa jina jipya Mfano. TANZANIA PRAISE Halafu kila mwaka inafinyika mara moja ingependeza sana. baada ya kufanya live DVD recording Dar es salaam pia wangezunguka semu kama Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na mikoa mingine mikubwa nadhani ingekuwa safi sana