Kwanini waende Kanisani au Kuhiji Vatican na mabango?

Kwanini waende Kanisani au Kuhiji Vatican na mabango?

Endasak Masqaroda

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
1,728
Reaction score
3,957
Habari wana jukwaa!

Huko mitandaoni nimeona habari kuhusu jamaa wa LBTQ kuwa wameruhusiwa na Kanisa Katoliki kuhiji kwa mara ya kwanza huko Vatican.

Nimeona pia humu kuna uzi mmoja kuhusu habari hiyo. Kuna watetea kuwa Kanisa linapokea wadhambi wote, i.e wezi, majambazi, makahaba n.k wanapohitaji kurudi kwa Mungu kwa maana hata Yesu alikula na kunywa na wadhambi.

Hoja yangu mimi ni kwanini watu hao waruhusiwe kuingia Kanisani na alama/ishara zao? Tatizo sio kuingia Kanisani, kwa maana mtu akivaa tu modestly akaenda ibada kuna tatizo?

Kwanini hawa watu wanaruhusiwa kuingia na nguo zenye maandishi, vipeperushi na ishara zote zinazo watambulisha? Mbona kama vile ni mpango wa watu wazito kupitia Kanisa?
Kwani wezi na makahaba tunawatambua tunapokuwa nao Kanisani?

Why LBTQ waruhusiwe kujitangaza kanisani? Lengo ni nini?

1000207159.jpg
 
Wanavaa alama zao za upinde kuashiria kua hatua hiyo ni ushindi kwao dhidi ya Kanisa au dhidi ya amri za Mungu,

Huo ni mpango wa watetezi wa hao LGBTQ ili huko mbeleni ije kuonekana au kuzoeleka kua uchoko ni jambo la kawaida tu hata kwenye Nyumba za ibada! lengo kuu ni kuupromote ushoga,hakuna lengo lingine zaidi ya hilo,zingine ni porojo tu.
 
Kwa kifupi PAPA sio kiongozi wa kidini tu bali ni kiongozi wa kimfumo wa dunia/kisiasa na ajenda za siri za taasisi za siri za kidunia zinazosimamiwa na kuzimu toka enzi..
DOLA YA RUMI toka ikiwa na nguvu ikitawala dunia karne nyingi zilizopita,iliwaua mitume wa Yesu Kristo na kuzuia injili ya Yesu isihubiriwe wala biblia isitumike karne hizo nyingi zilizopita.
Lakini baada ya kuona UKWELI hauwezi kuzuiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi...huwezi kupinga injili ya Kristo kwa kuwaua mitume na wahubiri na kuzuia biblia zisisomwe...iliposhindikana kuungamiza Ukrusti na injili ya kweli ya Kristo

Walichokifanya walidanganya kuigiza kama walikubali kuupokea ukristo na kuahidi kuacha upagani wao wa miungu yao mingi ya KIRUMI YAKIPAGANI..
ILA KIUHALISIA waliingiza upagani kwenye INJILI YA KRISTO kwenye Ukristo...halafu wakaongeza mafundisho yao na na tamaduni zao za KIPAGANI kanisani..wakaziita ni amri za kanisa...na kuondoa baadhi ya vifungu na kuongeza mafundisho yao ya kipagani katika ukristo.

Mifano michache sana ya vifungu walivyoviondoa mfano
amri ya pili ya MUNGU ambayo Musa alipewa na Mungu katika amri kumi za Mungu.alizopewa Musa na Mungu
Kut 20:2-5

Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao

utaona hapa Mungu anakataza watu kuchonga sanamu,ila kwa vile wao ya tamaduni zao ni kuchonga masanamu na miungu ya masanamu ,wakaamua kuyabadilisha na kuchonga sanamu za mitume na watakatifu aua sanamu wanayosema ni ya YESU,MARIA NA YOSEFU na nyingine ..lakini lengo la hizo sanamu sidhani kama ni kwa utukufu wa Mungu ,mana Mungu amesema hafurahishwi na sanamu hata kama ni za watakatifu au vitu vilivyoko mbinguni

Zamani hawa mababa wao watakatifu na mababa viongozi wao wa kiroho walikuwa wanauza kwa waumini wao mpaka vyeti vya msamaha wa dhambi,KWAMBA baba mtakatifu binadamu mwenzako anaweza kukuuzia cheti cha msamaha wa dhambi wa miaka kadhaa kadiri ya ulivyoliopia,wakati biblia inakataza kumuita mtu mwingine yeyote baba kwa maaba ya kiroho ,tunaye baba yetu mmoja tu wa kiriho ambaye ni Mungu,mwana na roho mtakatifu.
Na jina tulilolipewa upaswalo kuokolewa kwalo ni jina moja tu la YESU hakuna jina lingine na yeye Yesu ndiyo njia na kweli na uzima...Wakaleta HIRIZI zinaitwa ROZALI ni sawa na hirizi za maji ya upako,mafuta ya upako,keki za upako n.k

Wakaleta mambo ya POMBE kuruhusu ulevi wa pombe

wakaleta vitu vingi vya kipagani waka uchanganya ukristo KANISA LA KWANZA LA MITUME wa yesu kanisa la KIROHO likachanganya na upagani wa mila na tamaduni za KIRUMI zikaingizwa kanisani/upagani ukaingizwa kanisani..tofauti na ukristo wa mwanzo asilia injili asilia ya kweli ya mitume wa Yesu .
Toka hapo mauaji ya mitume na katazo la mahubiri ya injili ya kweli ikakoma maana UKRISTO ukawa umechanganya na upagani wa KIRUMI.

MPINGA KRISTO NI NANI
ANTI CHRIST ni kitu chichote au mtu yeyote anyaechukua nafasi ya YESU KRISTO kiroho na kufubdisha mafundisho ya uongo
Yani mfano mtu anataka badala ya watu waombe moja kwa moja kwa Mungu ila waombe kupitia yeye au yeye yeye ndiye awe baba wa kiriho badala ya Mungu ,amekalia KITI cha uongozi mkubwa duniani wa dini ya kikristo na anahubiri kristo mdomoni ila moyo wake uko mbali na Yesu Kristo na hafanyi matendo yale anayoyapenda Yesu,na anahubiri mafundisho ya uongo yanayotoka kwa baba wa uongo shetani yani mwenye kuudanganya ulimwengu..
MFANO MMOJA WAPO ndio hayo mafundisho ya NDOA ZA JINSIA MOJA..huko mbeleni zitaanza kufungishwa makanisani kabisa..

na huyu mpinga KRISTO au papa (black papa na white papa) wanafanya kazi kufanikisha agenda za joka kuu shetani.

Halafu atatokea NABII WA UONGO..huyu atasafishiwa njia na kiongozi mkuu wa kanisa papa ili alete mafundisho ya uongo mkuu ,haya yate yameshaanza kutokea.
UNYAKUO UMEKARIBIA SANA ...halafu DHIKI KUU ITAFUATA na chapa ya mnyama hesabu yake 666 na micro chip.
 

Attachments

  • images - 2025-09-11T222254.195.jpeg
    images - 2025-09-11T222254.195.jpeg
    9.9 KB · Views: 33
  • quote-antichrist-is-the-pope-and-the-turk-muslim-together-a-beast-full-of-life-must-have-a-mar...jpg
    quote-antichrist-is-the-pope-and-the-turk-muslim-together-a-beast-full-of-life-must-have-a-mar...jpg
    60.2 KB · Views: 34
Wanavaa alama zao za upinde kuashiria kua hatua hiyo ni ushindi kwao dhidi ya Kanisa au dhidi ya amri za Mungu,

Huo ni mpango wa watetezi wa hao LGBTQ ili huko mbeleni ije kuonekana au kuzoeleka kua uchoko ni jambo la kawaida tu hata kwenye Nyumba za ibada! lengo kuu ni kuupromote ushoga,hakuna lengo lingine zaidi ya hilo,zingine ni porojo tu.
Hii point.
 
mpinga kristo ni chochote kinachochukua nafasi ya Kristo.
Maandiko yanatufundisha tunaye baba yetu mmoja tu aliyeko mbinguni na kwa maana ya kiroho tusimuite yeyote baba hapa duniani..YANI BABA YETU KWA MAANA YA KIROHO ni Mungu/Yesu/Roho mtakatifu.
Mpinga Kristo sio pekee wale wanaopinga uwepo wake pekee tu ni zaidi ya hao.
Hata WALIOKALIA KITI CHA MUSA NA KUBEBA FIMBO YA MUSA lakini wanafundisha mafundisho potofu yaani wameingiza upagani na agenda za kuzimu kanisani na kuwafundisha wanakondoo mafundisho yatokayo kwa shetani..badala ya ile kweli ya neno la kweli la Mungu.Mafundisho potofu..ili kuwapoteza waumini katika dhambi.
Tuzijaribu sana hizi mafundisho kwa kuangalia neno la Mungu,tipime hizi imani..tukifuata tu mafundisho eti kwa vile BABA MCHUNGAJI sijui baba askofu sijui papa mtakatifu kwa vile amesema na wewe unafuata unaamini tu unafuata ,wengine ni maajenti wa shetani wamevaa kanzu ya kondoo kumbe bi mashetani halisi..utapotea ..SOMA NENO SHIKA NENO..omba mwenyewe kwa Mungu,Mungu atusaidie ,Roho mtakatifu atifundishe kujuua neno lake..kataa kufuata mafundisho ya UONGO.
 
Tunaishi katika nyakati/zama za mwisho kabisa huku unabii kuhusu UNYAKUO WA WATAKATIFU WALIOKO DUNIANI /KURUDI KWA YESU MARA YA PILI kukiwa kumekaribia sana kwa mujibu wa ufunuo na maandiko.
WAKATI WAKATI TULIONAO NI MCHACHE SANA...sisi kama RAIA WA MBINGUNI tunaosafiri safari ya kuelekea MBINGUNI kwenye makao yetu ya kudumu,tukijua hapa duniani sio kwetu na tunapita tu na maisha ya duniani ni ya muda mfupi sana.

1)hatujui saa wala dakika ambayo tutatwaliwa tutaondolewa/MUDA wetu wa kuishi hapa duniani utaisha ama unyakuoa utatokea ,hivyo kila dakika ya MUDA tulionayo tukiwa hapa duniani ni mali endapo tuki itumia kwa utukufu wa Mungu ,na itakuwa ni hasara tukitumia muda wetu mwingi zaidi na kuwekeza TUKIZITUMIKIA MALI na kupenda pesa na kuzitafuta pesa,
nyakati za mwisho.
watu watapenda pesa kuliko chochote ,kuliko kumpenda Mungu,kuliko utu..upendo kati ya mtu na utu UTAPOA ,watu watapenda viti/mali kuliko utu/Mungu..na wengi hali wakiitamani pesa watajifarakanisha na imani yao na kujichomankwa maumivu makali.
PIA wengi sasa watakuwa wanaitumikia pesa badala ya kumtumikia MUNGU ,na huwezi kuwatumikia ma bwana wawili,yani umtumikie Mungu na utumikie Mali,lazima utampenda mmoja zaidi .
Biblia imetupa maneno ya hekima katika hili..kwamba tulinde sana moyo wote kwani ndipo zitokapo chemichemi za uzima kwa maana kule hazina yako iliko ndiko uliko moyo wako yaani kama utawekeza zadi katika kiyafikia mafanikio ya hapa duniani kuliko unavyowekeza katika hazina yako ya mbinguni kwa Mungu, mkwamba ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ilivyo kwa tajiri kwa sababu moyo wako utakuwa zaidi kule ulikowekeza MUDA wako zaidi na hiyo pia ni IBADA YA SANAMU KUTUMIKIA MALI..badala ya Mali zitumike kumtumikia Mungu,ikiwemo MUDA ,muda nao ni mali unagawaje muda wako katika masaa 24 ya siku ,unawekeza zaidi wapi huko ulikowekeza zaidi ndiyo ibada yako ndiyo moyo wako uliko..

watu wengine hatuji kwenye ibada kusali kama kuna kazi ya kuingiza ipo inakuhitaji kufanya MUDA huo ambayo itakuingizia hela au lipo jambo ambalo inaliona ni muhimu kuhudhuria au kufanya MUDA huo,tunakuja kwenye ibada muda ambao tunafikiri hatuna mambo mengine dearest ya kufanya muda huo.
Ila biblia inatumbia tuutafute kwanza ufalme wa mbingu,na mengine yote tutazidishiwa,na kwamba BWANA asipoujenga mji au asipoulinda mji yeye aujengao na kuulindao afanya kazi bure.
Kama unakusanya bila uwepo/kumtanguliza Mungu basi haukusanyi bali UNATAPANYA yani ni sawa na kuweka katika MFUKO ULIOTIBOKA.
Msingi imara wa kujenga/ kufanya jambo lolote ni kujenga juu ya MWAMBA IMARA ambao ni YESU.
hata dhoruba ikija jambo lilojengwa kwa kuanza na msingi imara YESU halitatikisika/halitatetereka halitabomoka.
Na mtu mwenye akili nyingi na aliyechagua fungu lililo JEMA ni yule tu anayemtanguliza na kumtegemea Mungu wakati wote na muda wote..GOD FIRST(MUNGU KWANZA)mengine yote yafuate NYUMA baadae.
Heri anayemtumikia Mungu kuanzia wakati wa UJANA WAKE mpaka mwisho amechagua fungu lililo JEMA.
Hakuna aliyewahi kumtumikia Mungu halafu BWANA akampungukia akamuacha yeye na uzao wa watoto wake.
Kumtumikia MUNGU sio ujinga ,wala sio kupoteza MUDA ,vijana wanaoimba kwaya kanisani au kuhubiri injili au kufanya kazi za kanisa SIO KWAMBA NI WAJINGA au wanapoteza MUDA au hawafanyi kazi au wanachezea muda wao ,ila nawaonea wivu wamechagua fungu lililo jema ,na hawa NDIO WENYE AKILI..na watauona mkono wa Mungu katika maisha yao na watoto wao..SADAKA WALIYOITOA YA MUDA WAO wa ujana wao katika kumtumikia Mungu.

SIOKWELI kwamba watu WOTE ambao tunapitia hali duni za kiuchumi,hatujajipata kiuchumi,bado tuna jitafuta kimaisha kwamba ETI hatufanyi kazi kwa bidii,ama hatuna akili,ama ni wavuvu ama ni wazembe..la hasha ,WAPO bbaadhi yaa masikini wanafanya kazi kwa bidii,wamesoma kuliko wengine ,wanaomba ajira ,wanajishighulisha na wanamtumikia MUNGU lakini bado WAKATI WA BWANA kuwainua hauhafika...SARA alipata mtoto katika uzee wake ..MUNGU huwa anajibu kwa wakati wake ,hachelewi wala hawai.

Tusijipambanie kwa nguvu zetu wenyewe,ipo njia ionekanayo ni njema machoni pa mwanadamu ila mwisho wake ni mauti,

PIA TUSIJILINGANISHE NA MTU YEYOTE
Utaona mwenzako wa umri rika lako ama mnafanya shughuli moja ama mnapokea mshahara sawa ,ama mnalingana elimu,umri ,n.k..lakini ghafla unaona mwenzako mmeanza pamoja ila yeye ana mafanikio makubwa kuliko wewe,
HUJUI hayo mafanikio ameyapataje...MAISHA SIO MASHINDANO haushindani na yeyote,kila mtu anakusudi lake na ameitwa kutumika kwa nafasi yake na wakati wake na kuna vitu tofauti vipawa na karama tofauti kwa watu tofauti na hata vidole vya mikono yako havilingani.Na kila mtu na kila jambo lina wakati wake.
WAKATI wa Mungu ni sahihi,tuwe na IMANI isiyokuwa na mashaka ,TUMAINI,na UVUMILIVU..na yale matunda ya Roho mtakatifu..tukikosa hivi ndio utaona IBRAHIMU na SARA walipofika ukomo wa uwezo na akili za kibinadamu katika kusubiri kupata mtoto ,wakajipigania wao wenyewe wakaishia kupata mtoto ISHIMAILI ,lakini Mungu alikuwa amewaandalia ISAKA. ukikimbia kwa haraka ,USIHARAKIE MAISHA ,utajikuta hata kazini unachukua RUSHWA,UNAIBA /ufisadi,wizi,unadhulumu unafanya biashara haramu,madili ili UPATE MAFANIKIO YA HARAKA HARAKA..ukijipambania mwenyewe kwa akili za mwanadamu..na hiyo njia hata kama inaonekana ni njema machoni pa wanadamu ila mwisho wake ni MAUTI

.kwa hiyo hata ukichelewa kupata MAFANIKIO kama mtoto kazi,nyumba na gari ndoa,kazi/ajira,mgonjwa umekosa AFYA,n.k

Mungu ATAKUREJESHEA kicheko (Isaka),atakurejeshea wakati /ataukomboa wakati/muda hiyo AFYA iliyougua atakurudishia afya,na miaka iliyoliwa na tunutu,nzige,madumadu.

YOTE KATIKA YOTE
Tumtangulize Mungu kwanza pamoja na mbio zetu za kutafuta mafanikio ,pesa na misha ya hapa duniani ambapo sipo kwetu tunapita,tuwe na kiasi,tufanye yote kwa utukufu wa Mungu.
GOD FIRST..MUNGU KWANZA.
 
Back
Top Bottom