SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,916
Good morning ladies and gentlemen,
Jana nilipata nafasi ya kuangalia boli la AFL. Sina mengi ya kusema maana nimepumzika kuongelea sana kuhusu mambo ya mpira huku mitandaoni ila nina maswali mawili.
Kuna ishara ya vidoli viwili kwa kila mkono ambavyo wachezaji wa Al Ahly waliifanya baada ya kufunga goli la kwanza la kutangulia na ni ishara hiyo hiyo waliirudia baada ya kurudisha goli la pili. Ile ishara ina tafsiri gani?
Pili, nani alitoa ushauri kuweka katika jezi za Simba zilizozinduliwa kwa ajili ya AFL maneno "Simba vs Al Ahly"? Katika maisha yangu hapa duniani sijawahi kuona timu ya mpira inacheza mechi ya kiushindani halafu katika jezi ikaweka jina la timu pinzani.
Jezi zilivyozinduliwa nililiona hili nikasema ngoja nisubiri hadi nitakapoona jezi za Al Ahly zilivyo maana inawezekana timu zote zitavaa design hizo. Kwa ajili ya washabiki siyo mbaya kutoa jezi za namna hiyo kama kumbukumbu ingawa nayo inaleta maswali, Simba haikuwa inaamini ina uwezo wa kuvuka hatua hii hadi kutoa jezi za mechi moja.
Kauli zadhaa za hivi karibuni za Mwenyekiti Salum zilikuwa zinaonyesha haamini Simba itavuka hatua hii. Kiufupi jezi za wachezaji zisingeitaja Al Ahly, ingetosha tu kusema "African Football League 2023".
Mengine nayaacha kama yalivyo. Kuna uzi niliwahi kuuleta hapa kuna jambo umenikumbusha ila ngoja niuache.