Al Ahly ikiitoa Simba itakuwa ni dharau kubwa sana

Mr Alpha

Senior Member
Jul 31, 2018
195
522
Mechi kati ya Al Ahly na simba ni kisasi ambacho ni kati ya dubwana lenye nguvu dhidi ya kijana mdogo, mechi ya kariba hiyo ni rahisi japo ngumu. Al Ahly kupangwa na simba ni kama bahati kwao maana wanauzoefu wa kuitoa simba, ni Simba yenye deni la kufuta uteja huo.

Simba inapaswa kutumia kila mbinu kuhakikisha awamu hii lazima Al Ahly apishe njia vinginevyo tunatolewa kama kawaida na dharau itaendelea kudumu kwamba hatuwawezi Al Ahly

Ukiangalia mechi mbili zilizopita za Super League Simba ilipambana vizuri mno ila ikaruhusu magoli ya kijinga kabisa magoli ya uzembe usio kifani

Itaendelea kuwa kibonde wa AL Ahly mpaka lini? hakika inatosha

Ni muda muafaka wa Simba kulazimisha heshima haijalishi Al Ahly wana ukubwa gani, awamu hii inabidi wapishe njia

Kamati ya ufundi ihakikishe kila mchezaji wa simba ataepata nafas kwenye mechi dhidi ya Al Ahly ajue sio mechi ni kisasi lazima kupambana kama jihadi, matokeo ni lazima sio majaliwa lazima Mwarabu apigike

Inawezekana kabisa mbona wale wabrazil Fluminense waliwapakua goli 3 kirahisi kabisa kwenye klabu bingwa dunia?
ff44868cf441efdf6d234aa5ff8d2531.jpg
 
Huo uteja wa kutolewa na Al Ahly umeanza lini? Unajua takwimu za timu hizo mbili katika mechi zao 6 zilizopita? Unajua wamekutana mara ngapi katika hatua ya mtoano hadi kutengeneza huo uteja unaodai?

Wazee wa propaganda mpo kazini.
Kwenye hiyo mechi Simba ni Underdog kwa Al Ahly ila kwenye mpira lolote linaweza kutokea...
 
Neno "underdog" mnalitumiatumia labda bila kuelewa maana yake hasa. Hakuna kigezo chochote unachoweza kutumia kumuita Simba "underdog" katika mechi hiyo.
Sio mshindani hana Kombe la CAF anashindana na mtu mwenye mataji mengi ya mpira kwa Afrika ndio Timu bora ya Karne hata Yanga au Mamelodi akicheza na Al Ahly ni Underdog tu ingawaje matokeo yeyote yanaweza kutokea..
 
Sitabishana na wewe ila kaulizeulize watu wako wa karibu watakuelekeza ili siku nyingine ujue ni mahali gani sahihi pa kulitumia hilo neno.
 
Kilala kheri mtani , ni muda wa kuwaonesha Tanzania tuko serious hatuna jambo dogo
 
simba kafungwa na kumfunga ahly marangapi kimahesabu
Mechi hizi zipo kwenye mfumo wa kutoana sio kufungana Timu zinaweza zikafungana ila moja ikatoka kutokana na idadi ya magoli iliyofungwa ndio kinachotokea kwenye hatua hii ingawaje walitumia hiyo sheria kwenye makundi pia kwa Yanga kuwafunga CRB goli nyingi zaidi ya wao ila Points wapo sawa ikabidi wapite Yanga bila hata mechi ya mwisho kuchezwa...
 
Sitabishana na wewe ila kaulizeulize watu wako wa karibu watakuelekeza ili siku nyingine ujue ni mahali gani sahihi pa kulitumia hilo neno.
Wewe ni underdog kwa Al Ahly ndio ukweli wenyewe hata Yanga nae vile vile kwa Mamelod. Al Ahly kakuzidi kila kitu, yaani hata humkaribi ardhi na mbingu.

Sometimes tunazipenda timu zetu ila kwenye ukweli tuongee,wewe subiria bahati ila kiuwezo kama timu na quality ya mchezaji mmoja mmoja wa Al Ahly na ww,ni ardhi na mbingu ukija kwenye miundombinu na uwekezaji ndio kabisa humsogelei na ndio maana ww ni underdog.

Kitakacho ivusha Yanga na Simba ni bahati, ila kiuuwezo wote ni underdog.
 
Mechi hizi zipo kwenye mfumo wa kutoana sio kufungana Timu zinaweza zikafungana ila moja ikatoka kutokana na idadi ya magoli iliyofungwa ndio kinachotokea kwenye hatua hii ingawaje walitumia hiyo sheria kwenye makundi pia kwa Yanga kuwafunga CRB goli nyingi zaidi ya wao ila Points wapo sawa ikabidi wapite Yanga bila hata mechi ya mwisho kuchezwa...
umekosa
 
Sitabishana na wewe ila kaulizeulize watu wako wa karibu watakuelekeza ili siku nyingine ujue ni mahali gani sahihi pa kulitumia hilo neno.
Mkuu ungekua unajua maana yake ungeeleza hapa maana mimi umeniuliza nimekujibu kwa mifano toa mifano ya Underdog hapa hata Ulaya nipo tayari sio uongee mambo ya mpira kwa watu wa mpira harafu useme nenda kaulize nyumbani..
 
Mechi kati ya Al Ahly na simba ni kisasi ambacho ni kati ya dubwana lenye nguvu dhidi ya kijana mdogo, mechi ya kariba hiyo ni rahisi japo ngumu, bwana mdogo asipotumia akili kubwa na mikakati anatifuliwa mtaro. Al Ahly kupangwa na simba ni kama bahati kwao maana wanauzoefu wa kuitoa simba, ni Simba yenye deni la kufuta uteja huo.

Simba inapaswa kutumia kila mbinu kuhakikisha awamu hii lazima Al Ahly apishe njia vinginevyo tunatolewa kama kawaida na dharau itaendelea kudumu kwamba hatuwawezi Al Ahly

Ukiangalia mechi mbili zilizopita za Super League Simba ilipambana vizuri mno ila ikaruhusu magoli ya kijinga kabisa magoli ya uzembe usio kifani

Itaendelea kuwa kibonde wa AL Ahly mpaka lini? hakika inatosha

Ni muda muafaka wa Simba kulazimisha heshima haijalishi Al Ahly wana ukubwa gani, awamu hii inabidi wapishe njia

Kamati ya ufundi ihakikishe kila mchezaji wa simba ataepata nafas kwenye mechi dhidi ya Al Ahly ajue sio mechi ni kisasi lazima kupambana kama jihadi, matokeo ni lazima sio majaliwa lazima Mwarabu apigike

Inawezekana kabisa mbona wale wabrazil Fluminense waliwapakua goli 3 kirahisi kabisa kwenye klabu bingwa dunia?View attachment 2941076
Ngja TUONE
 
Ungekua unajua ungeeleza hapa hujui Mpira unataka kuongea mambo ya mpira kwa watu wa mpira...

Mkuu ungekua unajua maana yake ungeeleza hapa maana mimi umeniuliza nimekujibu kwa mifano toa mifano ya Underdog hapa hata Ulaya nipo tayari sio uongee mambo ya mpira kwa watu wa mpira harafu useme nenda kaulize nyumbani..
Tuongee kimpira na uwe tayari kujifunza pale unapoambiwa ufahamu wako hauko sahihi katika jambo uliloliongelea ndiyo utampa nafasi upande wa pili akueleweshe. Ila ukishaanza kutumia lugha za "haujui mpira", si kila mtu atakuwa na time na wewe baada ya hapo.
 
Wewe ni underdog kwa Al Ahly ndio ukweli wenyewe hata Yanga nae vile vile kwa Mamelod. Al Ahly kakuzidi kila kitu, yaani hata humkaribi ardhi na mbingu.

Sometimes tunazipenda timu zetu ila kwenye ukweli tuongee,wewe subiria bahati ila kiuwezo kama timu na quality ya mchezaji mmoja mmoja wa Al Ahly na ww,ni ardhi na mbingu ukija kwenye miundombinu na iwekezaji ndio kabisa humsogelei na ndio maana ww ni underdog.

Kitakacho ivusha Yanga na Simba ni bahati, ila kiuuwezo wote ni underdog.
Kwa kuwa wewe ni underdog unalazimisha na mwenzio awe hivyo hivyo ili upate usingizi
 
Tuongee kimpira na uwe tayari kujifunza pale unapoambiwa ufahamu wako hauko sahihi katika jambo uliloliongelea ndiyo utampa nafasi upande wa pili akueleweshe. Ila ukishaanza kutumia lugha za "haujui mpira", si kila mtu atakuwa na time na wewe baada ya hapo.
Samahani ila haujui mpira kama unataka tuongelee underdog kati ya Yanga na Mamelodi tufanye mambo mengine tu mkuu..
 
Kwa kuwa wewe ni underdog unalazimisha na mwenzio awe hivyo hivyo ili upate usingizi
Tatizo lenu mpira hamjui, hivi nitajie eneo lolote lile, kitimu,mchezaji mmoja mmoja, kiuwekezaji na kimiundo mbinu ambalo mmewazidi Al Ahly?

Jitahidi uujue mpira ili uachane na ushabiki maandazi na oya oya kama wale mashabiki wanao kimbilia kamera baada ya mechi kuisha na kupiga kelele na kuanza kumpa lawama kocha.

Wewe jiandae kisaikolojia hiyo tar 29 kwani ww ni underdog unacho tegemea ni bahati.
 
Samahani ila haujui mpira kama unataka tuongelee underdog kati ya Yanga na Mamelodi tufanye mambo mengine tu mkuu..
"Underdog" ni neno la kiingereza linalotumika katika maeneo na muktadha tofauti na maana yake kwa kiasi kikubwa huwa ni ile ile pale inapotumika. Kwa hiyo kusema eti sijui mpira inaweza isiwe hoja nzito sana kutoka kwako.

Simba siyo underdog kwa Al Ahly katika mechi hii ya 29/03. Kwa upande wa Yanga pamoja na kwamba sitamshangaa wala kumbishia nikisikia mtu akiwaita Yanga ni underdog kwa Mamelodi katika mechi yao ya 30/03 lakini binafsi bado nao nitasita kuwaita hivyo. Naweza kusema Yanga siyo favorite kushinda hiyo mechi ila sitawaita underdogs, hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom