Kwanini Wabunge wa CCM wanapenda sana Kumjaribu na ni kama vile Wanamdharau sana Katibu Mkuu wao Dkt. Bashiru?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,912
Nakumbuka ni mwaka huu huu na Rekodi zipo tena akiwa ‘ amefura ‘ kabisa Mithili ya Mbogo aliyejeruhiwa Katibu Mkuu wa CCM na Mwanazuoni Dkt. Bashiru Ally Kakurwa alipiga Marufuku Wabunge wote wa CCM Kuanzisha Mashindano ambayo yanabeba Majina yao ( kwa Mfano GENTAMYCINE CUP ) na badala yake akawataka wakiyaanzisha wawe wanatumia tu Majina ya ‘ Waasisi ‘ wetu Wakuu nchini.

Cha Kushangaza kabisa tena akiwa mkavu na akijiamini huku ‘ akijimwambafai ‘ zake kupitia Kituo cha Redio cha Clouds fm Kipindi chao cha Michezo cha Saa 3 Usiku cha ‘ Sports Extra ‘ Mbunge wa Mpanda Mjini ( CCM ) Ndugu Sebastian Kapufi amepanga Kufanya Mashindano ya Kugombea Ng’ombe huko Jimbon Kwake Mpanda Mjini ambayo Mwenyewe amesikika akisema yataitwa ‘ Kapufi Cup ‘ na Yeye ndiye atadhamini kila Kitu ( Watoto wa Mjini wanasema atasimamia Shoo Mwanzo Mwenga )

Katika Kumbukumbu zangu nadhani hii sasa ni ama mara ya Pili au ya Tatu naona baadhi ya ‘ Matamko ‘ ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ‘ yanadharaulika ‘ hasa na wana CCM hali ambayo inaanza Kunishtua na Kunifanya nijiulize Maswali mengi ambayo yanakosa majibu dhidi ya Uimara na Mvuto wake Katibu Mkuu wa CCM Bashiru mbele ya wana CCM Wenzake.

Je, unadhani ni kwanini Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ‘ Matamko ‘ yake mengi yanapuuzwa na wana CCM?
 
Bashiru huwa anahisi wanaccm ni wanafunzi wake wa chuo,mambo ya siasa ni mambo ya ridhaa tu


USSR
 
Back
Top Bottom