Let's go at it and see nani ni mshabiki.
Unachosema hapa ni kwamba watu wa Syria wanapendana sana sema Marekani na Urusi ndiyo sababu ya hawa watu kuchinjana lakini baina yao hakuna chuki.
Hii si kweli.
Wanaopigana ni Syrians. Pia wana chuki baina yao za kihistoria. Assad ni Allawite anayefungamana na Shia. Wengi wa waasi wengine ni Sunni. Allawites do not want to go back to the mountains, if you know what I mean.
Au unakataa kwamba hakuna chuki baina ya makabila na madhehebu hayo Syria?
Anamuadabisha vipi kwa kumuondoa Assad? Will that stop Gazprom operations?
Urusi na Ulaya zimefanya biashara ya gesi miaka mingi. Gazprom na BP walikua washirika wa kibiashara. Leo EU inaweka sanctions kwa Urusi huku ikitegemea gesi kutoka Urusi.
Let's say you are correct. Marekani ikishamwadabisha Urusi, nani ata-supply gas Ulaya?
Unaongea kama waasi ni wamoja. Ndani ya waasi kuna ugomvi na vita baina yao. Ndani ya waasi kuna ISIS na vikundi vya mlengo huo.
Unataka kusema marekani inamsaidia ISIS?
Kitu kingine hugusii, mbona husemi Qatar na Saudi wanawasaidia waasi wenye mrengo wa Sunni? Au huu ni uongo?
Unajua ukisema hili utaonyesha ukweli kwamba waarabu si wamoja. Sasa hapa nani mshabiki?
Gesi inatoka wapi? Israel? Unajua gas reserves za Israel au unjaribu kuungaunga hadithi.
Tanzania ina gas reserve nyingi kushinda Israel. Hilo bomba litakua linapitisha nini?
Acha utani.
Nitasema wewe unaongelea kishabiki.
Unakataa ukweli kwamba kuna chuki baina ya waarabu za kikabila na kidhehebu, na kukimbilia kusingizia Wamarekani kwa ugomvi wao ukijaribu kuonyesha kana kwamba hawa watu wanapendana sana na wakichonganishwa kidogo tu na Marekani wananchinjana kama kuku.
Ndugu, hata mimi na wewe hapa tumepishana kimtazamo, tunapigana vita ya maneno najua huko uliko unafurahi unatafuta majibu yako unarusha! Na mie vile vile nacheka nafurahi then natafuta la kukujibu ninaloona sahihi!! Hivi akatokea mtu mwingine huko akatumia mwanya wa tofauti zetu kutuchonganisha zaidi kiasi kwamba nikahakikisha hukai kwenye keybord tena maisha yako yote !! Halikadhalika na wewe pia ukaanza kuhakikisha natokemea kabisa katika ulimwengu huu, hapo kaka mkubwa utasema nini? Mimi na wewe tulikuwa hatupendani kwa sababu ya kupishana hoja na mtizamo?
Maana yangu ni kwamba utofauti wa mawazo na mtizamo upo kila mahali hapa duniani!! Hao Waarabu mie huwa siwapendi kabisa, utofauti wa Sunni na Shia haukuwa chanzo cha yote haya ila kuna waliotumia advantage hiyo kuhakikisha hao watu hawali tena pamoja na hawalali tena pamoja kwa maslahi yao (kikubwa mafuta).
Kaka mgogoro wa Urusi na Marekani hujawahi kuusikia! Kiburi cha Urusi kinatokana na gesi anayosambaza Ulaya maana akiikata kuna mataifa yataumia sana na hilo ndilo linalohofiwa! Marekani kwa sasa inatafuta kusambaza gesi kutoka Mashariki ya kati kwenda Ulaya ili kuidhibiti Urusi hasa anataka akiweka vikwazo viweze kuwekeka kweli lakini kubwa ni kumaliza ushindani uliopo ambao ulianza tangu kuna USSR. Unadhani kwa nini kwenye kutafuta suluhu ya Syria kulikuwa kuna mitizamo miwili mikali sana kutoka Marekani na kutoka Urusi ambayo mitizamo hiyo ilikuwa haiwezekaniki kukaa meza moja kiasi kwamba naona sasa hivi wameamua kuacha mambo kama yalivyo?
Kuwa katika ukanda mmoja na nchi moja wapo ikasaidia waasi si kitu cha ajabu, hata hapa kwetu nchi zilizopo kwenye maziwa makuu kila siku tunakaa mezani kutafuta amani lakini wakitoka nje Uganda na Rwanda wanaenda kusidia waasi kusihambulia Congo! Ninachopingana na wewe hapa ni swala moja tu, mimi nilisema kuwa machafuko ya nchi za Arabuni yamechagizwa na mataifa makubwa yanayonufaika na rasilimali zinazopatikana Arabuni wewe ukasema mimi ni muongo!! Hivi utakapokuwa unapambana na mimi akatokea mtu akakusogezea rungu karibu ili unimalize, tutasema ulipata msaada au hukupata msaada??
Hawa jamaa upande mmoja wanatumia silaha na vifaa vya kivita vya Kirusi ilhali upande wa pili za Kimarekani na Kichina!! Kumbuka ni katika nchi moja, hilo nisizungumzie sana inawezekana wamenunua katika masoko tofauti.
Ni hivi mimi sijakataa swala la kutokupendana, kupishana mitazamo, sera na hata maisha!! Hayo yapo lakini anapotokea mtu akatumia tofauti zenu kuwagomabisha zaidi kwa maslahi yake huyo ndiye mkorofi. Kwani hao Sunni na Shia wameziona tofauti zao miaka hii tu? Miaka ya nyuma mbona wasipambane na kuchinjana kama ilivyo sasa?
Huwa mara nyingi sipendi kujibizana kwenye mitandao sababu kwa sasa source kubwa ya habari ni mitandao na mitandao ina kila kitu!! Uwongo na ukweli, so ukiamua kuleta evidence hapa patachimbika na mimi vile vile vile lakini kikubwa ninapenda kudigest na kuchukua kile naona angalau kina ukweli kidogo!! Mfano, ukisoma magazeti ya UK na US kuhusu habari za Syria ni tofauti sana na utakavyosoma habari hiyo hiyo kwenye magazeti ya Urusi!
Hata habari za Ukrain, soma websites za UK na US then soma ya Urusi uone viroja! So kubishana kwenye mitandao sichukulii kama ushujaa sanaaa!!