Kwanini waafrika wanajibadilisha rangi?

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Kwa nini waafrika wanajibadilisha rangi?

Mitindo ingekuwa na maendeleo kiasi gani bila uwepo utumwa na ukoloni?

Katika mfululizo wa Barua kutoka kwa Waandishi wa habari wa Afrika, Mwandishi na Mtunzi wa Riwaya,Tricia Nwaubani anaangazia mada ya kung'arisha Ngozi.
Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita, nilijenga tabia ya kuwauliza waafrika wenzangu kutoka nchi tofauti tofauti wanafikiria bara letu lingekuwaje kama wafanya biashara ya utumwa na Wakoloni wasingeingia Afrika.

Baadhi wanaona kuwa jamii za kiafrika zingekuwa na maendeleo, ikienda sambamba na maendeleo ya dunia.
Wengine wanaona kuwa Afrika ilikuwa na maendeleo sawa na maendeleo ya dunia nzima, lakini utumwa na ukoloni viliingilia kati na kukwamisha maendeleo.
Wengine wanaamini kuwa sisi waafrika tungeuana kwa mapigano ya kikabila na migogoro, bara lingekuwa na makundi machache ya kikabila yaliyo mbali mbali.
Ninapenda kufikiria kuwa sisi waafrika tungeweza kujisimamia kwa mambo mengi.Tungegundua umeme ,tungetengeneza viyoyozi na majokofu, tungejiuliza ni vitu gani vinaonekana kwenye bahari, kisha tukkatuma wanaume kwa wanawake kufanya uchunguzi.

Weupe unapewa maana zaidi miongoni mwa jamii ya Watu weusi wengi

Ingeweza kuchukua miongo mingi, hata karne, lakini jamii za kiafrika zingeweza kupata hadhi ya kuwa moja ya bara la ulimwengu wa kwanza.
Pia nafikiri kuwa, kwa kiasi fulani ,mwafrika alipaswa kufikiria''Nywele zangu zimejinyonga nyonga na zimependeza.lakini swali ni je zingekuwaje kama zingenyooshwa.
''ingekuwaje kama nywele zangu zingekuwa za bluua au nyeusi kama za gold?''
Mwafrika wa namna hii angetengeneza dawa za nywele na rangi ya nywele, ingawa haonekani na nywele ndefu.
Kusingekuwa na kasumba ya kutaka kufanana na Watu weupe.


Wanawake wengi barani Afrika wanajichubua ili kuwa na mvuto zaidi

Waafrika wangeweza kuangalia uwezekano wa kubadili rangi za ngozi.

''baadhi yetu rangi zetu za ngozi ni nyeusi na nzuri,wengine ngozi ni angavu nao pia ni wazuri.je itakuwaje mwenye rangi nyeusi akataka awe mweupe na mweupe kuwa mweusi?'

'weusi ung'aao'

Wanawake wengi wa Nigeria ninaowafahamu wanaotumia vipodozi vya kung'arisha ngozi si kwamba ngozi zao za asili ni weusi.
Na kuna wanawake wenye ngozi nyeupe lakini wanataka kuongezea zaidi ya rangi waliyonayo.
Kumekuwa na kasumba kuwa na ngozi nyeupe kumeonekana kuwa kwa kipekee zaidi kwenye jamii ya watu wengi walio na ngozi nyeusi.
150121101522_vipodozi_afrika_512x288_bbc_nocredit.jpg
130102135546_south_africa_skin_bleaching_640x360_bbc_nocredit.jpg
150121101415_afrika_urembo_512x288_bbc_nocredit.jpg
 
Kwasababu washafundishwa tangu utotoni kuwa uafrika haufai. Mtu anapewa jina la kizungu kama Rose,lazima atataka kuwa kama mzungu

Anaabudu dini ya kizungu, anashinda siku nzima anawaona wazungu kwenye tv
 
akili zao ni za kujitawazia tu hawa mabinti, hivi ulitegemea kuona reasonable answer tofauti na hili alilolitoa?
Na kwa akili yako ndogo unadhani ningekua najichubua ningekupa jibu kama hilo? Acha kuchukulia kila kitu serious. Hata wanaojichubua wasingekujibu hivyo
 
Na kwa akili yako ndogo unadhani ningekua najichubua ningekupa jibu kama hilo? Acha kuchukulia kila kitu serious. Hata wanaojichubua wasingekujibu hivyo
Lakini mimi nilikujibu kulingana na comment yako, sikujua kama haukua au ulikua serious. Mimi niliichangia tu bila kufahamu kwamba ulikuwa una act umjinga ilihali ni mtu mwenye akili zake timamu. Niwie radhi
 
Back
Top Bottom