mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Unajua fika, na ndio ulio ukweli, kuwa uchu wa madaraka kwa viongozi wa kisiasa, hasa nchi za dunia ya tatu, siyo tu kwamba ni chanzo cha uvunjifu wa amani katika hizo nchi, pia ndio chimbuko la migogoro ndani ya vyama vya siasa na hata michezo. Migogoro hiyo hutiwa chumvi zaidi na matumizi mabaya ya mali za vyama.Unawezaje kupambana na adui dhaifu kama ulivyoainisha na kushindwa kummaliza kwa miaka >28 na bado hauchoki?Hapo dhaifu ni nani?
Hamwezi kuishinda imani waliyonayo Watanzania kwa CDM kirahisi.Ni kwa kuwa hatuwezi kuambiwa lakini Nina uhakika gharama ya kuiangamiza CDM ni kuwa sana=Ufisadi wa Mali ya CCM na Taifa.Nadhani sehemu kubwa ya mapato halali na haramu ya CCM yanaenda kwenye hiyo project ya muda Mrefu ya kuiua CDM.
Pathetic reasoning and decision on Democratic Process.
Kwa sababu kuu hizo, ni mtazamo finyu na hafifu kuendeleza fikra kwamba adui mkubwa wa CHADEMA yuko nje ya chama. Ni matatizo kiuongozi ndani ya vyama ya kutaka kuwa na madaraka makubwa ili kiongozi awe na nguvu ya maamuzi ya juu rasmali zake. Kwa Tanzania kuna mifano hai ikuhusu NCCR-Mageuzi, CUF na sasa CHADEMA inanyemelewa kumeguka na mzimu huohuo.
CCM, chama cha siasa kikongwe nchini pia kilifikia mahali kikaonesha dalili za kumeguka. Adui walikuwa ndani kwa ndani na hasa viongozi kugombea madaraka ili wajinufaishe na mali za chama. Matokeo ya uchunguzi wa mali za chama na kamati iliyoundwa na M/Kiti, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa sasa, ni ushahidi wa jinsi viongozi wa vyama vya siasa wanavyofisadi mali za chama.
Hivyo basi, kwa CHADEMA, tuhuma za matumizi mabaya ya fedha dhidi ya Mbowe, M/Kiti wa chama, zinaweza kuwa za msingi na chanzo cha chokochoko zinazojitokeza kwa sasa. Suluhisho la kukiokoa chama wakati nchi ikielekea Uchaguzi Mkuu, ni kwa watuhumiwa kuweka wazi mambo wanayotuhumiwa ili kujenga imani ndani na nje ya chama.
Viongozi wakuu wa CHADEMA, hasa wa Kamati Kuu, ambao wanatuhumiwa kuodhi madaraka na maamuzi, wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi Mkuu ujao si wa kichama bali wa kitaifa. Wapiga kura ni pamoja na wasio wanachama wa chama chochote. Katika mazingira ya viongozi wa CHADEMA kutuhumiana hakika wanakiweka chama kwenye mtihani wa kukubalika na jamii.
Mnaomtetea Mbowe na genge lake, kwa kuhamisha lawama, hamumtakii mema na ni kama kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.