Kwanini vyama vingi vinataka CHADEMA ife?

Kwanini vyama vingi vinataka CHADEMA ife?

Peoplesssssssssss!
Chadema inapendwa sana, tena bila sababu. Kwanza yale mavazi yao nikiyaona huwa nachanganyikiwa.
Nikisikiliza hoja zao bungeni, looh!
Chadema ipo mioyoni mwa watu. Haifi.
 
Umeandika mashudu matupu
Anayeiua Chadema ni Mbowe,
Huyu kiumbe mkabila na mfanyabiashara wa kisiasa anaonekana wazi amepewa au ameahidiwa mpunga mrefu sana ili kuhakikisha Tanzania haipati Chama chenye Demokrasia na kushika Dola.

Tukiacha ushabiki tukamtafakari Mbowe vizuri na wenyeviti wenzake tutapata jibu na ama kuwatimua kwa marungu na mawe toka kwenye Ofisi za vyama vya watanzania na kuweka katiba bora zinazojenga vyama kitaasisi sio vyama vya mtu binafsi.

Nimemsikiliza vizuri Kibajaji Bungeni nikagundua kuwa yule jamaa anaipenda sana Chadema na anaumia sana anavyoona jinsi Mbowe anavyoiua kwa manufaa yake.

Serikali nzima ya Awamu ya Tano iliingia ikiwa na imani ya kupata sapoti kubwa kutoka Chadema kuliko kutoka CCM kwani wengi walikua ni wale walikua wanachukizwa na ufisadi,uzembe, ubabaishaji,wizi,rushwa umangi meza na kila aina ya uhalifu uliokuwa unafanywa na watawala.

Cha ajabu Mbowe alibadili gia angani na kupinga kila kitu mpaka ushauri mzuri wa kujenga makao makuu ya Chadema Dodoma aliokuwa amepewa na Mh . Rais siku ya kuzindua Bunge . Hapo ndipo nilipoanza kumtoa Mbowe kwenye thamani kabisa. Nikamfutilia Mbali kabisa kwenye orodha ya wanasiasa wenye nia nzuri na nchi yetu alipochukua tena form na kugombea Uenyekiti kwa awamu ya nne.
Mbowe anazeeka huku Chama chake kikiwa kinakufa kwa kasi ya ajabu.
Sijui angeacha Demokrasia ikashamiri ndani ya Chadema angepata hasara gani !
Bora Mbowe angeachia mwingine Chama kisimfie mikononi mwake. Hakika Mbowe atafuta historia yake nzuri kwa uroho wa madaraka.

Wachawi wa vyama vya upinzani ni wenyeviti wao na sio CCM.
CCM ya sasa ni Chadema asilia kwa hiyo kama Mbowe angecheza karata yake vizuri angekijenga Chama chake vizuri sana na kumwachia mwingine kiti kidemokrasia kabisa.

Ukiua Demokrasia kama Mbowe inabidi utumie nguvu kubwa kulinda kiti chako.

ACT Wazalendo kitakua Chama kikuu cha upinzani mana kinaongozwa na mtu aliyekua na maono ya kuujenga upinzani , ubinafsi wa Mbowe akamfukuza.
Chama kitakachofuatia kwa kuwa na wabunge wengi kitakuwa ni NCCR kikifuatiwa na Chadema
 
Mashudu tupu
Mbowe ndie anataka chadema ife I'll asiwepo was kuhoji matumizi ya ruzuku na michango ya bilioni nane alizotafuna

Anajua kikifa Hakuna was kuhoji anaingia zake mitini kimya kimya kusitafuna

Tunashukuru Takukuru kumuwahi na kugundua ujanja wake

Mbowe anatamani chadema ife hata leo
 
Hakika
Ni mapandikizi ya ccm yaliyonunuliwa kwa bei poa.. Lakini CHADEMA is there to stay.. View attachment 1464000

Jr
FB_IMG_1589256244101.jpeg
 
Sitoacha kuwapigia kura chadema kamwe,pamoja na maswaibu yote wanayopitia,tena ya kukandamizwa ni chama kinachojielewa sana ukilinganisha na vyote hata Chama Tawala
 
Kwanini vyama vyingi vinataka chadema ife?
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kila chama kina haki ya kushiriki uchaguzi
Kila chama kina haki ya kusimamisha wagombea
Swali,ni je, kwanini vyama vyingi badala ya kutaka ccm iondoke madarakani vinataka chadema ndio ife?
Ukifanya utafiti usio rasmi utagundua cuf,nccr tlp na baadhi ya vyama viko tayari ccm iendelee kubaki madarani kuliko chadema kupata wabunge wengi au kushika dola,je vyama vyingine vya upinzani kutaka chadema ife lkn ccm ibaki madarakani viko sahihi?na kwanini unafikiri vinatamani chadema ife?
Hakuna chama kinataka CHADEMA kife ila, kwa mujibu wa viongozi wanaokihama, chama kimeonesha kina:
• uongozi dhaifu;
• viongozi wasaliti;
• viongozi waoga;
• viongozi wasiojitambua;
• ufisadi wa mali ya chama usiothibitiwa; na
• kikundi cha viongozi, wanachama na wafuasi wasio na adabu, wao lugha ya matusi imekuwa ndiyo sifa moja kuu na imefanywa pia moja ya itikadi ya chama.
 
Mbowe ndie anataka chadema ife I'll asiwepo was kuhoji matumizi ya ruzuku na michango ya bilioni nane alizotafuna

Anajua kikifa Hakuna was kuhoji anaingia zake mitini kimya kimya kusitafuna

Tunashukuru Takukuru kumuwahi na kugundua ujanja wake

Mbowe anatamani chadema ife hata leo
Huu ukweli unapigwa vita kwa nguvu zote.
Kuna Kisacoss Fulani kwenye Eneo Fulani kilikua kinaitwa Talanta. Kilikua kinawanachama wasio na elimu ya kutosha lakini kiliongozwa na wasomi na wajanja wajanja wa kuwashawishi wakulima na wafanyabiashara wadogo wadogo na hata wa kati kujiunga. Kikafanikiwa sana. Baadae viongozi wake na mhasibu wao walianza kujichukulia fedha na kuanzisha miradi yao binafsi na kujitajirisha huku wakiwaaminisha watu kuwa kuna wanachama hawajarudisha marejesho ya mikopo yao na pia watu hawatoi michango yao. Wakati huo wao wanazidi kuneemeka na wakawa wanawaziba midomo wale walikua wanahoji kuhusu mgao wa hisa zao na faida ya sacoss yao. Ulafi wa viongozi ndio ulioua ushirika wao .Mwishowe Saccos ikafa na sasa wana mgogoro mkubwa upo kwa mkuu wa Wilaya.
 
Anayeiua Chadema ni Mbowe,
Huyu kiumbe mkabila na mfanyabiashara wa kisiasa anaonekana wazi amepewa au ameahidiwa mpunga mrefu sana ili kuhakikisha Tanzania haipati Chama chenye Demokrasia na kushika Dola.

Tukiacha ushabiki tukamtafakari Mbowe vizuri na wenyeviti wenzake tutapata jibu na ama kuwatimua kwa marungu na mawe toka kwenye Ofisi za vyama vya watanzania na kuweka katiba bora zinazojenga vyama kitaasisi sio vyama vya mtu binafsi.

Nimemsikiliza vizuri Kibajaji Bungeni nikagundua kuwa yule jamaa anaipenda sana Chadema na anaumia sana anavyoona jinsi Mbowe anavyoiua kwa manufaa yake.

Serikali nzima ya Awamu ya Tano iliingia ikiwa na imani ya kupata sapoti kubwa kutoka Chadema kuliko kutoka CCM kwani wengi walikua ni wale walikua wanachukizwa na ufisadi,uzembe, ubabaishaji,wizi,rushwa umangi meza na kila aina ya uhalifu uliokuwa unafanywa na watawala.

Cha ajabu Mbowe alibadili gia angani na kupinga kila kitu mpaka ushauri mzuri wa kujenga makao makuu ya Chadema Dodoma aliokuwa amepewa na Mh . Rais siku ya kuzindua Bunge . Hapo ndipo nilipoanza kumtoa Mbowe kwenye thamani kabisa. Nikamfutilia Mbali kabisa kwenye orodha ya wanasiasa wenye nia nzuri na nchi yetu alipochukua tena form na kugombea Uenyekiti kwa awamu ya nne.
Mbowe anazeeka huku Chama chake kikiwa kinakufa kwa kasi ya ajabu.
Sijui angeacha Demokrasia ikashamiri ndani ya Chadema angepata hasara gani !
Bora Mbowe angeachia mwingine Chama kisimfie mikononi mwake. Hakika Mbowe atafuta historia yake nzuri kwa uroho wa madaraka.

Wachawi wa vyama vya upinzani ni wenyeviti wao na sio CCM.
CCM ya sasa ni Chadema asilia kwa hiyo kama Mbowe angecheza karata yake vizuri angekijenga Chama chake vizuri sana na kumwachia mwingine kiti kidemokrasia kabisa.

Ukiua Demokrasia kama Mbowe inabidi utumie nguvu kubwa kulinda kiti chako.

ACT Wazalendo kitakua Chama kikuu cha upinzani mana kinaongozwa na mtu aliyekua na maono ya kuujenga upinzani , ubinafsi wa Mbowe akamfukuza.
Chama kitakachofuatia kwa kuwa na wabunge wengi kitakuwa ni NCCR kikifuatiwa na Chadema
Kwa nyogeza, kitendo cha kushindwa kuwabakiza kwenye chama viongozi wenye ushawishi na maono ni kosa kubwa la kisiasa. Mifano
√ EL Lowassa, kwa kiasi kukibwa alikiwezesha chama kupata Wabunge wengi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 na mara kadhaa akiwaasa kuacha siasa za uharakati lakini uongozi wa Mbowe uliweka pamba masikioni;
√ Slaa, Katibu Wakuu alikuwa mahiri katika kujenga hoja mbadala zenye nguvu ya ushawishi kwa WaTz wa kila rika, jinsi, elimu na hata kipato;.
√Wako wapi wabobezi wa kuchambua siasa km Prof Baregu na Prof Safari?

CHADEMA ya sasa ina kundi la viongozi vuvuzela mabingwa wa kuongea kwa matusi, kundadia hoja na kushadadia matukio.
 
Kwanini vyama vyingi vinataka chadema ife?
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kila chama kina haki ya kushiriki uchaguzi
Kila chama kina haki ya kusimamisha wagombea
Swali,ni je, kwanini vyama vyingi badala ya kutaka ccm iondoke madarakani vinataka chadema ndio ife?
Ukifanya utafiti usio rasmi utagundua cuf,nccr tlp na baadhi ya vyama viko tayari ccm iendelee kubaki madarani kuliko chadema kupata wabunge wengi au kushika dola,je vyama vyingine vya upinzani kutaka chadema ife lkn ccm ibaki madarakani viko sahihi?na kwanini unafikiri vinatamani chadema ife?
vibaraka vya CCM. kama unavyoona wabunge wananunuliwa vipande vya fedha, hivi vyama uchwara vinatamani vipate upendeleo wa kupewa ubunge wa mezani kwa mbinu za uchaguzi wa serikali za mitaaa! Mbatia anatamani apate marupurupu y KUB...... hivyo mtu anajitoa ufahamu kabisa!
 
Paka anampa Panya ushauri.
Hivi ushauri wa kujenga Makao makuu ya Chadema Dodoma hayakua ya maana kweli?
Tuache siasa za chuki na kutothaminiana.
Ndio maana Mbowe hathamini michango ya hali na Mali ya wabunge wenzake. Anaongelea yeye tu kuwa nimefungwa,nimetoa Mali zangu,nimefilisiwa na kila kitu kwa kujionea huruma yeye tu na kuona kuwa fidia yake ni kukalia kiti. Anasahau wenzake wamumizwa na wamepata nafasi zao kwa dhiki kubwa tofauti na yeye aliyerithishwa utajiri na hata Chama.
Alipaswa kuwasikiliza na kuwapa wenzake nafasi pia baada ya yeye kupata nafasi na muda wake wa miaka kumi kuisha. Huo ndio uungwana .
Mandela alifungwa miaka 27 lakini alipopata urais aliamua kungatuka baada ya awamu moja tuu.
Alijua wapo wengine wengi waliopambana wakati yeye akiwa Gerezani.

Chadema ingejenga Ofisi Dodoma kwa michango ya watu na sio kwa Hela zake toka mfukoni wala Ruzuku. Mbona watu walichanga mil. Mamilioni kuwatoa gerezani ndani ya siku tatu.

Chama chenye wanachama wengi kinashindwa vipi kuwahamasisha wanachama wake kujenga Ofisi zao kila mkoa.
Hivi makanisa na misikiti inajengwa ya nini kama haina umuhimu katika kujenga itikadi na imani?

Mbona mnakua na siasa nyepesi sana halafu mnataka kuingia Ikulu kufanya mambo mazito.
Mbowe hafai tena kuendelea kukijenga chama .
Ofisi ni center nzuri ya kujenga itikadi za vyama. Kila taasisi inapokua na Ofisi inakua na uhakika zaidi wa kufanya mambo yake.

Kuna wakati utafikia wananchi wataogopa hata kuipangishia Chadema nyumba za ofisi. Je , watafanyia wapi mambo yao?
Tuache ubishi na dharau zisizo na tija kwa kufuata mkumbo wa Mbowe.
Mbowe anatumika vibaya na makundi ndani ya CCM kuhakikisha kuwa 2025 chadema inakua taabani ili makundi hayo yapate nafasi ya kurudi tena madarakani ndani ya CCM. Mbowe ni mfanyabiashara hafanyi jambo lolote kwa hasara.
Najua ninachokisema.! Ndio maana viongozi wenzake ndio wanaokimbia mana wanajua nini kinaendelea. Sio muda mrefu Mbowe atakosa mpaka Katibu Mkuu mana yeye sio mfanyabiashara ni mwanasiasa mwenye kutamani kuona serikali mbadala inaingia madarakani wakati Mwenyekiti wake anavizia maslahi yake kiuchumi.
Subirini mtaona !
Mnyika anapotezewa kipaji Chake kwa manufaa ya Mbowe. Tundu Lisu anapotezewa kipaji chake kwa manufaa ya Mbowe.
Hakuna nia ya kushika Dola zaidi ya kushika uenyekiti. Dola linahitaji watu wengi wenye uwezo na Mbowe ndio anaowafukuza kutoka kwenye chama Chake.
 
Kwanini vyama vyingi vinataka chadema ife?
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kila chama kina haki ya kushiriki uchaguzi
Kila chama kina haki ya kusimamisha wagombea
Swali,ni je, kwanini vyama vyingi badala ya kutaka ccm iondoke madarakani vinataka chadema ndio ife?
Ukifanya utafiti usio rasmi utagundua cuf,nccr tlp na baadhi ya vyama viko tayari ccm iendelee kubaki madarani kuliko chadema kupata wabunge wengi au kushika dola,je vyama vyingine vya upinzani kutaka chadema ife lkn ccm ibaki madarakani viko sahihi?na kwanini unafikiri vinatamani chadema ife?
Hivyo ulivyovitaja kwa umoja wao ni CCM bila kufahamu/kimkakati zaidi.Huwezi kuwa na lengo LA kuingia madarakani halafu badala ya kupambana na aliyeyashikilia kwa kudhoofisha washinda wenzako.
CCM wanawafadhili hao ili ijinufaishe.Wanafahamu CDM ikidhoofu/kufa kama wanavyopenda kusema wao wanapata ushindi.Fikiria ya TLP kumpitisha mgombea wa CCM kama mgombea wao hats kabla ya wakati, msajili kimya na CCM wanashangilia.Sina uhakika wanawawakilisha Watanzania gani hawa.Katiba yao inaruhusu mambo hayo?
Hao siyo wapinzani Bali instruments za CCM.
 
Kosa walilofanya Chadema 2015 liliwapa faida ya muda mfupi ila litawapa hasara ya muda mrefu sana.
 
Jibu simple: Hata CUF ilipokua chama kikuu cha upinzani CHADEMA walitaka CUF ife au muulizaji umezaliwa 2015.
 
Hakuna chama kinataka CHADEMA kife ila, kwa mujibu wa viongozi wanaokihama, chama kimeonesha kina:
• uongozi dhaifu;
• viongozi wasaliti;
• viongozi waoga;
• viongozi wasiojitambua;
• ufisadi wa mali ya chama usiothibitiwa; na
• kikundi cha viongozi, wanachama na wafuasi wasio na adabu, wao lugha ya matusi imekuwa ndiyo sifa moja kuu na imefanywa pia moja ya itikadi ya chama.
Unawezaje kupambana na adui dhaifu kama ulivyoainisha na kushindwa kummaliza kwa miaka >28 na bado hauchoki?Hapo dhaifu ni nani?
Hamwezi kuishinda imani waliyonayo Watanzania kwa CHADEMA kirahisi.

Ni kwa kuwa hatuwezi kuambiwa lakini Nina uhakika gharama ya kuiangamiza CDM ni kubwa sana=Ufisadi wa Mali ya CCM na Taifa.Nadhani sehemu kubwa ya mapato halali na haramu ya CCM yanaenda kwenye hiyo project ya muda Mrefu ya kuiua CDM.
Pathetic reasoning and decision on Democratic Process.
 
Back
Top Bottom