SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,896
Wakuu,
Kuna mambo ambayo nimekuwa napambana nayo kwa muda mrefu sana katika maisha yangu. Nimejaribu njia nyingi, hasa za maombi hadi chumvi. Wakati mwingine naona kuna unafuu unakaribia kuja halafu ghafla narudi kule kule. Niliwahi kuleta uzi humu kuelezea hali yangu.
Kwenye masuala ya uchumi, nimefungwa vibaya sana hauwezi kuamini nikikwambia mambo niliyopitia. Unaweza kudhani mimi ni mzembe, mvivu au sina vipaji au akili ila ungenijua uwezo wangu pamoja na uchakarikaji wangu, utashangaa sana kwa nini sina mafanikio.
Kuna hili ambalo limeanza kujitokeza hivi karibuni. Kuna vifaa fulani vidogo ambavyo nilinunua kitambo kwa ajili ya shughuli ninazofanya. Nilikuwa nimepanga kuanza kuvitumia kuanzia mwezi uliopita. Sasa nimekuwa navitafuta katika chumba ambacho ni mimi pekee ninaingia, havionekani. Hii iliwahi kunitokea kwa kifaa kingine, nilikuwa nakihitaji sikukiona kabisa kila sehemu hadi mahitaji yalipokwisha ndiyo nikaja kukiona pale pale nilipokuwa nakitafuta.
Sasa nimetoa karibu kila kitu katika chumba nimechambua kila sehemu hivi vitu havionekani kabisa. Na naamini hivi vifaa vingeniletea mabadiliko makubwa sana katika maisha yangu.
Nimekuwa najizuia kuamini kwamba kuna watu (ndugu, rafiki au adui) wamenichezea kwenye mambo ya kiroho ila kuna mambo yanayonitokeaga nikiangalia vizuri naona kabisa kuna jambo haliko sawa nyuma ya pazia.
Kuna matukio mengi sana, na mengi yanafanana nikisema niyaorodheshe hapa sitamaliza. Kiufupi, namshukuru Mungu kwa uhai na afya njema na naamini nitaweza kubadilisha hali yangu ila ni miaka sasa sina kipato pamoja na juhudi na maarifa yote niliyonayo.
Najiuliza, mpaka lini haya yataendelea? Ni lazima nibadili hii hali aisee!