Kwanini vitambi hakuna vijijini wakati wamama na wanaume hula viporo?

Daah kijijini mafuta ya kutengeneza kitambi yatakaa wapi muda wote mara umepanda mlima mara ukarudishe mifugo haujatulia mtu kaleta mbegu za mahindi uangalie mara ukatoe kuni kwenye bati harafu hicho kitambi kitakaa wapi...mjini mtu anapoenda anapaona pale ila anapanda dala dala kutembea wanafanya mazoezi Mjini wakati kijijini kutembea ni sehemu ya maisha..
 
Maisha huko mtu anaamka anatoka saa 12 asubuhi anaenda kwenye mishe zake shambani tena anatembea kilomita kadhaa, anarudi saa 12 jioni
Kwa style hiyo kitambi kitapatikanaje

Ova
 
Vijiji vingi vina ufukara wa hali ya juu.. vyakula wanavyokula ni duni na hata kumudu kula vyakula vyenye mafuta mafuta ni tatizo. Ukijumlisha na mihangaiko mingine basi automatically no kitambi
 
Maisha huko mtu anaamka anatoka saa 12 asubuhi anaenda kwenye mishe zake shambani tena anatembea kilomita kadhaa, anarudi saa 12 jioni
Kwa style hiyo kitambi kitapatikanaje

Ova

Ulishawahi kuona mtu anaezama chini kupandisha mchanga au kuchimba, au anaeenda kulima anakua na kitambi? Halafu kazi ndio mwisho wa maneno lazima mwili ujibalance
 
Huku mjini wakishabofya bofya kompyuta sjui kushika mafaili
Anakuambia nmechoka kwerikweri


Ova

Acha kabisa, mtu mwendo wa ubungo mataa hadi manzese anasema nimechoka wakati bush mtu anatembea kutoka buguruni labda kuvuka kibaha ndio shamba lilipo na ni nenda rudi na hachoki na kazi anafanya kitambi kitatoka wapi
 
Uvivu unafanya tunenepe

Kwa mfano hauna kazi ngumu, tuwe wakweli milo miwili inatosha au mlo mmoja wa maana hasa asubuhi, halafu usiku chakula chepesi tu huna haja ya milo mitatu ambayo inakwenda kuleta matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula yaani unakuta unagonga milo mitatu na choo haupati na ukipata ni kwa shida sana, mwisho wa siku magonjwa yanakuandama mara presha, mara sukari, na ukumbuke asilimia kubwa ya magonjwa ya binadamu huanzia tumboni au mfumo wa chakula ukiacha magonjwa kama ya zinaa na kansa,
 
Vijijini hakuna wanawake wenye vitambi wala wanaume pamoja na kwamba wanakula viporo na lishe isiyo bora kama mjini.

Je, watu wa town nao waishi kwa viporo na vyakula kama vijijini?
Mnawaza vitambi tu na kulakula. Fanyeni kazi nyie.
 
Back
Top Bottom