Kwanini vijana wasomi wanayumba sana mtaani?

Kwanini vijana wasomi wanayumba sana mtaani?

Ndo inavyokuww.. Na usikute kazi zenyewe ndo zile za kamlete, alafu mtu anaona ambao hawajapata ni wajinga!
Biashara sa hiv ni ngumu pesa mtaani hakuna kabisa watu hawana mitaji huko kujiajiri wanajiajiri vip? Au wewe unadhani kujiajiri ni rahisi?
Shukuru mungu upo kazini unakula mema ya nchi you are no more than hao jobless walioko kitaa they are just unfortunate kushindwa kupata kazi.
Tatizo la wabongo mtu akitoboa kidogo basi unaona wenzio wote mamburula hawajui kitu ipo siku io ajira yako itakoma utakuja kitaa uone shoo yake.
 
Mara nyingi wanao wadhihaki wasomi n wale ambao hawakubahatika kusoma had juu.Mtu anamiliki kibodaboda anajiona dunia yeye ndoo tajiri mtu anamilik kinyumba cha slope anawaponda graduate achani UK---MA
 
Kusoma mpaka chuo halafu kufungua genge la nyanya ni ujinga.bora hata chuo usingefika ungeishia lasaba.

Kwangu Mimi hii ' post ' yako naiona ina Thamani Kubwa na Umeandika vyema kabisa japo najua wapo baadhi Wavivu wa Uelewa watakupinga, watakubishia na hata kukukebehi pia. Nimekuelewa mno Kiongozi.
 
Hii Topic ni mzito na inafikirisha Hata wakipewa kazi ni incompetent Kwani mujibu WA utafiti E. A vijana was Tanzania Ndio wanaongoza Kwani kutoajirika. TUJITATHMINI.
 
Kwangu Mimi hii ' post ' yako naiona ina Thamani Kubwa na Umeandika vyema kabisa japo najua wapo baadhi Wavivu wa Uelewa watakupinga, watakubishia na hata kukukebehi pia. Nimekuelewa mno Kiongozi.
Naomba mdahalo na wewe, kwako Graduate afanye nini unataka???
 
Hebu tuache kuwaonea hawa vijana ni kweli wana matatizo lakini jamii imezidi wahukumu sana. Ni jamii hii hii ambayo iliwatuma kusoma na kuwakazania wasome kwa juhudi wakajitahidi wakatimiza jamii ilichowataka lakini jamii ile ile inaanza kumuona hana thamani.
Sijui kwa sasa hivi ila kijana mpaka afike college amejiexclude na jamii kwa muda mrefu sana, fikiria miaka saba ya primary, sita ya secondary na mitatu ya college system imekutenga na jamii kwa miaka 17. Fikiria ili ufaulu vizuri si wakati wa likizo au wa masomo Mchikichini/msuli mkali ndio ulikua mkombozi wako kwenda mbele la sivyo ungeishia njiani. Ili kufikia malengo yako ulipaswa kutumia muda mwingi kusoma kuliko kuishi na jamii yako wewe ni msuli na kula. Umejitahidi umefanya yote hayo jamii ile ile ilyokuhusudu wakati unakomaa sasa hivi wanakuhumu.

Naamini vijana watabadilika lakini sio kwa vile tunavyotaka sisi ni process itakayochukua muda. Huwezi mfananisha la saba drop out ana experience ya mtaa kuliko yeye kama miaka kumi. The education has failed them they need to wake up ila sio kufanyiwa dhihaka.
umeongea vizuri sana, kuna watu wanawahukumu hawa vijana wakati wao wenyewe msingi wa maisha yao baada ya kuhitimu ni kuajiriwa na sio kujiajiri. mimi kibinafsi nilifanya kazi ya kijasiriamari lakini ilikuwa ya ngazi ya chini japo ilinisaidia kwa kiwango chakutosha lakini bado ilikuwa changamoto kubwa kutoka kwa jamii inayokuzunguka. tusiwalaumu wala kuwakebehi pale tunapoweza kuwasadidia tuwasidiea mawazo na vingine
 
Utamkuta mtu mwaka wa saba Sasa anakaa kwa shemeji yake kaz kupiga story tu Nina degree Mimi usinione hivi.
Ina Mana vijana degree zenu huwa ni kifungo kinachokuzuia kufanya shughuli zingine za kuingiza pesa wakati ukisubir hiyo ajira, kumbuka sku hz wasomi wengi tofauti na zaman, zaman ukimaliza form four tu unaajiriwa moja kwa moja siku hz na degree zetu ndio tumejaa kitaa.
Vijana tubadili fikra Kuna maisha bila ya degree
vijana tunalaumiwa sana lakini jamii inayotunzunguka ndio inatufanya tusithubutu maana kuna kazi ukianza kufanya jamii inaanza kukusimanga kuwa pamoja na digrii au elimu yako unafanya kitu ambacho mtu wa darasa la saba anatakiwa afanye.
Yaani jamii inayotuzunguka wanaamini ukiwa na elimu fulani basi ufanye jambo ambalo litakutanabaisha kama msomi kweli kweli. Na ndio maana watu wanashauriwa unapotaka kufanya jambo nenda sehemu ambayo watu hawakufahamu ndipo utafanikiwa.
Kwa mfano mimi baada ya kumaliza chuo nililima maharage nikavuna baadae nikauza nakufanikiwa kununua boda boda used nikaanza kuwa boda boda. ndugu,marafiki na jamii ilinisema sana kuwa pamoja na kusoma ila nimerudi kuwa boda boda sikumsikiliza mtu nilipiga miezi sita kazi ya boda boda nikaiuza nkalima tena nikapata kama ml 4 hivi nikanunua bajaj used napo hawakuishia kusema wakaendelea kusema ila mimi nakiri wazi kwamba kwa hii kazi yangu ya bajaj sifikirii tena hata ajira maana kama kwa siku nalala na kuanzia elf 40+ niwaze tena ajira ya kazi gani?
Hivyo msituhukumu sana ila inatakiwa jamii ndio ielimishwe kuhusiana na huyu kijana msomi maana inatuathiri kisaikolojia.
 
Kuna lingine lolote ulilolibakisha labda Wewe Moron?

Cc: gwankaja
Wewe ni moja ya wale mulipo hitimu mulipewa pesa ya kilakitu na mzazi mpaka nauri za kwenda kwenye interview ndio maana unakuja kusapoti utumbo then unajinasibu una IQ kumbe kiazi tu mmoja.
 
umeongea vizuri sana, kuna watu wanawahukumu hawa vijana wakati wao wenyewe msingi wa maisha yao baada ya kuhitimu ni kuajiriwa na sio kujiajiri. mimi kibinafsi nilifanya kazi ya kijasiriamari lakini ilikuwa ya ngazi ya chini japo ilinisaidia kwa kiwango chakutosha lakini bado ilikuwa changamoto kubwa kutoka kwa jamii inayokuzunguka. tusiwalaumu wala kuwakebehi pale tunapoweza kuwasadidia tuwasidiea mawazo na vingine
vijana tunalaumiwa sana lakini jamii inayotunzunguka ndio inatufanya tusithubutu maana kuna kazi ukianza kufanya jamii inaanza kukusimanga kuwa pamoja na digrii au elimu yako unafanya kitu ambacho mtu wa darasa la saba anatakiwa afanye.
Yaani jamii inayotuzunguka wanaamini ukiwa na elimu fulani basi ufanye jambo ambalo litakutanabaisha kama msomi kweli kweli. Na ndio maana watu wanashauriwa unapotaka kufanya jambo nenda sehemu ambayo watu hawakufahamu ndipo utafanikiwa.
Kwa mfano mimi baada ya kumaliza chuo nililima maharage nikavuna baadae nikauza nakufanikiwa kununua boda boda used nikaanza kuwa boda boda. ndugu,marafiki na jamii ilinisema sana kuwa pamoja na kusoma ila nimerudi kuwa boda boda sikumsikiliza mtu nilipiga miezi sita kazi ya boda boda nikaiuza nkalima tena nikapata kama ml 4 hivi nikanunua bajaj used napo hawakuishia kusema wakaendelea kusema ila mimi nakiri wazi kwamba kwa hii kazi yangu ya bajaj sifikirii tena hata ajira maana kama kwa siku nalala na kuanzia elf 40+ niwaze tena ajira ya kazi gani?
Hivyo msituhukumu sana ila inatakiwa jamii ndio ielimishwe kuhusiana na huyu kijana msomi maana inatuathiri kisaikolojia.
That's the spirit kaka piga kazi hao wanaoo ongeaga ni wivu tu, you have what they have through what they do, ila hawana kile ambacho unacho, na hio inawatia hasira sana mwishowe wanaanza kebehi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom