Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Haki ya kupata ilipatikana pale ambapo muajiri hakukupa taarifa ya kuongeza prob. kabla ya miezi mitatu ya mwisho kwa scenario hii mwezi October 2023 alipaswa akujulishe kama anania ya kuongeza muda ila kwakuwa alikaa kimya basi we subiria barua.
Sawa mkuu
 
Nina shida Ndugu zangu,Kwenye tangazo la kuita watu Kwenye usailii inaonyeshaa Siku ya usailii ni tarehe 16 na Kwenye ajira portal pia ilikuwa inasema hivyo but saivii nimeingia kuangalia Kwenye ajira portal tarehe imebadilika wameandika tarehe 15 ila wao hawajasema kama Kuna mabadiliko yeyote ko hapo tarehe ya ukwelii ni ipii??
 
Nina shida Ndugu zangu,Kwenye tangazo la kuita watu Kwenye usailii inaonyeshaa Siku ya usailii ni tarehe 16 na Kwenye ajira portal pia ilikuwa inasema hivyo but saivii nimeingia kuangalia Kwenye ajira portal tarehe imebadilika wameandika tarehe 15 ila wao hawajasema kama Kuna mabadiliko yeyote ko hapo tarehe ya ukwelii ni ipii??
wanasemaga pdf ndio inakuwa na ratiba ya ukweli ila kama kuna mabadiliko wataweka tangazo kwenye web yao uwe unapitia pale kwenye matangazo
 
Leo katika historia (9Th January) ni siku ambayo IT alimwaga moto pale penye section ya chini ya vimulimuli, moto ukiwa umepamba majina mengi likiwemo langu, ni siku muhimu ya kuikumbuka.

Wito: Usikate tamaa, usiache kwenda kujaribu hadi kieleweke.
Kwangu Mm November nadhani itakuwa siku ya kukumbukwa sana baada ya kubadilishiwa Masharti ya Ajira kutoka Mkataba kwenda kudumu.

Hakika tumekumbukwa baada ya kitambo kirefu sana! Sasa wacha tulinde maliasili zetu kwa uadilifu mkubwa sana..

Tusikate Tamaa..
 
Wakuu naona wengi wenu humu mnapotoshana sana kuhusu kupata Ajira na uhusiano na Mungu

Ajira sio Mambo ya kiroho, ni mambo ya Matendo, naona mnaanza kupeana Hope ambazo haziwezi kuwasaidia katika hili

Kuna zaidi ya 70% ya wanaopata Ajira utumishi hawajawai kwenda kwenye mkesha,hawajawai Kufunga mfungo mtukukufu,na wala hawajawai kuwa swala 5 na wala hawajui mafuta ya mwamposa yanafananaje

Mtu atapata kazi alafu atakwambia ni Mungu tu kusema ukweli me nilifanya vibaya ila niliamua kumrudia Mungu,niliamua kumlilia Mungu,niliamua kusema na Mungu

Come on brothers and sisters, hii mitihani ya Utumishi sio rahisi kama tunavofikiria na wala sio migumu kama tunavyoichukulia, ukitaka kujua mitihani ni migumu angalia marks za Written, kuna watu wanapata hadi 1 au 9 na alijiandaa huyo usidhani yeye kazi alikuwa haitaki

Kupata Ajira ni swala la Performance, Ukipata kazi jipige kifuani kwa sababu ulipafomu kuliko wengine, hizi mark's za oral ni Siri ila ukweli ni kwamba ukitaka kujua reality we angalia mark's za kwenye Written basi utajua kuwa ata kwenye Oral kuna watu wanafeli pia tena sana tu

Unaweza kujihisi wewe hukufanya vizuri ila uhalisia ni kwamba kuna aliefanya vibaya zaidi kuliko wewe, hizo marks zako 40 ndio zimekupa kazi na kumnyima aliepata 20 kushuka chini

Mara ya pili hii nasisitiza wekeza katika kufika Oral, kwenye Written tumia mbinu zozote ambazo haziwezi kukuharibia ili ufike Oral, weka kijiji,igilizia nk ili Tu ufike oral, kwenye oral kuna watu wengi sana hujitoa wenyewe kwenye mashindano kwa sababu mbali mbali

Ukikaa na panelists wanaosimamia oral wakakupa tathmini ya watahiniwa unaweza kucheka na kushangaa inakuaje mtu ana bachelor ya kitu Fulani na hawezi kujielezea, kuna muda hadi wao wanafanya adjustment tu ili waweze kupata watu wanaowataka

Kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral ata sauti waga hazitoki ila hawezi kuja kukwambia,kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral wanaishia tu kusema Dahh/Mungu wangu hakuna point wanakumbuka ila hatokwambia, kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral waga wanakumbuka point 1 Tu kila swali ila hatokwambia, kuna kundi kubwa la watu kwenye oral waga wanapanick na kuanza kulia Tu hadi dakika zake zinaisha ila hawatokwambia

Ndomana ukichunguza kwenye Oral kuna ambao waga wanakaa sana na kuna ambao waga wanakaa kidogo Tu unashangaa katoka, kiufupi ni kwamba wanafunzi wa kitanzania kwenye Oral tuko shallow sana, zaidi ya sana kwahiyo jitajihidi sana kujitofautisha na wengine ili wewe uwe katika kundi la wenye unafuu

Kwahiyo kwenye kundi la watu wa namna hiyo ukitokea wewe ambae utaweza angalau kujibu points 2 kwenye kila swali basi unapata kazi yako kiroho Safi bila shida yoyote maana wewe ulikuwa ni mwenye nafuu kuliko wengine, utumishi wakiamua kufata taratibu zote basi watarudia sana kutangaza kazi

Mungu hawezi kubadili 25% ikawa 60% Mungu hawezi kubadili point ya Uongo ikawa ya Kweli, Mungu hawezi kubadili kingereza chako cha hovyo kikawa kizuri katika chumba cha mtihani, mtataka kumpa lawama za bure tu Mungu wenu

Kwakuwa watu watakaopanick kwenye oral lazima wawepo tu hiyo ni pie, basi wewe tumia udhaifu huo kujinoa vile utaona inafaa ili usije kuwa katika kundi la wanaopanick hovyo, jua ni namna gani utaweza kupunguza pressure,jua ni namna gani utaweza kuwa relaxed during interview, ikiwezekana jifunze body posture and body language

Nakupeni Siri tu ambayo itawasaidieni, Asilimia 60% ya wanaopata kazi utumishi sio kwa sababu walifikisha cut off points, lahasha kwa sababu wao walikuwa na unafuu sana kuliko wengine, tuliopata kazi kupitia utumishi tunalijua hili, kuna muda hadi unaona Huruma kwani aliekusaidia kwenye written hadi ukaingia kwenye oral yeye anakosa kazi naww unapata na unajua yeye ni Bora mara 100 zaidi yako
Sema yote kufurahisha genge lakini kwa hile nyomi bila Mungu kusimama upande wako hutoboi
 
Oral niliifanya tu vizuri,na mpaka sasa status inasoma selected for oral interview both web na app, wasiwasi wangu ni kuwa isije ikawa kwa vile nimepata hii ya contract wakaninyima zile za permanent
Haina uhusiano ukipata wanakuita na ile inakua imeishia pale unawapa taarifa wanamsogeza mwingine!
 
Back
Top Bottom