Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mkuu haya yote yataisha ni suala la Muda Tu mkuu, Ipo siku tutatoka kwenye huu ujobless, uvumilivu unahitajika kwa umakini mkubwa sana. Nyakati ngumu hazidumu ni mapito Tu yataisha haya mkuu
Kabisa mkuu yaan mpk sasa maumivu ninayo nayakumbuk maneno yake dahh jmn binaadam lazim tusaidiane hata km upo ktk cheo ni jambo la mda tu hujui Nan atakaekuj kukufaa kesho yak inawezekan huyo jamaa yko uliemsaidia akadharau lkn yule wa mbal akasaidia
 
Wakuu na vijana wenzangu wasaka asali, Kijana mwenzenu nilichoka private sector na kuhamasishwa na thread hii ya JF kutafuta ajira serikalini.

Kwa mara ya kwanza application yangu ikafanikiwa na kuitwa kwenye usaili pale Udom (written), licha ya nyomi na baridi ya kufa mtu Mungu akanisaidia kuitwa na oral pale Rose migiro.

Swali langu, Acc yangu kwenye Web na App vinasoma SELECTED for Oral.. ila nataka kufahamu kama vina uhusiano wowote na oral niliyopiga?

Mwisho nawatakia heri na baraka wasaka asali wote.. Mungu ni mwema tuendelee kusubiri maana ni Mwaminifu na humpa kila amwombaye. Amen.
Mambo ya Status hata kama yana maana yake, binafsi nakushauri uendelee na mishe zako wala usihangaike nazo kabisa.

Baki tu kufuatilia PDF ya placement kuanzia miezi 3 mbele tangu tarehe uliyofanya oral.
 
Hongera sana je ulifanya taasisi gani? uhusiano upo kwa tafsiri isiyo rasmi umefaulu usaili yaani upo katika kundi la waliopata juu ya 50 oral, kwahiyo itategemea taasisi uliyofanyia usaili inataka watu wangapi na wewe kati ya hao mliofanya oral na kupata 50+ wewe ni wangapi, kama taasisi wakiita watu kazini na usipoona jina lako ujue walioitwa walikuzidi maksi hivyo utabaki database kwa muda wa miezi 12 kusubiri bahati yako .

Shukrani Mkuu, nilifanya oral za MDA’s. Ngoja tuendelee kusubiri.
 
Back
Top Bottom