Mamlaka ya ajira iliyotangaza nafasi za ajira kada za afya ni sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali ya mtaa/LGA. Wizara ya afya kama mamlaka ya ajira haikutangaza nafasi za ajira!
Katibu wa Sekretarieti yaAjira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti zaMikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwaWatanzania wenyesifa na uwezo wa kujaza nafasi 9483 kama ilivyoainishwa katikatangazo hili.
NINAVYOFIKIRI: Baada ya usajili, na wizara ya afya ikiwa imeshapata kibali cha kuajiri iliamua kuchukua watu kutoka database! Waliokuwa wamewekwa database baada ya usajili wakajikuta wameokota dodo kwenye mwarobaini!! Wizara ikatoa placement kutoka database na waliokuwa wamefaulu zaidi wakiwa wanasubiria mamlaka zao za ajira zitoe placement na wengine kudhani hawakufaulu!! Kipindi hiki ndo LGA/halmashauri zimepamba moto kutoa placement!! Kwa maneno mengine watu kutoka database wamepangwa MDA/wizara na taasisi zake kama muhimbili, NIMR, nk wakati waliofaulu zaidi wameishia LGA!!