HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mi nadhani pdf la wale ma CDOs nafasi 800
Hizo nafasi 800 sidhani kama watazitoa kwa siku moja!! We fikiria nafasi 100 za fisheries Officers zimeanza kutoka mwezi wa nne hadi Septemba bado zinatoka mdogo mdogo!! Ila nadhani zinakaribia kuishia!!
 
Hawa jamaa hiki kimya sio cha bure nahisi kuna kitu kinaendlea pale psrs
Hizo ni hisia zako Mzee baba kazi lazima ziendelee watu hawawez kukufikiria wewe
Kama unakazi zako we endelea kufanya ukisubir pdf kama itatoka mwaka huu

Watu hawaajiriwi ovyo ovyo lazima kuwepo na fungu la fedha za kuwapa
 
Mkuu unahisi mtu akiwa Mwalimu utasema anafanya kazi TAMISEMI au mtu akiwa anafanya kazi TRA utasema anafanya kazi wizara ya fedha??
Mi hapo nimezungumzia muundo wa wizara yetu ya mifugo na uvuvi tu,so hizo wizara nyingine na Mambo Yao hata sijui chochote mkuu
 
Hizo ni hisia zako Mzee baba kazi lazima ziendelee watu hawawez kukufikiria wewe
Kama unakazi zako we endelea kufanya ukisubir pdf kama itatoka mwaka huu

Watu hawaajiriwi ovyo ovyo lazima kuwepo na fungu la fedha za kuwapa
Kwan kuna sehemu nimesema wasimamishe kz au wanifikirie mimi kwani hilo pdf likitoka linakua na jina langu peke yang mzee mbona unakrupuka kujbu comment bila kuelewa inakusudia nini? Acha roho mbaya mzee
 
Hizo ni hisia zako Mzee baba kazi lazima ziendelee watu hawawez kukufikiria wewe
Kama unakazi zako we endelea kufanya ukisubir pdf kama itatoka mwaka huu

Watu hawaajiriwi ovyo ovyo lazima kuwepo na fungu la fedha za kuwapa
Bila shaka utakua unasumbuliwa na roho mbaya mkuu maisha hayaendi hvyo kama ww umepata its ok kila mtu ana fungu lake acha kuwakatisha watu tamaa
 
Mambo magumu
Screenshot_20230912-084537.jpg
 
Haya yakizingatiwa angalau yatasaidia kuboresa mazoezi ya usaili yanayoendeshwa na Utumishi nchini:

1. Katika upande wa mwombaji Waboreshe utoaji wa taarifa kama kuitwa, matokeo, ratiba na mabadiliko yoyote kupitia sms kwa sababu taarifa wanazotoa kwenye website na mifumo inaweza kukwamishwa na mtu kutokuwa na intaneti. Pia kuwe na notifications kwe mfumo ua ajira, notifications zinaonesha kila kinachoendelea.

2. Mfumo uweze kuonesha ajira zinazosubiriwa, zilizopita, n.k. katika majedwali tofauti. Hii itasaidia mwombaji kufuatilia kwa umakini bila kukosea kama ameitwa au la ili asichanganye au kusahau ajira yoyote aliyoomba

3. Usajili ulipaswa kufanyika kila mkoa kulingana na wahusika walioomba kama wanapatikana. Na kama itakuwa ni ngumu, basi saili zifanyike katika kanda zote nchini. Hii itasaidia watu kumudu gharama za kusafiri na kufanya usahili.

4. Kuwe na machine ya utambuzi kwa namba za kutoka NIDA. Kutokana na changamoto mbalimbali za waombaji kutokuwa na vitambulisho au nyaraka za utambulisho, mwombaji anaweza kutumia namba ya NIDA kukamilisha utambulisho wake kwa sababu ni njia ya halali na ya kuaminika itakayo ondoa usumbufu katika zoezi la ukaguzi.

5. Waombaji wajulishwe matokeo ya kila hatua ya usahili hata usaili wa mahojiano kwa wakati. Kuna kipindi usahili unaweza kufanyika lakini matokeo yanatoka kesho yake. Napendekeza matokeo yatoke ndani ya siku moja kwa hatua zote za usahili. Hii itaepusha gharama za kuendelea kusubiri kutokana na wengi wao kusafiri kutoka mbali na makazi yao.
No.5 itakuwaje akati kuna wale wazee lazima wajiridhishe kuwa usaili ulienda vizuri(oral),haki ilitendeka na waridhie majina yote ya waliofaulu na kufeli?
 
Back
Top Bottom