HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mkuu mbingunikwetu naomba unisaidie kunielewesha hapo kwenye posho za kujikimu,, hapo walipoandika sehem nyingine. Hizo sehem ni zipi?

IMG-20230522-WA0009.jpg
 
Psrs sasa hv wamekuwa kama nabi na yanga yaan wanataka wazungumzwe wao tu....hizi stress za watu zingeshaisha kama MDA &LGA wangemaliza kuita mara moja maisha yaendelee...afu pia hako ka neno kanzi data wakatoe tu kasiweoo maana kanatukera sana kutumiwa kuundermine watu
 
Nimeongea kitu ambacho nilifanya na nikafanikiwa ( experience )
Ni sawa ni kumshauri mtu alale mlango wazi wakati wa joto ili kupata hewa kwa kuwa wewe uliwahi kufanya hivyo ukafanikiwa!! Au kumwambia mtu aibe kwa kuwa wewe uliiba ukafanikiwa!! Sijui hayo masomo uliyosoma kwa mtindo huo ni level ipi na kama ilihusisha field work ya karibuni mioezi miwili kila mwaka!! It is totally unimaginable!! The stakes are too high to afford such a risk and for no reasonable reasons!!
 
Mkuu mbingunikwetu naomba unisaidie kunielewesha hapo kwenye posho za kujikimu,, hapo walipoandika sehem nyingine. Hizo sehem ni zipi?

View attachment 2630963
Hizo sehemu nyingine ni sehemu zote ambazo si miji mikuu ya mikoa au miji mukuu ya wilaya. Kwa mfano kuna sehemu zina sifa ya kuwa miji midogo. Mfano: Mlandizi- Pwani, Kemondo-Bukoba, nk
 
Vipi kama nataka kuhama kada kwa kusoma open je naweza kusaidiwa gharama?
Ukihama kada huwezi kusaidiwa gharama. Lakini pia ukifanikiwa kupata shahada yako, mwajiri hataipa tuzo! Kwa mfano wewe ni mwalimu wa diploma. Kisha ukaomba ruhusa kwenda kusoma kwa kujigharimia mwenyewe halafu ukasoma shahada eg bachelor of commerce. Ukimaliza mwajiri ataendelea kukutambua kama mwalimu wa diploma tu. Lakini ukisoma Bachelor of commerce with education hapo mwajiri atakubadilishia muundo na kukutambua kama mwalimu mwenye shahada.

Mfano mwingine kama ulikuwa na shahada ya kwanza na ukaenda kusoma shahada ya pili ambayo haihusiani na shahada ya kwanza hautapewa zile nyongeza mbili za mshahara, na mwajiri hatakutambua kama mwajiriwa mwenye masters.

Lakini ukibadilisha kada lakini unajua mwajiri anaweza kuitumia hiyo kada yako mpya, hapo mwajiri anaweza kukubadilishia muundo/kukufanyia recategorization. Kwa hiyo unapoamua kusoma kada nyingine ni vizuri kuona kama hiyo kada mpya mwajiri anaweza kukutumia kwa kada hiyo mpya!! Ila hutamdai, itabidi uwe mpole na uombe wakati nafasi hiyo itakapopatikana.

Mfano wewe uliajiriwa na haslmashauri kama Clinical officer. Lakini ukaomba kwenda kusoma shahada ya pharmacy. Halmashauri yako ina uwezo wa kukutumia kwenye kada yako mpya ya pharmacy kwa hiyo ukiomba, na nafasi hiyo ikawepo hapo wanaweza kukubadilishia kada na majukumu.

Ila kama ukienda kusoma MD wakati ulikuwa clinical officer, hapo ukimaliza tu wanakutambua kama daktari.
 
Shukrani. Mimi pia nipo hapa ni afsa mstaafu katika utumishi wa umma. Nawatia moyo vijana kutokukata tamaa pia kuwaelezea taratibu, miongozo haki na wajibu wa waajiriwa katika utumishi wa umma.
Sawa @ Mbinguni kwetu nakumbuka kuna siku ulitoa maelezo ya stahiki za fedha ya kujikimu kwa mwajiriwa mpya ukasema kuwa malipo yanajumuisha pia watoto na mke au mume , usafiri wa mizigo na tiketi za safari, ila naona uhalisia wake sivyo ndivyo, mostly wanalipa tu rate kati ya Tsh 80,000 ×7 days au Tsh 100,000×7days na gharama ya tiketi tena hii ni mpaka uwe nayo, isipokuwepo ndio basi tena.
 
Ukihama kada huwezi kusaidiwa gharama. Lakini pia ukifanikiwa kupata shahada yako, mwajiri hataipa tuzo! Kwa mfano wewe ni mwalimu wa diploma. Kisha ukaomba ruhusa kwenda kusoma kwa kujigharimia mwenyewe halafu ukasoma shahada eg bachelor of commerce. Ukimaliza mwajiri ataendelea kukutambua kama mwalimu wa diploma tu. Lakini ukisoma Bachelor of commerce with education hapo mwajiri atakubadilishia muundo na kukutambua kama mwalimu mwenye shahada. Mfano mwingine kama ulikuwa na shahada ya kwanza na ukaenda kusoma shahada ya pili ambayo haihusiani na shahada ya kwanza hautapewa zile nyongeza mbili za mshahara, na mwajiri hatakutambua kama mwajiriwa mwenye masters.

Lakini ukibadilisha kada lakini unajua mwajiri anaweza kuitumia hiyo kada yako mpya, hapo mwajiri anaweza kukubadilishia muundo/kukufanyia recategorization. Kwa hiyo unapoamua kusoma kada nyingine ni vizuri kuona kama hiyo kada mpya mwajiri anaweza kukutumia kwa kada hiyo mpya!! Ila hutamdai, itabidi uwe mpole na uombe wakati nafasi hiyo itakapopatikana. Mfano wewe uliajiriwa na haslmashauri kama Clinical officer. Lakini ukaomba kwenda kusoma shahada ya pharmacy. Halmashauri yako ina uwezo wa kukutumia kwenye kada yako mpya ya pharmacy kwa hiyo ukiomba, na nafasi hiyo ikawepo hapo wanaweza kukubadilishia kada na majukumu. Ila kama ukienda kusoma MD wakati ulikuwa clinical officer, hapo ukimaliza tu wanakutambua kama daktari.​
Hiyo nyongeza mbili ya mshahara inakuaje
 
Sawa @ Mbinguni kwetu nakumbuka kuna siku ulitoa maelezo ya stahiki za fedha ya kujikimu kwa mwajiriwa mpya ukasema kuwa malipo yanajumuisha pia watoto na mke au mume , usafiri wa mizigo na tiketi za safari, ila naona uhalisia wake sivyo ndivyo, mostly wanalipa tu rate kati ya Tsh 80,000 ×7 days au Tsh 100,000×7days na gharama ya tiketi tena hii ni mpaka uwe nayo, isipokuwepo ndio basi tena.

Kiasi kamili cha posho ya kujikimu kwa siku kinategemea na 1. Ngazi ya mshahara 2. Hadhi ya mji ambako umepangiwa kituo. Kama ni graduate kwa ngazi ya TGS D ukapangwa mji ambao si mji mkuu wa mkoa au wilaya hapo ndipo utapata 80,000/= kwa siku, kama ni manispaa ni 150,000/=.

Kama una mke na watoto lazima uwe umeonesha kwenye fomu ya taarifa zako binafsi. Barua yako ya kuomba posho kwa mke na watoto lazima uambatanishe nakala ya cheti cha ndoa na nakala ya birth certificate za watoto na ziwe certified na wakili au mahakama. Hapo hakuna jinsi lazima wakupe, kama siyo sasa baadaye watakupa tu.

Kuhusu mizigo ni kweli waajiri wengi hawatoi, lakini huo ni uonevu kwa sababu waraka unaainisha wazi kuwa mwajiriwa mpya anastahili kulipiwa gharama ya MIZIGO YAKE BINAFSI/PERSONAL EFFECTS. Hakuna binadamu ambaye hana mizigo binafsi hata kama ni mwajiriwa mpya.

Ina maana hana kitanda, hana godoro, nk. Tatizo ni kwamba ni vigumu mwajiriwa mpya kukomalia haki zake hizi kwa kuogopa kuonekana mkorofi. Kwa mawazo yangu ni vizuri kuziomba kwa barua stahiki zako zote halafu wasipokulipa unakaa kimya kwa sasa, lakini madai yatakuwepo kwenye faili lako. Madai huwa hayaozi.

Baada ya miaka kadhaa kazini, na umeshazoea kazini unaweza kulianzisha tena.
 
Aisee hivi zile ajira za MDA &LGA zilizotoka mwezi wa nne wanaanza kuita watu kwa ajili ya interview lini aisee , mtaalamu wa ubashiri , bwana makofia
 
Back
Top Bottom