Kwanini utawala huu unafumbia macho kauli za kukufuru?

Kwanini utawala huu unafumbia macho kauli za kukufuru?

Kauli unaweza kuwa ina fanana na dini au dhehebu lako lakini aimanishi asiongee hii ni nchi huru
 
Katika uzinduzi unaoendelea sasa hivi amesikika mbunge Bona Kamori akisema "Mheshimiwa Rais sema neno moja tu na roho zetu zitapona".

Kwa sisi Wakatoliki kauli hii husemwa wakati ambao tunaamini Mungu ameshuka wakati wa mageuzi. Sala hii husomwa kwa Mungu mwenyewe tukiamini neno lake moja tu linaweza kuponyesha roho zetu.

Swali la kujiuliza ni je, huyu mama amefikia hatua ya kumpandisha Magufuli kufikia kumlinganisha na Mungu!? Kwanini kauli hizi za kukufuru zinafumbiwa macho na Rais mwenyewe ambaye ni mkatoliki na bila shaka anafahamu madhara ya kauli kama hizi!? Kwanini viongozi wa dini wapo kimya kukemea huu ujinga unaomea kwa kasi kubwa miongoni mwa wasaka tonge hawa wa kisiasa?

Pia kauli ya Makonda kuwa Rais pekee ndio mwanaume mwenye ujasiri nchi hii inamaanisha nini?
Chama cha kijani ni majinga sana kuna jinga lingine la Tabora huko lilisema Mungu amshukuru rais magufuri kwa kazi nzuri anazofanya, lingine likasema miujiza aliyoifanya rais Magufuri hata Yesu kristu hajawahi kuwafanyia wana wa Israel, lumumba zimejaa empty set a.k.a.tabulalasa.
 
Unajua nimecheka sana hapa
IMG-20190914-WA0028.jpeg
 
Huyu jamaa yetu ni mshamba Leo hii unaweza kumtukana matusi na kesho yake ukienda Kwa magoti kuomba msamaha Hana shida ilimradi umempigia magoti yaani Kwa kifupi anajiona MUNGU
Si kama mbowe anavyo jiona mungu mtu ndani ya chadema bila yeye chama akina uhai.
 
Hadi leo hujui kuwa ni mungu!!
Mleta uzi anashangaza sana. Watanzania tunapenda kujitoa akili,sijui kwanini. Yaani hajui simple fact kama hiyo, hasikii pia nyimbo za kumsifu na kumtukuza.
Wakati wa wimbi la wabunge wa chadema kuhamia ccm kuunga mkono juhudi, aliwaambia wapinzani wengine "njooni kwangu nyinyi nyote mlioelemewa na mizigo nami nitawapumzisha"....video clip ipo.
 
Chama cha kijani ni majinga sana kuna jinga lingine la Tabora huko lilisema Mungu amshukuru rais magufuri kwa kazi nzuri anazofanya, lingine likasema miujiza aliyoifanya rais Magufuri hata Yesu kristu hajawahi kuwafanyia wana wa Israel, lumumba zimejaa empty set a.k.a.tabulalasa.
Lakini ndio ukweli wenyewe mkuu.Wengi tunaamini hivyo.
 
bila shaka anafahamu madhara ya kauli kama hizi
Ndugu, Una uhakika gani kama Mheshimiwa Rais anafahamu madhara ya kauli hiyo?
By the way, sijaona shida ya hiyo kauli.

Japo kuwa kwa namna ambavyo umetafsiri uko sawa, na muheshimiwa Rais pia yuko sawa kwa namna alivyotumia.
 
Back
Top Bottom