Kwanini utawala huu unafumbia macho kauli za kukufuru?

Marisi schweini

Senior Member
Joined
Dec 3, 2018
Posts
130
Reaction score
374
Katika uzinduzi unaoendelea sasa hivi amesikika mbunge Bona Kamori akisema "Mheshimiwa Rais sema neno moja tu na roho zetu zitapona".

Kwa sisi Wakatoliki kauli hii husemwa wakati ambao tunaamini Mungu ameshuka wakati wa mageuzi. Sala hii husomwa kwa Mungu mwenyewe tukiamini neno lake moja tu linaweza kuponyesha roho zetu.

Swali la kujiuliza ni je, huyu mama amefikia hatua ya kumpandisha Magufuli kufikia kumlinganisha na Mungu!? Kwanini kauli hizi za kukufuru zinafumbiwa macho na Rais mwenyewe ambaye ni mkatoliki na bila shaka anafahamu madhara ya kauli kama hizi!? Kwanini viongozi wa dini wapo kimya kukemea huu ujinga unaomea kwa kasi kubwa miongoni mwa wasaka tonge hawa wa kisiasa?

Pia kauli ya Makonda kuwa Rais pekee ndio mwanaume mwenye ujasiri nchi hii inamaanisha nini?
 
Hivi huyo mama si ndio yule alipigwa divorce na mumuwe akamkataza asiendelee kutumia jina lake?
 
Bavicha mnakibarua kizito sana. Hivi hata hili nalo ni la kujadili?
 
Yeye ameona huyo ni Mungu kwake we shida yako Nini? Kwani we umewahi kuambiwa Mungu wa Bona Kamori ni Nani?
 
Katika uzinduzi unaoendelea sasa hivi amesikika mbunge Bona Kamori akisema "Mheshimiwa Rais sema neno moja tu na roho zetu zitapona".

Kwa sisi Wakatoliki kauli hii husemwa wakati ambao tunaamini Mungu ameshuka wakati wa mageuzi. Sala hii husomwa kwa Mungu mwenyewe tukiamini neno lake moja tu linaweza kuponyesha roho zetu.

Swali la kujiuliza ni je, huyu mama amefikia hatua ya kumpandisha Magufuli kufikia kumlinganisha na Mungu!? Kwanini kauli hizi za kukufuru zinafumbiwa macho na Rais mwenyewe ambaye ni mkatoliki na bila shaka anafahamu madhara ya kauli kama hizi!? Kwanini viongozi wa dini wapo kimya kukemea huu ujinga unaomea kwa kasi kubwa miongoni mwa wasaka tonge hawa wa kisiasa?

Pia kauli ya Makonda kuwa Rais pekee ndio mwanaume mwenye ujasiri nchi hii inamaanisha nini?
Pinga
Pinga
Pinga
Pinga

Mtawapinga hata wazazi wenu kuwa hawakuwazaa.
 
Kuna msemo mwingine wa " Utatu Mtakatifu" nao wanaupenda sana hao mahayawani, na wakati kwenye imani yetu unapoongelea Utatu Mtakatifu unaongelea Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu!

Hizo ndizo nafsi kuu tatu za Mungu.Na Utatu wetu huo kwa misingi ya kanisa Katoliki la Mitume, haujawahi kufananishwa na kitu kingine chochote kile! iwe duniani na hata mbinguni.
 
Yeye ameona huyo ni Mungu kwake we shida yako Nini? Kwani we umewahi kuambiwa Mungu wa Bona Kamori ni Nani?
Mbona hajasema ni Mungu? Hiyo ni kauli tu hakuna sehemu imeandikwa itumike kwa Mungu tu.
 
Kuna msemo mwingine wa " Utatu Mtakatifu" nao wanaupenda sana hao mahayawani, na wakati kwenye imani yetu unapoongelea Utatu Mtakatifu unaongelea Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu!

Hizo ndizo nafsi kuu tatu za Mungu.Na Utatu wetu huo kwa misingi ya kanisa Katoliki la Mitume, haujawahi kufananishwa na kitu kingine chochote kile! iwe duniani na hata mbinguni.
Wakatoliki huwa hatumind vitu vidogo vidogo, ili mradi suala halipo kimungu tunapuuza.
 
Huyu jamaa yetu ni mshamba Leo hii unaweza kumtukana matusi na kesho yake ukienda Kwa magoti kuomba msamaha Hana shida ilimradi umempigia magoti yaani Kwa kifupi anajiona MUNGU
 
Awamu hii tuna miungu wengi,kuna mungu wa dar a.k.a bashite na mungu wa lumumba a.k.a jiwe anaewapa uhai buku7 wa kuja kupost na kuchangia pumba humu jukwaani.
 
Bavicha mnakibarua kizito sana. Hivi hata hili nalo ni la kujadili?

Kwanini lisiwe la kujadili? Hivi hufahamu lugha kama hizo huchochea viongozi wang'ang'anie madarakani? Kama hizo lugha ni sawa, iweje kukitumika lugha kuwa ni dictator kilio kinakuwa kikubwa?
 
Upotoshaji lazima uwekwe wazi ili hao wanaotumia maandiko ya Mungu kinyume na utaratibu, kwa makusudi au kwa bahati mbaya watambue.
Hilo andiko la Mungu limeandikwa wapi kwenye biblia?
"Sema lolote na roho yangu itapona"
 
Back
Top Bottom