Katika uzinduzi unaoendelea sasa hivi amesikika mbunge Bona Kamori akisema "Mheshimiwa Rais sema neno moja tu na roho zetu zitapona".
Kwa sisi Wakatoliki kauli hii husemwa wakati ambao tunaamini Mungu ameshuka wakati wa mageuzi. Sala hii husomwa kwa Mungu mwenyewe tukiamini neno lake moja tu linaweza kuponyesha roho zetu.
Swali la kujiuliza ni je, huyu mama amefikia hatua ya kumpandisha Magufuli kufikia kumlinganisha na Mungu!? Kwanini kauli hizi za kukufuru zinafumbiwa macho na Rais mwenyewe ambaye ni mkatoliki na bila shaka anafahamu madhara ya kauli kama hizi!? Kwanini viongozi wa dini wapo kimya kukemea huu ujinga unaomea kwa kasi kubwa miongoni mwa wasaka tonge hawa wa kisiasa?
Pia kauli ya Makonda kuwa Rais pekee ndio mwanaume mwenye ujasiri nchi hii inamaanisha nini?