Kwanini unaruhusu mwili wako uitawale akili?

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Worth sharing!

Ndani ya verossa, unaweza kudhani ni gari ya kawaida, ila ndio humo alipopoteza bikira yake, utu na heshima yake.

Ndani ya verossa alitegemea kupata lifti ya kumpeleka nyumbani, humo ndimo alipoahidiwa kazi, maisha mazuri, na kila kitu.

Ndani ya verossa ndimo alipomvua nguo zake na kuzizima kabisa ndoto zake, ndimo alimopoteza degree yake anayoihangaikia mwaka wa tatu huu, haki ya kuwa mke wa mtu na familia.

Ndani ya verossa muathirika mwingine wa UKIMWI aliongezwa katika bajeti ya kuchukua dawa za kupunguza makali ya UKIMWI yaani ARVs. Alionekana ni mtu mzima mzuri tu, ana afya njema anaendesha Verossa hawezi kuwa na UKIMWI.

Ndani ya Verossa alimpa nafasi ya kumgusa, kumpapasa na kumpetipeti. Mshtuko na msisimuko wa raha ulipita katikati ya vena za mwili wake.

Ndani ya verossa alimvua top yake taratibu, ilipofika karibu na kichwa chake akakumbuka maonyo yote aliyokuwa akipewa na mama yake siku zote. Ndani ya verossa akafungua kifungo cha suruali yake ya 'skin jeans' akaacha avuliwe kirahisi kama anabadili nguo vile.

Ndani ya verossa, mama yako anajua? Kwamba mlikuwa siti za mbele sasa mmehamia siti za nyuma na gari mmepaki kwenye kichaka kidogo.

Ndani ya verossa kama gari yako vile msichana mdogo, miguu ukampanulia na kumuacha aiondoe kabisa. Hakuvaa hata 'protection' na hukumuuliza, ilikuwa raha ee?

Ndani ya Verossa ilikuchukua mwezi mmoja tu kugundua umebeba ujauzito, ulifikiri nini? Hapana siwezi kuwa na mimba! Hey haukusoma 'Reproduction' katika Biologia kidato cha tatu?

Ndani ya verossa, ukaenda kupima afya baada ya miezi miwili. Si ndicho ulichokuwa ukitegemea? Hatimaye ulifaulu vipimo. Ukakutwa na HIV postive yaani umeathirika, mimba ya miezi miwili na ghonorea.

Ndani ya verossa chuoni nako matokeo yakatoka umefeli una supplimentary nne pamoja na carry moja, kiufupi huna chuo tena!

Ndani ya verossa, ulitaka kumpigia aliyekusababishia hayo yote, lakini namba yake haipatikani, ameku block kila sehemu anaendelea kula maisha na warembo wengine.

Ndani ya verossa, unaweza kudhani ni gari ya kawaida, ila humo ndimo alimopoteza bikira yake, elimu yake, utu na heshima. Ndimo alimopoteza haki ya kuwa mke wa mtu.

Inside a Verossa you'd think its some sleek automobile, There she lost her virginity, her dignity and her guile!!!

Hakuna tunu kubwa duniani kama uhai na afya njema, mwenye kusoma asome sana, mwenye kazi afanye kazi kwa bidii, kila mtu ale kwa jasho lake, shortcut zina madhara makubwa sana!
 
Salaam wakuu,

Pamoja na salamu hizo niseme tu kwa kuanza nimefurahi kuona hii kitu imewekwa hapa imetafsiriwa. Ni faraja kuwa ujumbe uliokuwa umetarajiwa umewafikia wengi.

Hii meseji nilianza kuiona inasambazwa kwenye makundi ya whatsapp ikiwa imetafsiriwa hivi...nikafurahi lakini nikashtuka, 'mbona huyu mtafsiri haja-acknowledge mwandishi wa awali'?

Naomba ku declare kwamba mimi Mentor ndiye mwandishi halali wa shairi hili na nililiandika kwa kiingereza (kama mnavyoona paragraph ya mwisho alisahau kuifuta ikabaki kwa kiingereza)

Ninafurahi kuona kazi ninayofanya inapendwa na kuwafikia wengi lakini hata kusema kazi hii nimeitafsiri kutoka kwa Mentor si dhambi....walau umeonesha ujuvi wako wa kutafsiri lugha.

Kwa ushahidi thread yangu hii hapo;

Verossa

Cc: Paloma, Kaizer, mzee wa celica KakaKiiza, Asprin, Kaunga, KOKUTONA, King'asti, Kongosho, mshana jr, mwallu, Asnam, Mtambuzi (ile hadithi ya Tabata nayo waliifanya hivi hivi), everlenk, Paulo Sergio De Souz, RRONDO, @judgememt, cute b, Ntuzu, Belo, et al et al....
 
Binadamu wengine ni wabaya sana,hata Imani zao ndogo ivi mtu unajua umeadhirika kwanini unamfanyia mwenzio
ubaya kiasi hicho hata kumwambia?
 
Ndo hvyo ila wengi bado hawajifunzi mifano kutoka kw wenzao.wanawake wanakuw wahanga sn kw kutojua au kuiga.polen sn wadada maana nyie mnapata madhara zaid y mwanaume mnabebeshw bendi
 
Salaam wakuu,

Pamoja na salamu hizo niseme tu kwa kuanza nimefurahi kuona hii kitu imewekwa hapa imetafsiriwa. Ni faraja kuwa ujumbe uliokuwa umetarajiwa umewafikia wengi.

Hii meseji nilianza kuiona inasambazwa kwenye makundi ya whatsapp ikiwa imetafsiriwa hivi...nikafurahi lakini nikashtuka, 'mbona huyu mtafsiri haja-acknowledge mwandishi wa awali'?

Naomba ku declare kwamba mimi Mentor ndiye mwandishi halali wa shairi hili na nililiandika kwa kiingereza (kama mnavyoona paragraph ya mwisho alisahau kuifuta ikabaki kwa kiingereza)

Ninafurahi kuona kazi ninayofanya inapendwa na kuwafikia wengi lakini hata kusema kazi hii nimeitafsiri kutoka kwa Mentor si dhambi....walau umeonesha ujuvi wako wa kutafsiri lugha.

Kwa ushahidi thread yangu hii hapo;

Verossa

Cc: Paloma, Kaizer, mzee wa celica KakaKiiza, Asprin, Kaunga, KOKUTONA, King'asti, Kongosho, mshana jr, mwallu, Asnam, Mtambuzi (ile hadithi ya Tabata nayo waliifanya hivi hivi), everlenk, Paulo Sergio De Souz, RRONDO, @judgememt, cute b, Ntuzu, Belo, et al et al....
Furahia kazi yako ikisambaa ili watu wengi wa Jifunze
 
Mentor kwa kweli una kipaji cha utunzi.
Umenisisimua.

Nawaonea huruma wasichana wanao anza maisha. Wengine tulikulia kikoloni. Mwanaume akikutongoza unaanza kuwaza mama ataniua unakimbia. Naomba Mungu wanangu wanisikilize nitakacho wafundisha.
 
Back
Top Bottom