Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,495
- 5,531
Habari za wakati huu;
Leo nataka tuzungumzi kitu kinaitwa "Business Model"aka mfumo au muundo wa Biashara.Wajasiriamali wengi huwa wanakama katika Biashara kwa kujikita zaidi kujenga Biashara badala ya kujenga Business Model.Ndio maana wengi hujikuta wakifanya bashara za kuigizana bila kuwa na aina yoyote ya ubunifu.
Business MODEL nini.Business ni mfumo kamili wa kibiashara ambao unaonesha aina ya bidhaa/huduma,aina ya wateja,jinsi faida itavopatikana na jinsi ya kuhakikisha kwamba biashara inakuwa endelevu.Ili nieleweke vizuri nitatumia mfano wa duka la reja reja.Kwa kawaida katika maduka ya rejareja faida huwa ni kati ya asilimia 10 hadi 40 kwa bidhaa nyingi huku wastani wa bei ya bidhaa ukiwa ni kati ya shingi 50 hadi sh 40,000 kwa kutegemea aina ya bidhaa na mahali duka lilipo.Kwa kawaida Muuzaji akifanya mauzo ya TZS 1,000,000 basi faida yake itakuwa ni kati ya TZS laki 4 hadi laki moja.
Wastani wa Mauzo katika duka la rejareja ni asilimia kumi ya stock iliyopo.Yaani kama Kwenye duka lako kuna mzigo wenye thamani ya Milioni 10 basi unatakiwa mauzo yako kwa siku yasipungue TZS 1,000,000 ili uweze kuendesha biashara yako vizuri.Kama mauzo yako yakiwa chini ya hapo inamaana kwamba utakuwa unaingia gharama kubwa sana za kuhifadhi mzigo ambazo sio za lazima na ambayo inaweza kupelekea kupata hasara katika biashara yako.
Najua hii business model niliyoelezea hapa sio kila mtu ataielewa ila ninachotaka kusema ni kwamba unapokuwa na mzigo mkubwa dukani kwako na kwa mwezi hauzungusihi mara tatu basi ujue kuwa unafanya biashara ya kuhifadhi mzigo(Warehousing) na sio kuuza.Kwa kila siku mzigo unapokaa dukani kwako unakuingizia gharama za nafasi,ulinzi,na tarehe ya expiry inakaribia.Ni muhimu sana ulitambue hilo ili uweze kufanya biashara kwa kujiamini.
Business MOdel yako lazima izingatie gharama zote na malipo unayopata wewe.Unaweza kuwa unauza TZS laki 5 kila siku ambayo kwa mwezi ni sawa na milioni 15 kama unafanya kazi kila siku.Ila kama mzgo wako ulioko stoo unathamni ya milioni 200 basi unafanya biashara kichaa.
Karibuni tujadili zaidi kuhusu Business Model na jinsi ambavyo unaweza kufaidika kwa kuwa na Business MOdel nzuri katika Biashara yako