Kwanini umeme wa TANESCO unazimazima ovyo?

Kwanini umeme wa TANESCO unazimazima ovyo?

Kwanza mvua kunyesha na upepo si sababu za kukatika kwa umeme kama mvua hizo ni zakawaida. Lakini ninavyojua mimi mvua kama zinazidi kiwango kama TMA walivyotangaza juzi hata kama nguzo imejengwa Imara vipi mafuriko yakija itabebwa. Nini nguzo hata nyumba zinabebwa. Acha uongo


Kuhusu contractors najua si kazi ya Tanesco kuangalia ubora wa mkandarasi bali Bodi ya kusajili Wakandarasi CRB: TANESCO inaingia je hapo. Contractor mlevi ana tumbo. Kwani contractor ndiye anachimba nguzo. Ndio yeye anavuta waya?

Kukatika kwa umeme kipindi cha mvua na upepo mkali Inawezakana kwa sababu line za umeme nyingine zinapita maporini. Matawi au miti inaweza kuangukia line.

Wewe unaegemea upande wa lawama kwa kuwa Hujui. Lori likigonga nguzo ni tanesco wamekata? Watu wakiiba waya u a mafuta ya Transfoma ni tanesco wamekata? Mada nyingine bwana. So do research first. Au uliza
Juzi Mbagala nimekuta semi trailer imezoa nguzo na waya kama mita 5 sijui TANESCO walirudisha umeme saa ngapi

come on big bro...can you speak these infront of tz kua mikoa yote na wilaya zote hizo ndio genuine reasons za kukatika umeme hovyo????..
those are cheap responses......kama ndo ume-research ukahitimisha hivyo basi elimu ya risechi nayo ifanyiwe risechi ku justify its reliability na validity ya uwepo wake!
 
Hii zima washa ya umeme Tanesco mkituunguzia vitu tutawashitaki EWURA NA Mahakamani. Ni nani anafanya huu mchezo wa kuwasha na kuzima. Pili mmebutua na kutoboa sana mabomba ya maji sababu ya kuweka nguzo mpya bila uchimbaji wa uangalifu kwanini msingeshirikiana na dawasco kuwaeleza hapa chini kuna.mabomba maeneo mengi sasa yanavuja sababu ya nguzo zenu mpya.
 
Hii zima washa ya umeme Tanesco mkituunguzia vitu tutawashitaki EWURA NA Mahakamani. Ni nani anafanya huu mchezo wa kuwasha na kuzima. Pili mmebutua na kutoboa sana mabomba ya maji sababu ya kuweka nguzo mpya bila uchimbaji wa uangalifu kwanini msingeshirikiana na dawasco kuwaeleza hapa chini kuna.mabomba maeneo mengi sasa yanavuja sababu ya nguzo zenu mpya.
Geita toka saa kumi usiku mpaka sasa umezima.
 
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kwanini umeme wa TANESCO unazimazima ovyo kila mvua ikinyesha au upepo mkali ukivuma?

Swali hili lilianza kugonga kichwa changu tangu nikiwa kidato cha kwanza. Nakumbuka tukiwa kidato cha kwanza kama miaka 17 iliyopita uliibuka mjadala wakati tuko kwenye mapumziko juu ya swali hili. Tulikuwa tukiteseka sana kwani kusoma usiku wakati ule ilikuwa vigumu sana na wengi walilazimika kutumia miwani kwaajili ya kusoma kwa tochi.

Kwenye mjadala huo nilitoa jibu ambalo lilinifanya nichekwe sana na kuonekana muongo.
Ni kuchwekwa huko kulikonifanya kila ninapopata fursa niulize juu ya swala hili.

Mara niliambiwa kuwa wakati wa mvua na upepo nguzo huanguka na kusababisha tatizo hili. Ila bado nikajiuliza kama wawekaji wa nguzo huwa hawajui kama kuna upepo na mvua?

Majibu yameendelea kuwa mengi na maswali kuwa mengi zaidi kwani kila jibu limekuwa likizua maswali zaidi na kila swali likileta majibu mengi ya hovyo hovyo.

Leo nimepata fursa ya kujua angalau kidogo kwanini umeme wa TANESCO hukatika katika kila mara mvua ikinyesha au upepo ukipiga.

Nimekutana na contractor anayekubalika na TANESCO mwenye tumbo kubwa, kichwa kidogo, miguu midogo na akili kidogo.

Wadau huwezi amini, contractor huyu hajui kusoma wala kuandika ila anajua kuweka sahihi.

Sijui mfumo anaofanyia kazi lakini ni rahisi sana kujua kuwa ni mtu wa kupenda pombe na mizaha.Mtu huyu anayepewa miradi mpaka ya milioni mia, neno viwango ni msamiati mkubwa sana kwake.Yeye na mafundi wake kufanya kazi baada ya kulewa ni kitu cha kawaida sana.

ANAJUA NAMNA YA KUCHEZA NA MIRADI YAKE INAKUBALIKA KWA UKAGUZI SIFURI.

Nahisi nimepata jibu, japo sio la kitaalam sana.

Wadau naomba majibu zaidi kama yapo.

Kwa arusha wanasema wanahamisha nguzo kwa ajili ya Ujenzi wa barabara toka sakina mpaka Himo ni project ya Miaka Saba.
 
Umeme umeanza kusumbua tena kwa kukatika hovyo jijini Dar.
Nilijua kwa vile tumepata Rais mkali,hili tatizo sugu litakwisha,lakini kidogo kidogo tatizo linashika kasi.
 
Back
Top Bottom