Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,351
- 9,837
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kwanini umeme wa TANESCO unazimazima ovyo kila mvua ikinyesha au upepo mkali ukivuma?
Swali hili lilianza kugonga kichwa changu tangu nikiwa kidato cha kwanza. Nakumbuka tukiwa kidato cha kwanza kama miaka 17 iliyopita uliibuka mjadala wakati tuko kwenye mapumziko juu ya swali hili. Tulikuwa tukiteseka sana kwani kusoma usiku wakati ule ilikuwa vigumu sana na wengi walilazimika kutumia miwani kwaajili ya kusoma kwa tochi.
Kwenye mjadala huo nilitoa jibu ambalo lilinifanya nichekwe sana na kuonekana muongo.
Ni kuchwekwa huko kulikonifanya kila ninapopata fursa niulize juu ya swala hili.
Mara niliambiwa kuwa wakati wa mvua na upepo nguzo huanguka na kusababisha tatizo hili. Ila bado nikajiuliza kama wawekaji wa nguzo huwa hawajui kama kuna upepo na mvua?
Majibu yameendelea kuwa mengi na maswali kuwa mengi zaidi kwani kila jibu limekuwa likizua maswali zaidi na kila swali likileta majibu mengi ya hovyo hovyo.
Leo nimepata fursa ya kujua angalau kidogo kwanini umeme wa TANESCO hukatika katika kila mara mvua ikinyesha au upepo ukipiga.
Nimekutana na contractor anayekubalika na TANESCO mwenye tumbo kubwa, kichwa kidogo, miguu midogo na akili kidogo.
Wadau huwezi amini, contractor huyu hajui kusoma wala kuandika ila anajua kuweka sahihi.
Sijui mfumo anaofanyia kazi lakini ni rahisi sana kujua kuwa ni mtu wa kupenda pombe na mizaha.Mtu huyu anayepewa miradi mpaka ya milioni mia, neno viwango ni msamiati mkubwa sana kwake.Yeye na mafundi wake kufanya kazi baada ya kulewa ni kitu cha kawaida sana.
ANAJUA NAMNA YA KUCHEZA NA MIRADI YAKE INAKUBALIKA KWA UKAGUZI SIFURI.
Nahisi nimepata jibu, japo sio la kitaalam sana.
Wadau naomba majibu zaidi kama yapo.