Kwanini umejikataa hujikubali?

Kwanini umejikataa hujikubali?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habari wana MMU

Natumaini mko wazima ila wachache wanaoumwa nami nawaombea kwa Mungu awaponye,

Leo nimekuja na hoja hii ya baadhi ya watu ambao wanakuwa katika hali fulani ya maisha yaani wanapitia kipindi kigumu mpaka inafikia hatua ya wao kujikattaa na kujiona kuwa hawafai lolote na si chochote wanabalki wanyonge wasio na mbele wala nyuma wanabaki mtazamo wa kuona kila kitu hawawezi kabisa. Kila walifanyalo wanaona hawawezi na wanaishia kushindwa kutimiza zile ndoto zao waliaojiwekea hata wengine wanakufa na maono na ndoto zao pasipo kutimiza. Wengine kutokana na kukataliwa na watu au wenzi wao wa maisha wameona hakuna haya ya kuishi na wanajifupisha maisha yao, wamesahau kuwa uhai Mungu amewapa ili wamtukuze na kumshukuru yeye. Wamesahau kuwa yuko ambaye anaweza yote na ndiye mtetezi wa maisha yao. hebu soma hapa Jeremia 29:11 inasema 'Maana nayajua mawazo ninayowazia ninyi, asema Bwana , Ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu mwisho' Jeremiah 32:'Maana nayajua mawazo ninayowazia ninyi, asema Bwana , Ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu mwisho' na soma hapa 'Jeremiah 32:27 inasema'Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili; Je kuna neno Je kuna neno gumu lolote nisiloliweza' Kwake Mungu hakuna neno au jambo lolote litakalomshinda yeye kwake yote yanawezekana kama umekataliwa na Mchumba, Baba/Mama au Mume wako au rafiki yako wa karibu yuko yeye ambaye ni rafiki wa kweli na wala si mdanganyifu kwani Binadamu atasema leo anakupenda na kesho amebadilika amekuwa mwingine kabisa mpaka inafikia unajisemea moyoni si huyu ndiye aliyeniambia kuwa ANANIPENDA NA NI RAFIKI YANGU iweje leo amenikataa. Hivyo ndivyo binadamu walivyo wachukulie hivyohivyo na jifunze kuwasemehe kwani ni kigeugeu kabisa mwangalie Mungu ndiye rafiki yako wa kweli soma hapa Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake, 14' Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo [Yesu] BASI ondoka na dhana ya kujikataa kutokujikulbali kwani unaye RAFIKI WA KWELI naye ni Mungu Baba
 
Kweli dada umekuja kivingine!
Hebu nambie ushapona kabisa?
 
yaani nimeshapona kabisa tena sana nashukuru kwa maombi yenu nimepona na niko kwa job napiga mzigo hapa asante kaka Erickb52
 
Last edited by a moderator:
ni kweli Filipo usemayo ndugu yangu na anayekuwa rafiki wakweli ni Mungu pekee yake kwani wanadamu ni wanafiki tu tena sana watakuwa nawe leo kesho wanakuteta pembeni mtegemee Yesu peke ayake ndiye rafiki wakweli kwani umeamua kusema hivyo kaka yangu Filipo
 
Last edited by a moderator:
Eimeeeeeeeeeeen kaka Bishanga nasikia umemuacha mkeo hivi ni kweli au?
 
Last edited by a moderator:
ubarikiwe sana kwa mawazo mazuri na yenye maana kubwa sana katika mwanzo huu wa mwaka
Naomba nami nikutakie kila la heri katika kutimiza malengo yako na kutimiza kile ulichokiandika ladyfurahia
 
Last edited by a moderator:
nawe pia nakutakia kila la kheri ufanikiwe sana tena sana katika maisha upate watoto double double@stevoh
 
pole ni kazi nyingi nini mpendwa kaka Erickb52
 
Last edited by a moderator:
pole ni kazi nyingi nini mpendwa kaka Erickb52
 

Attachments

  • ring 2.jpeg
    ring 2.jpeg
    6.6 KB · Views: 21
Last edited by a moderator:
samahani sana kaka Erickb52 zile hazikukuhusu wewe nilitaka kumtumia mwingine zile ring sorry 4 that my bro
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana tena sana nawe nakutakia kheri na baraka katika shughuli zako pia katika familia yako Mungu akujalie upate watoto matwin doubledouble tena kwa mpigo
 
nawe pia barikiwa sana uzae na kuongeza hii dunia iwe yako stevoh
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom