Usivunje Uhusiano wako na Mungu

Usivunje Uhusiano wako na Mungu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,206
Reaction score
1,695
Yn 15:14 SUV
[14] Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.

Mtu yeyote kuwa na urafiki na mtu mwingine, lazima kuna maeneo waliona wanaendana.

Urafiki wetu au ushirika wetu na watu wengine hautoki hewani, unatokana na mahusiano yetu yaliyounganishwa na jambo fulani linaloendana.

Waamini tunakuwa jamii moja na familia moja kwa sababu tumeunganishwa na Kristo.

Kile kitu kilichotuunganisha kinapopotea, ule urafiki hufifia kisha kupotea kabisa.

Urafiki wetu na Yesu unakuja pale tunapomwamini na kuliishi neno lake, hapo tunakuwa na uhusiano mzuri sana naye.

Tunapotoka nje na hapo, urafiki wetu na Yesu huisha hapohapo, na hapo tunakuwa tumekaribisha marafiki wengine.

Kuharibu uhusiano wetu na Yesu ni jambo hatari sana kwa maisha ya mwamini, anaweza kuharibu maisha yake kwa kuanzisha urafiki na adui shetani.

Tunaweza kulinda uhusiano wetu na Yesu kwa gharama yeyote ile, tuhakikishe tupo vizuri na Yesu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
Amina mtumish.....
Mahusiano yangu na MUNGU ndio msingi wa maisha yangu.... kila ijumaa hua nachukua mda kutafakali mahusiano yangu na MUNGU na njia zangu... kama zimekwenda vyema machoni pa MUNGU.... hii imenisaidia sana kujua wapi nilikuwa nimeteleza... na kumuomba YESU ANITIE NGUVU¡¡
Barikiwa sana mtumish
Cc. Matunzo 02 njoo utie neno huku¡
 
Back
Top Bottom