Kwanini unene(obesity) unazidi kuongezeka kwa kasi sio Tanzania tu Dunia nzima

kamala 23

Member
Dec 20, 2018
17
24
KWANINI UNENE(OBESITY) UNAZIDI KUONGEZEKA KWA KASI SIO TANZANIA TU DUNIA NZIMA
Somo ili linaletwa kwenu na DR KAMALA

Janga la unene au uzito uliopitiliza limezidi kuongezeka kwa Kasi sio tu kwa watu wazima bali na kwa Watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.
Utumiaji wa sukari au itu vilivotengenezwa kwa sukari (soda,juice za madukani nk , umechangia Zaidi ongezeko la unene.
Sasa kwa namna ipi hii sukari usababisha unene.

Kabla ya kuendelea mbele msomaji atambue ili ,mwili nao ufanya jitihada wenyewe ili kuzuia unene.
Moja ya jitihada ni kuzalisha kichocheo au (hormone) ambayo inaitwa leptin
Hii inazalishwa na seli (fat cells) pale kiwango Cha mafuta mwilini kinapokuwa kikubwa , ili kupunguza hamu ya kula.

TUENDELEE
Sukari au (sucrose) imetengenezwa na glucose(50%) na fructose(50%). Nadhani neno glucose utakuwa umelisikia mala nyingi , lakini neno fructose litakuwa geni kama ukusoma sayansi.usijali wewe lichukue ivoivo tu.
Glucose na fructose zote zina madhara hasa pale zinapotumiwa kwa wingi , lakini fructose inamadhara makubwa Zaidi kuliko glucose.
Ukila sukari ,Kwenye utumbo mdogo inamengenywa na kuwa glucose na fructose. Glucose inaweza kutumiwa na seli yoyote kwenye mwili wa binadamu kwaiyo
Asilimia themanini (80%) ya glucose inaenda Kwenye matumizi mengine katika seli za mwili kama ubongo ,figo, misuli na viungo vingine vyote.
Asilimia ishilini (20%) ya glucose inaenda moja kwa moja Kwenye ini ambapo kiasi kikubwa ubadilishwa na kutunzwa kwenye Mfumo unaoitwa (glycogen), ili kutumika baadae kama hujala chakula kwa mda muafaka na kiwango kidogo sana
kinachobaki ubadilishwa na kupelekwa kwenda kwenye Mafuta ambayo sio mazuri kwa afya yaani (very low density lipoprotein [VLDL]) ambayo pia yakiwa mengi usababisha maradhi ya moyo.

Sasa ile FRUCTOSE haiwezi kutumiwa na seli nyingine yoyote japokuwa mmengeno wake unafanyika kwenye ini pekee. Kwaiyo fructose yote inayopatikana kwenye sukari, soda,juisi na matunda kama nanasi uenda moja kwa moja mpaka kwenye ini(Liver).

Fructose inamadhara gani basi.
Kwanza Kabisa tumbo uzalisha kichocheo kiitwacho (ghrelin) iki upelekwa kwenye ubongo na kusababisha mtu awe na hamu ya kula tunategemea mtu akila chakula hiki kichocheo kiache kutolewa lakini mtu akila vyakula vyenye fructose havizuii kutolewa kwa kichocheo iki ivo kuletea kuongezeka kwa hamu ya kula kila wakati na kupelekea unene.
Pia fructose inazuia kichocheo ambacho tumekiona apo juu kinachoitwa leptin kisifike kwenye ubongo hivyo kuongeza hamu ya kula kila wakati ata ukiwa mnene.
Mmengenyo wa fructose kwenye ini usababisha uzalishwaji kwa wingi Mafuta ambayo sio mazuri kwa afya yaani (very low density lipoprotein [VLDL]) ambayo pia yakiwa mengi usababisha maradhi ya moyo, unene ,Pia mengine hubaki kwenye ini na kusababisha Maradhi Kwenye ini ambayo baadae uletea usugu wa insulin (insulin resistance) ambayo baadae upelekea kisukari .
Pia mmengenyo wa fructose kwenye ini usababisha uzalishwaji wa uric acid ambayo nikisababishi kikubwa cha shinikizo la juu la damu[pressure] (hypertension) na ugonjwa unaoitwa gout.

NI VITU GANI BASI TUFANYE KUZUIA UNENE AU UZITO ULIPITILIZA
Achana na vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia sukari, achana na soda ,juisi za matunda.
Penda kula matunda kama yalivo maana ukitengeneza juice kwanza umetoa nyuzi nyuzi ambazo ni muhimu katika mmengenyo, Pia ukitengeneza juisi utajikuta umekula matunda mengi kwa wakati mmoja ambayo sio Salama kwa afya.
Vinywaji vyako viwe hasa hasa maziwa na maji. Maziwa sio yale yaliyokuwa processed viwandani.
Achana na vyakula vilivyokobolewa maana vyakula ivi havina nyuzi nyuzi (fibers) za kutosha kwaiyo mmengenyo wake ufanyika haraka na kusababisha hamu ya kula baada ya mda mchache.
Milo Yako ipishane masaa manne kwenda juu , ikiwezekana jizoeze kula milo miwili pekee kwa siku. Epuka Kula milo isiyo lasimi katikati ya milo lasmi, mfano ;mapochopocho( snacks)
Epuka kula chakula usiku mwisho wa kula chakula uwe saa mbili usiku.
Jizoeze kufanya mazoezi kila wakati.

KAMA WEWE UMESHAUPATA UO UNENE SOMO JINGINE LINAANDALIWA KWA AJILI YAKO
Screenshot%20(415).jpg
 
Mimi nataka ninenepe kidogo maana nimekuwa mwembamba sana
Njia ngani salama naweza kuitumia kuongeza uzito?
 
Mimi nataka ninenepe kidogo maana nimekuwa mwembamba sana
Njia ngani salama naweza kuitumia kuongeza uzito?

Kunywa bia kila siku kabla hujalala,hakikisha mlo wako haukosi nyama za kutosha,maziwa fresh unywe ya kutosha,hakikisha tumbo halipati njaa,vyakula vya wanga ule sana.
 
Back
Top Bottom