Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,077
Reaction score
831,700
Ni sayansi gani hii? Ni uchawi!? Ni mazingaombwe ama ni jambo la kufikirika tu lisilo na ukweli wowote?

Niliahidi kuleta mada hii, baada ya Dr. Shika kuchagiza kwenye simulizi yake ya kutoroka watesi wake kwamba hakumwangalia yule mtesi mlinzi aliyebaki naye machoni la sivyo jamaa angeamka!

Tujadili kipengele kwa kipengele.

A. Kwenye mada zilizopita za jicho la tatu, majinamizi na jicho la rohoni tuliona jinsi jicho la tatu lilivyo na nguvu pale macho yaonekanayo yakiwa yamefumba, yamelala.. Kumbuka jicho la tatu liko kwenye paji la uso.. Tunapozungumzia mawasiliano ya kiroho kiunganishi ni jicho hilo la tatu kwamba kuna muunganiko usioonekana kati ya jicho la tatu na jicho la tatu lingine...
Kama nilivyosema kwenye mada ya majinamizi na ndoto mbaya hatushauriwi kulala chali kwakuwa juu yetu zinapita roho nyingi na za kila aina, ambazo connection yake ni jicho hilo la tatu

B. Wachawi na wanga hutumia sana jicho la tatu kufanya mawasiliano ya kiroho na ndio maana wanapotaka kuingia ndani ya nyumba kwanza kuingia kinyume nyume kwa rivasi na wakiwa uchi... Hapa ni kuepusha uwezekano wowote wa wewe kuna na direct connection ya jicho la tatu na yeye... Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake... Lakini kwakuwa tayari ile connection ishakuwa established basi subconscious mind inakuwa alert na ndio mwanzo wa kukabana..
Jiulize kwanini wanaoingiliwa na popobawa hawana kipingamizi chochote, hujikuta tayari washachafuliwa..

C. Muingiliano mwingine wa jicho la tatu ni ndege kunguru mwewe, huyu ni ndege mwerevu na mwepesi sana huwezi kumpiga akiwa mbali, hivyo wajuzi huenda kinyume nyume mpaka kumkaribia kabisa ndio hugeuka na kumpelekea moto... Ukiweza kurudi rivasi kwa kunyooka, unaweza kumkaribia kunguru mpaka umbali wa mita tano.. Unaweza kufanya majaribio

D. Mwili wetu huu una mashine tatu moja ni conscious mind na nyingine ni subconscious mind na ya tatu ni unconscious mind
-conscious mind- ni hii hali tuliyo nayo ya kuweza kufanya kila kitu kwa utashi na bila utashi, kuandika kuongea kuvaa nguo nk nk, ni katika hali hii subconscious mind (jicho la tatu) nayo hufanya kazi.. Hii hufanya kazi ya ulinzi kuzunguka mwili wote na ndio maana huwa tunahisi kuna mtu anatunyemelea, kuna mtu yuko nyuma yetu ama kuna hatari inatukaribia.. Lakini vilevile hufanya kazi ya machale... Jicho la tatu huona zaidi ya kuona (seeing beyond) huwa tunapewa tahadhari na nafsi zetu, huwa tunasita kufanya jambo . hii ni kazi ya subconscious mind... Halafu kuna hali ile ya kuzirai ama kupoteza fahamu... Hii ndio unconscious mind... Macho yote mawili yamezima, jicho la tatu nalo linakuwa kwenye dormance state.. Lipo lakini utendaji hupungua uwezo mpaka kufikia chini ya asilimia 50 ili kulinda uhai kidogo uliobakia. Ni sawa na kukipunguzia mizigo chombo baharini kinachokaribia kuzama ili kisizame

Sasa tuhitimishe kwa suala la Dr Shika, aliachwa na mlinzi lakini akalala kutokana na uchovu pombe na madawa.. Lakini kwakuwa tayari ana ufahamu (inbuilt intuition) wa kumlinda Dr, hivyo hata alale vipi lile jukumu kiroho hubaki kwenye subconscious mind/jicho la tatu na ikitokea ukamwangalia usoni una establishe connection kati yako na yeye na kumfanya ashtuke na kuamka
ef5089328ced34d6ad19285ea79b58d6.gif

Mojawapo ya mafunzo ya walinzi ni hili.. Na subconscious mbili zinapokutana moja ndio hu trigger nguvu ya kuamsha nyingine.. Hivyo haishauriwi kabisa kukutanisha macho Kwenye situation kama hizi

Naomba radhi kwa kuchanganya lugha
 
Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake

Kwa hiyo ipi bora kati ya buluu na nyekundu?
Ufafanuzi tafadhali.
 
Zamani simba akikuvamia kwenye pango lako atakuja akikuangalia.ananyata ili udishtuke halafu anavamia.Inabidi uamke na ujilinde ontime.

Yani maisha yako kila siku yawe ya kuogopa kuvamiwa na Simba au wanyama wengine hatari Kama nyoka hutaacha kujifunza kuamka?

Mwindaji yoyote anajifunza kuangalia windo lake na windo mwenyewe anabidi ajifunze kujua anapoangaliwa.
Kwasababu kusikia ni rahisi zaidi kwa windo kushtuka inabidi mwindaji ajifunze kutoshtua windo lake kwa sauti.ila baadae windo akaanza kushtuka bila hata kusikia sauti.

Kwa hiyo mababu zetu waliogopa giza kwasababu hiyo na baada ya miaka na miaka waliweza kujenga intuition kujua kuna kitu kinamwangalia au kinakuja hata Kama yupo gizani.

Ndio Maana na sisi japokuwa hatujalala mapangoni tunashtuka kitu kikituangalia wakati tumelala.
 
Dah! Hatari sana.

Sasa Mshana, hizo roho si bora zikikuta umelala chali ili mpambane kwanza kuliko kukuta umelala ubavu na kufanya yao kwa urahisi?
Nijuze kidogo
Hapana ukiwa kwenye mlalo mzuri I mean mshazari ni ngumu sana mwanga kufanya yake... Ni mpaka aidha uwe chali ama kifudifudi... Sana sana atasonya na kuondoka zake
 
Unatuhakikishia vip juu ya hili mkuu ?
 
Hapana ukiwa kwenye mlalo mzuri I mean mshazari ni ngumu sana mwanga kufanya yake... Ni mpaka aidha uwe chali ama kifudifudi... Sana sana atasonya na kuondoka zake
Kama sijakuelewa vizuri mara ya kwanza umeeleza kwamba mchawi akikuta umelala chali hataweza kuwanga tena bali ataanza mapambano ya kukupindua lakini hapa umeeleza kuwa akikuta umelala mlalo mzuri ukimaanisha mshazari hawezi kufanya yake ukimaanisha hawezi kuwanga pia lipi ni lipi hapa mkuu?
 
Ni sayansi gani hii? Ni uchawi!? Ni mazingaombwe ama ni jambo la kufikirika tu lisilo na ukweli wowote?

Niliahidi kuleta mada hii, baada ya Dr. Shika kuchagiza kwenye simulizi yake ya kutoroka watesi wake kwamba hakumwangalia yule mtesi mlinzi aliyebaki naye machoni la sivyo jamaa angeamka!

Tujadili kipengele kwa kipengele.

A. Kwenye mada zilizopita za jicho la tatu, majinamizi na jicho la rohoni tuliona jinsi jicho la tatu lilivyo na nguvu pale macho yaonekanayo yakiwa yamefumba, yamelala.. Kumbuka jicho la tatu liko kwenye paji la uso.. Tunapozungumzia mawasiliano ya kiroho kiunganishi ni jicho hilo la tatu kwamba kuna muunganiko usioonekana kati ya jicho la tatu na jicho la tatu lingine...
Kama nilivyosema kwenye mada ya majinamizi na ndoto mbaya hatushauriwi kulala chali kwakuwa juu yetu zinapita roho nyingi na za kila aina, ambazo connection yake ni jicho hilo la tatu

B. Wachawi na wanga hutumia sana jicho la tatu kufanya mawasiliano ya kiroho na ndio maana wanapotaka kuingia ndani ya nyumba kwanza kuingia kinyume nyume kwa rivasi na wakiwa uchi... Hapa ni kuepusha uwezekano wowote wa wewe kuna na direct connection ya jicho la tatu na yeye... Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake... Lakini kwakuwa tayari ile connection ishakuwa established basi subconscious mind inakuwa alert na ndio mwanzo wa kukabana..
Jiulize kwanini wanaoingiliwa na popobawa hawana kipingamizi chochote, hujikuta tayari washachafuliwa..

C. Muingiliano mwingine wa jicho la tatu ni ndege kunguru mwewe, huyu ni ndege mwerevu na mwepesi sana huwezi kumpiga akiwa mbali, hivyo wajuzi huenda kinyume nyume mpaka kumkaribia kabisa ndio hugeuka na kumpelekea moto... Ukiweza kurudi rivasi kwa kunyooka, unaweza kumkaribia kunguru mpaka umbali wa mita tano.. Unaweza kufanya majaribio

D. Mwili wetu huu una mashine tatu moja ni conscious mind na nyingine ni subconscious mind na ya tatu ni unconscious mind
-conscious mind- ni hii hali tuliyo nayo ya kuweza kufanya kila kitu kwa utashi na bila utashi, kuandika kuongea kuvaa nguo nk nk, ni katika hali hii subconscious mind (jicho la tatu) nayo hufanya kazi.. Hii hufanya kazi ya ulinzi kuzunguka mwili wote na ndio maana huwa tunahisi kuna mtu anatunyemelea, kuna mtu yuko nyuma yetu ama kuna hatari inatukaribia.. Lakini vilevile hufanya kazi ya machale... Jicho la tatu huona zaidi ya kuona (seeing beyond) huwa tunapewa tahadhari na nafsi zetu, huwa tunasita kufanya jambo . hii ni kazi ya subconscious mind... Halafu kuna hali ile ya kuzirai ama kupoteza fahamu... Hii ndio unconscious mind... Macho yote mawili yamezima, jicho la tatu nalo linakuwa kwenye dormance state.. Lipo lakini utendaji hupungua uwezo mpaka kufikia chini ya asilimia 50 ili kulinda uhai kidogo uliobakia. Ni sawa na kukipunguzia mizigo chombo baharini kinachokaribia kuzama ili kisizame

Sasa tuhitimishe kwa suala la Dr Shika, aliachwa na mlinzi lakini akalala kutokana na uchovu pombe na madawa.. Lakini kwakuwa tayari ana ufahamu (inbuilt intuition) wa kumlinda Dr, hivyo hata alale vipi lile jukumu kiroho hubaki kwenye subconscious mind/jicho la tatu na ikitokea ukamwangalia usoni una establishe connection kati yako na yeye na kumfanya ashtuke na kuamka
ef5089328ced34d6ad19285ea79b58d6.gif

Mojawapo ya mafunzo ya walinzi ni hili.. Na subconscious mbili zinapokutana moja ndio hu trigger nguvu ya kuamsha nyingine.. Hivyo haishauriwi kabisa kukutanisha macho Kwenye situation kama hizi

Naomba radhi kwa kuchanganya lugha
nwezaje kutumiahilo li jicho uliloweka hapo kama avatar na likaendelea kuchezacheza hivyohivyo?
 
Hakuna ukweli wowote. Fix tu.
Jambo kama hili simple sana kuprove. Sijawahi kuangalia mtu usoni akiwa kalala akaamka, wengine hadi nawagusa kabisa bado wamelala.
Kama kawaida conspiracy theorists watajaa hapa na kushangilia kitu kipya bila kushughulisha bongo zao hata kidogo. Story hii haina basis yoyote ile, tungo tu
 
Kama sijakuelewa vizuri mara ya kwanza umeeleza kwamba mchawi akikuta umelala chali hataweza kuwanga tena bali ataanza mapambano ya kukupindua lakini hapa umeeleza kuwa akikuta umelala mlalo mzuri ukimaanisha mshazari hawezi kufanya yake ukimaanisha hawezi kuwanga pia lipi ni lipi hapa mkuu?
Ukiwa chali ni rahisi sana kukutanisha macho, hivyo wengi hujitahidi kukwepa hii na kufanya yao.. Ila ikitokea mmekutanisha macho vita huanzia hapo, ukilala kifudifudi ndio hapo kabisa hupanda mgongoni na kuanza kukuchezea kwa kadiri atakavyo
Lakini ukiwa mshazari hukosa pozi kabisa la kukuingia ila ni lazima uwe mshazari timilifu, kuna baadhi hupenda kulala nusu mshazari
ZAIDI ni kwamba hizi hali si lazima zimtokee kila mmoja wetu, unaweza kulala vyovyote vile na kisikupate chochote..... Ni sawa na kuambiwa kuwa ajali zinaua lakini ni wangapi wanapata ajali mbaya na kutoka bila hata mchubuko?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom