Ndugu zangu mimi kama vijana wengine ninafikiria kujenga nyumbani lakini Gharama za ujenzi ni kubwa sana na sijui vizuri sababu hasa ni nini? Miaka ya nyuma 1995-2000 nakumbuka gharama za ujenzi zilikuwa zinaendana na uchumi lakini sasa naambiwa Gharama za ajabu. Mimi kwa sasa naishi Texas na kiwanja kizuri chenye umeme, lami na maji ni $40,000 na ujenzi wa nyumba nzuri yenye A/C na vyumba vitano ni $90,000 na Gharama zote ni $130,000 kwa sehemu nzuri kabisa yenye shule nzuri sasa nyumba hiyo hiyo Tanzania naambiwa sehemu yenye umeme, barabara na maji zinaenda mpaka $50,000 kwa kiwanja na $100,000 kwa ujenzi wa nyumba ya standard ileile ya Texas. Sasa sijajua vizuri ni kwa nini Gharama zimeongezeka sana wakati zamani vitu vilikuwa vya UK, Ital na Dubai na gharama ilikuwa nogo kuliko sasa wakati wa vitu vya China