Kwanini Ujenzi ni Gharama sana Tanzania?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,550
8,643
Ndugu zangu mimi kama vijana wengine ninafikiria kujenga nyumbani lakini Gharama za ujenzi ni kubwa sana na sijui vizuri sababu hasa ni nini? Miaka ya nyuma 1995-2000 nakumbuka gharama za ujenzi zilikuwa zinaendana na uchumi lakini sasa naambiwa Gharama za ajabu. Mimi kwa sasa naishi Texas na kiwanja kizuri chenye umeme, lami na maji ni $40,000 na ujenzi wa nyumba nzuri yenye A/C na vyumba vitano ni $90,000 na Gharama zote ni $130,000 kwa sehemu nzuri kabisa yenye shule nzuri sasa nyumba hiyo hiyo Tanzania naambiwa sehemu yenye umeme, barabara na maji zinaenda mpaka $50,000 kwa kiwanja na $100,000 kwa ujenzi wa nyumba ya standard ileile ya Texas. Sasa sijajua vizuri ni kwa nini Gharama zimeongezeka sana wakati zamani vitu vilikuwa vya UK, Ital na Dubai na gharama ilikuwa nogo kuliko sasa wakati wa vitu vya China
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka.
Ingia Bongo kutafiti utaona kuwa hizo gharama unazopewa ni za ujanjaujanja tu.
 
Mkuu hizo gharama za viwanja hutegemea maeneo,ujenzi pia hutegemea ana ya materials.

1)Viwanja dar vinatofautiana sana kuna maeneo ni zaidi ya hata hiyo $50,000 lakini kuna maeneo ni chini hata ya $10,000 enep kubwa la kujimwaga.

2)Viwanja mikoani bei ni chini sana hata chini ya $5,000 na uwanja ni mkubwa.


Hivyo vyote vianategemea wewe umefocus kuwa na makazi wapi hivyo ndivyo vnadetermine gharama.

Ukija kwenye swala la ujenzi pia huenenda na mambo mengi;

-Aina ya makazi unayowish kuyajenga.

-Construction materials in general.

-Construction technology itayotumika kujengea.

-Size ya jengo lako pia linainfluence kweny gharama.

Kama ukipata wataalamu wazuri na waaminifu wakushauri huwezi kuogoga kujenga nyumba uitakayo nyumbani.

Labda ili tukupe picha ya nini unaweza kufanya ili kuejenga tuweke wazi unataka kujenga wapi kama ni dar au mkoani,taja na specific area i.e dar-mikocheni,kijichi,Tegeta n.k na kama Mwanza-Ilemela,ukerewe n.k

Taja aina za materials ungependa uzitumie.

unaweza aidha kutaja size ya jengo na picha kimuonekano,.
Japo tambua pia kuwa kuna mfumuko wa bei na shilingi yetu imekuwa ikishuka thamani mwaka hadi mwaka na asilimia kubwa ya vifaa vya ujenzi kwa asilimia kubwa vinatoka nje.

Nina hakika hutajiuliza mara nyingi juu ya ujenzi Nyumbani tanzania na kumbuka wengine hutake advantage ya kuwa unaishi ughaibuni hivyo una pesa za masihara.

Kila jema mkuu!
 
Naomba unutafutie kiwanja Texas mkuu. Na mimi ni miliki mjengo ughaibuni, kama bei ni poa kuliko bongo.
 
Naomba unutafutie kiwanja Texas mkuu. Na mimi ni miliki mjengo ughaibuni, kama bei ni poa kuliko bongo.

hata hivo kuna kamentality hapa bongo kwa wenye maduka na hata hawa mafundi,kwamba mtu akianza kujenga anazo, hivo bei za material zinapandaa kila kukicha na mafundi labour chajiwanaiweka juu bila sababu ya msingi, wakikuona mwanamke ndo kabisaaaa. Bora mtu ufany surveyya kutosha kabla hujaanza hizi shoping. Sijui wanafikir pesa tunaokota?
 
Tatizo la bongo maeneo yanayofaa kuishi, i mean yanayofikika ki urahisi na yenye huduma muhimu ni machache. Hii husababisha watu kugombania maeneo hayo na hivyo demand kuwa juu. Kwa mikoa mingi isipokua Dar na Arusha bado hali siyo nzuri sana.

Tatizo kubwa uendelezaji makazi na mipango miji zimeachiwa halmashauri ambazo hazina uwezo wa kufanya jukumu hilo na ni fisadi wa kutupwa.

Watu binafsi na makampuni wakianza kununua maeneo na kupima viwanja kwa wingi kama ilivyokuwa kwa mradi wa viwanja 20000 itasaidia sana kupunguza bei ya viwanja.

Kuhusu ujenzi, labor charges ziko juu kwa mafundi wazuri. Mafundi wengi ni wababaishaji, wazuri wako wachache hivyo automaticalu wanakua ghali.

Building materials nyingi zinatoka njee. Ingawa wakati mwingine bidhaa za nje ni nafuu kuliko zinazotengenezwa nchini.

Lakini pia miaka nenda rudi ujenzi wetu umekua ni wa kutumia matofali na cement. Ujenzi ambao ni ghali. Nafikiri kuna haja ya wataalamu wetu kubuni materials na njia bora zaidi za ujenzi kutumia material kama mbao, pvc na gypsum board.
 
nilifanya sana survey nikapata mafundi weenye bei halali, anaetaka fundi mason, fundi tiles, fundi rangi, fundi madirisha ( aluminium), fundi milango/furniture, kitchen,fundi umeme, plumper, gardener, fundi grill za madirisha,milango ....anione kwenye email pcocall@live.com . Utafurahi na hizi bei almost 30% - 40% down ya bei za wajanja. karibuni

Even Architecture and Engineer
 
Nadhani kuna input kubwa sana ya fedha haramu Tanzania.....fedha ufisadi/rushwa, madawa ya kulevya na biashara nyingine haramu zimefumua nidhamu uchumi wetu.
Kweli bei nyingine hazina mantiki kabisa.
 
nilifanya sana survey nikapata mafundi weenye bei halali, anaetaka fundi mason, fundi tiles, fundi rangi, fundi madirisha ( aluminium), fundi milango/furniture, kitchen,fundi umeme, plumper, gardener, fundi grill za madirisha,milango ....anione kwenye email pcocall@live.com . Utafurahi na hizi bei almost 30% - 40% down ya bei za wajanja. karibuni

Even Architecture and Engineer
Madalali ni tatizo lingine linalotomaliza. Kila kitu kina dalali.
 
Kupenda sifa tu, kuna matofali mazuri sn ya udongo bei rahisi sn. Nyumba nyingi sana south afrika zinajengwa nayo, uganda hata ulaya, nyumba ya milioni 20 unaijenga kwa chini ya kumi
 
Tanzania tunajenga majumba makubwa na yana vitu ambavyo wengine hardly kuvitumia.........balcony.........carpot......studyrooms
 
Tanzania tunajenga majumba makubwa na yana vitu ambavyo wengine hardly kuvitumia.........balcony.........carpot......studyrooms

Kwenye RED hiyo inahiotajika sana, Chumba cha wageni kwangu imegeuzwa Study ROOM, siyo Sebuleni mtoto anajitayarisha kwa ajili ya mtihani wenzie wanaangalia TV
 
Nimeona nyumba naambiwa ya milioni 150 hata AC system haima na Quality ni ya kawaida tu kwa mawazo yangu kuna katatizo hapa labda viwanda vya simenti, vigae, vioo, rangi etc havitoshi au kodi ya serikali na gharama za umeme ni juu sijui lakini sio realistic kuona gharama hizo kwa nchi inayotegemea misaada kama Tanzania!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom